
WANAMTANDAO wa kutetea Haki za Binaadamu (Human Rights Defenders Coalition -THRD), kwa kushirikiana na mashirika mengine wakiwemo FemAct, GDSS, wadau wa sekta ya habari, viongozi wa kiroho yaani masheikh mapadri na wachungaji, wanasheria na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu na wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT), wameandaa kongamano la masaa matatu (saa 4 asubuhi – saa 7 mchana). Kongamano hilo litafanyika Jumatano katika viwanja vya TGNP tarehe 12 Septemba 2012. Kama sehemu ya harakati zetu za kutetea haki za raia na haki za binadamu kwa ujumla tuomba ushiriki wa kila moja wetu tuunganishe nguvu ili kudai uwajibikaji kwa wahusika.
Nimefarijika sana na hatua zinazochukuliwa na WANAMTANDAO wa kutetea Haki za Binaadamu (Human Rights Defenders Coalition -THRD), kwa kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Tanzania inayoua raia kinyama siku hadi siku. Nami naungana nanyi kupinga vikali ukiukwaji wa haki za binadamu hapa Tanzania.
Kwa kweli wakati umefika kuwaelimisha watanzania wote tusimame na kupinga vikali dhuruma ya kukatishwa kwa maisha yetu kikatili.
Lo! angalia Tume ya ajabu ya waziri wa mambo ya ndani Emanuel Nchimbi isiyo na hata mishipa ya aibu wala hofu ya Mungu, ilivyo toa ripoti ya uongo yenye kuwalinda wauaji. Tunakwenda wapi? Haiwezekani katika hali hii tukabaki kimya. Lazima tupiganie haki zetu kwa pamoja.
Ahsante.
Adrehem Kayombo
Ubungo Kibangu
0753492827