
Na Mwandishi Wetu
MSANII nyota wa filamu Elizabeth Michael (18)ambaye anafahamika zaidi kwa jina la sanaa Lulu leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam akituhumiwa kwa kosa la kumuua msanii maarufu Steven Kanumba.
Lulu amefikishwa mahakamani majira ya saa tano na dakika 20 asubuhi na gari la Jeshi la Polisi ambalo linaonekana lilikuwa limebadilishwa namba za usajili. Gari hilo lilikuwa na namba za usajili T848DNV huku pembezoni katika vioo ikisomeka namba nyingine ya usajili PT 2565 aina ya Rav 4.
Lulu ambaye ni mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Agustina Mmbando.
Akisoma mashtaka hayo Wakili Kaganda alidaia mtuhumiwa (Elizabeth Michael) alitenda kosa hilo Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba Sinza Vatican jijini Dar es Salaam usiku.
Hata hivyo mtuhumiwa amepinga kuwa hana umri wa miaka 18 kama ilivyotajwa bali ana umri wa miaka 17. Mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea, na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 23, 2012.
mtoto asituchanganye kabisa, tunachotaka haki itendeke mara miaka 18 mara 17,tunaomba sheria ifuate mkondo wake…….
The crowd that came to Kanumba’s burial shocked everyone, and so the authorities are looking for a scapegoat. The dude fell and died of love heart attack, the girl was a miner and by wait comparison she cant push him down, leave alone causing death. The dude died before he even fell, so as many other sugar daddies.
Lulu kapelekwa mahakamani,je huo uchunguzi wa maini yake vp yanasumu?na vile vinywaji vina sumu?
mimi kama mdau wa filamu napenda kusema kuwa lulu anatakiwa kuchunguzwa kisaikologia na kutafutiwa mwanasheria atakaye muhoji kiundani zaidi ili kufahamu ukweli uko wapi. thanx
hata kama ana miaka 10 sheria ichukue mkondo,lulu ameiumiza tanzania
Najua wadau mna hasira sana kwa kumpoteza ndugu yetu Kanumba, nami naungana nanyi, ila naomba tuwe na subira wakati uchunguzi wa kifo chake cha utata unaendelea.