IBF Yateua Makamu Rais Wanne Kuongoza Bondia Kimataifa

Mchezo wa bondia kimataifa
Mchezo wa bondia kimataifa

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) limepanua wigo wake wa kusimamia na kuratibu mchezo wa ngumi Bara la Afrika, Mashariki ya kati, Ghuba ya Urarabu na Uajemi baada ya kuteuwa viongozi zaidi (makamu rais) kusimamia mchezo huo maeneo anuai.

Miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vijana wengi kujiunga na ngumi na hivyo wengi kuhitaji huduma za shirikisho la IBF na ili kujiweka vizuri katika nafasi ya kutoa huduma inayotakikana, IBF imewateua makamu wanne wa rais watakaomsaidia Rais wa IBF.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa IBF, Onesmo Ngowi, inaeleza uongozi huo umewateua Ayman Saad Bait-Saleem wa Oman (Fedha), William Steven Kallaghe (Masoko Utawala), Henry Mann-Spain wa Ghana (Oparesheni) pamoja na Louaa Debes wa Misri.

Taarifa inasema viongozi hao wameteuliwa kulingana na ukaribu wa wahusika kwenye mchezo wa ngumi, nafasi aliyonayo muhusika kwenye jamii, ukaribu wake na vijana, uwezo wake kielimu pamoja na mchango kwa michezo huo.

Akifafanua sifa zao alisema Ayman ni mhandisi mwenye shahada ya uzamili kutoka katika chuo kikuu cha Karolina ya Kusini (University of South Carolina, Colombia South Carolina, USA.) mwa nchi ya Marekani. Amewahi kufanya kazi kama Meneja Mkuu wa Bandari ya Sultan Qaboos kwa miaka mingi, Meneja wa kampuni ya APL Moller Group ya Denmark nchini Oman, Kampuni ya Marekani ya ushauri wa Kihandisi na nyingine nyingi. Kiongozi huyo kwa sasa Ayman ni mfanyabishara mwenye kampuni nyingi nchini Oman mojawapo ikiwa ni AL SWAYNI SPORT SERVICES katika jiji la Muscat, Oman

Aidha alisema William ni msomi aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Utawala na alisoma katika chuo kikuu cha Budapest, Hungary. Ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya uchumi na masoko na amefanya kazi na makampuni kadhaa kama Mkurugenzi Mkuu wa benki ya kiislamu ya NBC, Meneja Miradi wa benki ya CRDB, Meneja wa Masoko wa Kanda wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kabla ya kuhamishia ujuzi wake kama Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya NBC.

“Henry ni mfanyabishara aliyeboboea kwenye biashara mbalimbali na analimiki makampuni makubwa ya kutengeneza bidhaa za kilimo kama nguo na vyakula vya kugandishwa (Frozen Food). Ana Shahada ya Uzamili wa Biashara (MBA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Harvard kilichopo katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani. Henry amefanya kazi kwa miaka mingi na mashirika ya kimataifa yakiwamo UNHCR, ILO na UNDP.

Aliongeza kuwa kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Golden Crescent Ltd yanayojishughulisha na kutengeneza bidhaa kutoka kwenye mazao ya mifugo na kilimo nchini Ghana na kuyauza nchi za Ulaya, Marekani na Asia. Kwa upande wa Louaa alisema ni mfanya biashara anayeishi katika jiji la cairo nchini Misri na ana uzoefu nkubwa kweney masuala ya biashara za kutengeneza nguo.

Louaa Debes pia amesoma biashara kwenye Chuo Kikuu cha Cairo na amefanya kazi na taasisi za serikali kabla ya kuanzisha shughuli za biashara. Debes anamiliki makampouni ya ulinzi, maduka makubwa (Super markets) pamoja na kamouni ya ukodishaji wa magari.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.