Iran yajaribu kombora jipya

WANAJESHI WA iRAN WAKIWA KATIKA GWARIDE LA KUMALIZA MAFUNZO

IRAN inasema imefanya jaribio la kurusha kombora la masafa ya wastani.
Jaribio hilo lilifanywa wakati wa mazoezi ya jeshi karibu na Hormuz, mlango unaounganisha Ghuba na Bahari ya Hindi.
Jeshi la wanamaji la Iran linasema siku ya mwisho ya mazoezi Jumatatu, meli zitaweza kupita kwenye njia ya Hormuz, ikiwa tu jeshi hilo litaziruhusu.

Mkondo wa Hormuz ni njia inayopitwa na meli nyingi zinazobeba mafuta, na Iran inatishia kuifunga endapo itawekewa vikwazo zaidi.

-BBC

Related Post

One thought on “Iran yajaribu kombora jipya

  1. Iran inayo haki ya kujaribu makombora yake na haitakiwi hatua hiyo kuchukuliwa kama kitisho kwa mataifa ya amani,lakini ni kitisho kwa mataifa ya uadui.na huo ni ujumbe kwa mataifa hayo kwamba wakati wowote yatakapojaribu kufanya kosa kuishambulia Iran basi inatakiwa yajiandae kuchakazwa maana makombora hayo yanakwenda kwa jina la “Iranian Missile Destroyers”.

    Makombora hayo yana vifaa vya kisasa vya kukwepa kuonekana na rada, yana uwezo wa kufuata shabaha hata inayokwenda kwa kasi kubwa sana, na mara inapoigundua, huongeza kasi na kuichakaza kwa kuitungua.

    Link hiyo:http://www.imamtaqee.com/index.php?option=com_content&view=article&id=625:1&catid=7:1&Itemid=10

Comments are closed.