Blogs Tanzania | News |  Michuzi ya Habari leo

 

TUSKER, PORTS zakamilisha timu Kombe la Kagame

Tusker ya Kenya na Ports ya Djibouti zinawasili leo jioni kukamilisha idadi ya timu kumi na moja zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Kagame yanayoanza kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi za kesho ni APR ya Rwanda dhidi ya El Salam Wau ya Sudan Kusini itakayoanza saa 8 kamili mchana na kufuatiwa na ya saa 10 kamili jioni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Atletico ya Burundi.

Timu zote kutoka nje ya mazoezi zimeshapangiwa viwanja vya mazoezi ambapo zitavitumia kwa mujibu wa ratiba ambayo imepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makazi ya timu hizo na viwanja vya mazoezi ni kama ifuatavyo;

Timu: Uwanja wa mazoezi: Accommodation:
APR (Rwanda) Mabibo Hostel – Marriott Hotel (Mabibo External)
AS Vita (Congo) University of Dar es Salaam – Chichi Hotel (Kinondoni)
Atletico (Burundi) Mabibo Hostel – Lunch Time Hotel (Mabibo Hostel)
Azam (Tanzania) Azam Complex – Azam Complex (Chamazi)
El Salam Wau (S. Sudan) Zanaki Sekondari – Rungwe Hotel (Kariakoo)
Mafunzo (Z’bar) Kinesi – Rombo Green View Hotel (Sinza)
Ports (Djibouti) Kinesi – Rombo Green View Hotel (Sinza)
Simba (Tanzania) ……………………. – Vina Hotel (Mabibo Makutano)
Tusker (Kenya) Zanaki Sekondari – Rungwe Hotel (Kariakoo)
URA (Uganda) Loyola – Valentino Royal Hotel (Kariakoo)
Yanga (Tanzania) …………………. – ……………………….

Short URL: http://www.thehabari.com/?p=20152

Posted by on Jul 14 2012. Filed under Michezo na Burudani. You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. You can leave a response or trackback to this entry

Leave a Reply

*

 

 

Log in |

 

Google+