Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania http://www.thehabari.com Habari Tanzania | Online Newspaper Wed, 04 May 2016 18:33:44 +0000 en-US hourly 1 http://wordpress.org/?v=4.2.7 Azam Yabanwa,Yanga Sasa Ishindwe Yenyewe Kubeba Ndoo http://www.thehabari.com/azam-yabanwayanga-sasa-ishindwe-yenyewe-kubeba-ndoo/ http://www.thehabari.com/azam-yabanwayanga-sasa-ishindwe-yenyewe-kubeba-ndoo/#comments Wed, 04 May 2016 18:33:44 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71359 Baada ya Azam FC imepoteza matumaini ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ...

The post Azam Yabanwa,Yanga Sasa Ishindwe Yenyewe Kubeba Ndoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Azam FC Kukabidhiwa Kombe Kesho, Yanga na Simba Patashika...!

Baada ya Azam FC imepoteza matumaini ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

kwa Matokeo hayo yanamaanisha kwamba, Yanga wanahitaji pointi tatu pekee ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine ya Ligi Kuu.

Sare hiyo inaifanya Azam FC ijiongezee pointi moja na kufikisha 60 baada ya kucheza mechi 27 na inaweza kumaliza na pointi 69 ikishinda mechi tatu za mwisho, wakati Simba yenye pointi 58 inaweza kumaliza na pointi 70 ikishinda mechi zake nne zilizobaki.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Azam Yabanwa,Yanga Sasa Ishindwe Yenyewe Kubeba Ndoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/azam-yabanwayanga-sasa-ishindwe-yenyewe-kubeba-ndoo/feed/ 0
Rais Dk Magufuli Amkumbuka Asha-Rose Migiro http://www.thehabari.com/rais-dk-magufuli-amkumbuka-asha-rose-migiro/ http://www.thehabari.com/rais-dk-magufuli-amkumbuka-asha-rose-migiro/#comments Wed, 04 May 2016 18:08:23 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71355 Jiunge nasi kwenye social media Facebook Instagram Youtube Twitter

The post Rais Dk Magufuli Amkumbuka Asha-Rose Migiro appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
ASHA

taarifa

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Rais Dk Magufuli Amkumbuka Asha-Rose Migiro appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/rais-dk-magufuli-amkumbuka-asha-rose-migiro/feed/ 0
‘GREEN VOICES’ Sauti za Akinamama Wapambanao na Mabadiliko ya Tabia Nchi http://www.thehabari.com/green-voices-sauti-za-akinamama-wapambanao-na-mabadiliko-ya-tabia-nchi/ http://www.thehabari.com/green-voices-sauti-za-akinamama-wapambanao-na-mabadiliko-ya-tabia-nchi/#comments Wed, 04 May 2016 15:07:16 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71352 WANAWAKE wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa jinsi ...

The post ‘GREEN VOICES’ Sauti za Akinamama Wapambanao na Mabadiliko ya Tabia Nchi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Universitad Automous De Madrid, mara baada ya kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid, Spain hivi karibuni.

Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Universitad Automous De Madrid, mara baada ya kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid, Spain hivi karibuni.

WANAWAKE wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na mradi huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama María Teresa Fernández de laVega.

Taasisi hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao ambao kati yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza mradi mmoja, huku waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za akinamama hao kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira (EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika mikoa sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani ukihusisha miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.

Mratibu wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza miradi ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro.

Miradi mingine ni usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga na kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro.

Mradi huo unaotarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja unatoa fursa kwa kinamama kutoa ujuzo wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao kusikika. Hiyo ni kwa sabuabu kinamama wana uhusiano mkubwa na mazingira kutokana na kazi wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa familia kuhusiana moja kwa moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Wakiwa Madrid nchini Spain walikopata mafunzo wa wiki mbili katika chuo kikuu cha Autonomus Universitad De Madrid, akinamama hao na waandishi wa habari walijifunza kwa nadharia na vitendo jinsi nchi ya Spain inavyokabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuona njia ambazo na huku nchini zinaweza kutumika kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mafunzo kwa vitendo pia yalihusisha ziara za mafunzo kujifunza kilimo hai, na jinsi nishati jua inavyoweza kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Waandishi wa habari pia walipata nafasi ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti la Serikali ya Sapin la El Pais an kujifunza zaidi jinsi waandishi wa huko wanavyoandika habari zihusianazo na mabadiliko ya tabianchi.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post ‘GREEN VOICES’ Sauti za Akinamama Wapambanao na Mabadiliko ya Tabia Nchi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/green-voices-sauti-za-akinamama-wapambanao-na-mabadiliko-ya-tabia-nchi/feed/ 0
Mitandao ya Kijamii Yatishia Amani Magazeti ‘Print Media’ http://www.thehabari.com/mitandao-ya-kijamii-yatishia-amani-magazeti-print-media/ http://www.thehabari.com/mitandao-ya-kijamii-yatishia-amani-magazeti-print-media/#comments Wed, 04 May 2016 13:55:57 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71345 TAARIFA ya utafiti inaeleza kuwa vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti ...

The post Mitandao ya Kijamii Yatishia Amani Magazeti ‘Print Media’ appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mitandao ya Kijamii Yatishia Amani Magazeti 'Print Media'

TAARIFA ya utafiti inaeleza kuwa vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti vinakufa kadri teknolojia ya upatikanaji habari inavyo kuwa. Hivi sasa vyombo vingi vya aina hiyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu na mdororo wa mapato upandea wa matangazo jambo linalovilazimu kupunguza wafanyakazi. 

Kwa mujibu wa utafiti wa ‘Pew Research Centre’ unabainisha kuwa wakati idadi ya wasomaji wa habari za magazeti ya kawaida ‘wamakaratasini’ ikishuka, idadi ya wasomaji wa habari za mtandaoni inazidi kukua huku wanaoperuzi mtandaoni  kuonekana hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando. 

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba vyombo vya habari vya magazeti (print media) ‘makaratasini’, Digitali na TV, vimeonesha dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kutoweka. 
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa ‘print media’, ambapo gazeti kubwa la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali na idadi ya wasomaji wa mitandaoni. 
 Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni changa sana kuweza kutishia amani ya magazeti. 
Lakini kwa upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti. 
Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
“Ni kweli kwamba Tanzania ni bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uwongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji”, amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mitandao ya Kijamii Yatishia Amani Magazeti ‘Print Media’ appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mitandao-ya-kijamii-yatishia-amani-magazeti-print-media/feed/ 0
Serikali Yamfungia Snura na Chura wake http://www.thehabari.com/serikali-yamfungia-snura-na-chura-wake/ http://www.thehabari.com/serikali-yamfungia-snura-na-chura-wake/#comments Wed, 04 May 2016 13:25:30 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71346 Serikali kupitia Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo imesitisha kuchezwa kwa ...

The post Serikali Yamfungia Snura na Chura wake appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
snura-234

Serikali kupitia Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo imesitisha kuchezwa kwa wimbo na video ya Chura ya msanii Snura Mushi kwenye vyombo vyote vya habari nchini mpaka itakapofanyiwa marekebisho.

Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini na msemaji wa Wizara ya Habari Zawadi Msalla alisema video ya wimbo huo inadhalilisha utu wa mwanamke na inaifanya jamii ianze kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya sanaa kwa ujumla.

“Tumeufungia wimbo na video yake kuchezwa redioni, kwenye runinga, baa au sehemu yoyote ya wazi na yenye mkusanyiko wa watu wengi.

” Tunamtaka Snura aitoe video hiyo YouTube mara moja ili isiendelee kutazamwa na watu wengi kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo,”alisema Msalla.

Aidha Serikali inawakumbusha wananchi wote kutojiingiza katika makosa ya mtandao kwa kusambaza wimbo huo kwa njia yoyote ile ya mtandao.

Pia Serikali inavitaka vyombo vya habari viwe vya kwanza kuchuja maudhui ya kazi yoyote ya sanaa kabla ya kuwa mawakala wa uharibifu kwa jamii kupitia kucheza kazi chafu za wasanii.

Wakati huo huo Serikali imemfungia msanii Snura kujihusisha na masuala ya muziki mpaka atakapojisajili katika Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Serikali Yamfungia Snura na Chura wake appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/serikali-yamfungia-snura-na-chura-wake/feed/ 0
Simba Mkosi Juu ya Balaa, Michuano ya Basin Imepigwa Chini http://www.thehabari.com/simba-mkosi-juu-ya-balaa-michuano-ya-basin-imepigwa-chini/ http://www.thehabari.com/simba-mkosi-juu-ya-balaa-michuano-ya-basin-imepigwa-chini/#comments Wed, 04 May 2016 08:54:54 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71343 Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeahirisha michuano ya kuwania ...

The post Simba Mkosi Juu ya Balaa, Michuano ya Basin Imepigwa Chini appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
MASHABIKI-SIMBA

Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeahirisha michuano ya kuwania Kombe la nchi unakopita Mto Nile ‘Nile Basin Cup’.

Taarifa iliyotumwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye inasema kwamba wamepata taarifa za kuahirisha michuano hiyo kutoka kwa waratibu wakiwamo wenyeji Sudan.

Taarifa imesema wamekubaliana kuahirisha mpaka hapo watakapotangaza tena hivyo Simba iliyoteuliwa na TFF kushiriki michuano hiyo, imetaarifiwa kusubiri tarehe mpya ya mashindano.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Simba Mkosi Juu ya Balaa, Michuano ya Basin Imepigwa Chini appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/simba-mkosi-juu-ya-balaa-michuano-ya-basin-imepigwa-chini/feed/ 0
Uchaguzi wa Yanga Kufanyika Juni 25 http://www.thehabari.com/uchaguzi-wa-yanga-kufanyika-juni-25/ http://www.thehabari.com/uchaguzi-wa-yanga-kufanyika-juni-25/#comments Wed, 04 May 2016 08:46:25 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71340 Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza Uchaguzi Mkuu ...

The post Uchaguzi wa Yanga Kufanyika Juni 25 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
yanga

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga kuwa utafanyika Juni 25, 2016 badala ya Juni 5, 2016.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imelazimika kufanya hivyo kwa kuzingatia ushiriki wa Yanga ambayo inashiriki michuano ya kimataifa.

Sekretarieti ya Yanga ambayo ingefanya kazi kwa pamoja na Kamati ya Uchaguzi kwa kushirikiana na TFF kwa sasa inashughulikia pia kuiandaa timu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Yanga inatarajiwa kucheza na Esperanca ya Angola katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Mei 7, mwaka huu kabla ya kurudiana kati ya Mei 17 na 18, mwaka huu huko Angola.

Kwa mujibu wa ratiba mpya, fomu za kuwania uongozi wa Yanga zitaanza kuchukuliwa Mei 25, 2016 na kwamba uchaguzi huo utafanyika ndani ya muda ambao Serikali kwa kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) iliagiza uchaguzi kufanyika kabla ya Juni 26, 2016 hivyo uchaguzi utafanyika ndani ya wakati.

Katiba itakayotumika ni ya mwaka 2010 na kwamba Wanachama wa Yanga watatumia kadi za kawaida za uanachama na si za benki.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Uchaguzi wa Yanga Kufanyika Juni 25 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/uchaguzi-wa-yanga-kufanyika-juni-25/feed/ 0
Rais Magufuli Ashiriki Kikao cha Halmashauri Kuu CCM Taifa http://www.thehabari.com/rais-magufuli-ashiriki-kikao-cha-halmashauri-kuu-ccm-taifa/ http://www.thehabari.com/rais-magufuli-ashiriki-kikao-cha-halmashauri-kuu-ccm-taifa/#comments Tue, 03 May 2016 21:54:37 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71333 Jiunge nasi kwenye social media Facebook Instagram Youtube Twitter

The post Rais Magufuli Ashiriki Kikao cha Halmashauri Kuu CCM Taifa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Rais Magufuli Ashiriki Kikao cha Halmashauri Kuu CCM Taifa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/rais-magufuli-ashiriki-kikao-cha-halmashauri-kuu-ccm-taifa/feed/ 0
Dk Kigwangalla Kumsomesha Mtoto Aliyeiwakilisha Tanzania UN http://www.thehabari.com/dk-kigwangalla-kumsomesha-mtoto-aliyeiwakilisha-tanzania-un/ http://www.thehabari.com/dk-kigwangalla-kumsomesha-mtoto-aliyeiwakilisha-tanzania-un/#comments Tue, 03 May 2016 21:41:28 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71325 TAASISI ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla inayomilikiwa na Naibu Waziri ...

The post Dk Kigwangalla Kumsomesha Mtoto Aliyeiwakilisha Tanzania UN appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mwanzilishi wa Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha moja na Getrude Clement ambaye atalipiwa ada ya kidato cha tano na cha sita.

Mwanzilishi wa Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha moja na Getrude Clement ambaye atalipiwa ada ya kidato cha tano na cha sita.

Dk Kigwangalla Kumsomesha Mtoto Aliyeiwakilisha Tanzania UN

TAASISI ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla inayomilikiwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla imejitolea kumlipia ada mtoto Getrude Clement kwa kumsomesha kidato cha tano na sita ikiwa ni kutambua mchango wa mtoto huyo kuliwakilisha taifa.

Uamuzi huo wa kumsomesha Getrude umekuja baada ya mtoto huyo kukaribishwa kuzungumza kwenye kikao cha wabunge watetezi wa haki za watoto ambapo Getrude alipata nafasi ya kutoa historia yakee ambayo iliwatoa baadhi ya wabunge machozi.

Getrude aliwaeleza wabunge historia yake na hali yake ya kimaisha na kusema kuwa baba yake ni kinyozi na mama yake anafanya biashara ndogo ndogo za nyanya na vitunguu lakini bado amekuwa akijtuma katika masomo yake ambapo kwa sasa yupo kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Mnarani, Mwanza.

Baada ya kusema hivyo ndipo Dk. Kigwangalla aliamua kujitoa kumsaidia mtoto huyo ili aweze kujiendeleza zaidi kielimu na kufikia malengo yake na zaidi akiahidi kumsomesha katika shule za kisasa ili apate elimu bora zaidi.

“Kwa kuthamini kipaji chake na mchango wake na kutambua nafasi yangu kama Naibu Waziri kwenye Wizara inayosimamia mambo ya Watoto na kama mbunge na mzazi wa mabinti, lakini zaidi kama mtu kutoka kwenye background ya maisha ya chini na ninayethamini mchango wa elimu kwenye maisha yangu, nimeamua kujitolea kumsomesha kidato cha tano na cha sita kwenye shule za kisasa,”

“Taasisi yangu ya misaada ya kijamii ya Hamisi Kigwangalla Development Foundation itamlipia ada za masomo yake ya high school,” alisema Dk. Kigwangalla.

Getrude Clement ambaye ana miaka 16 amepata nafasi hiyo ya kipekee baada ya kupata nafasi ya kutoa hotuba kwa niaba ya watoto na vijana wengine duniani katika mkutano wa Umoja wa Mataifa ambapo alikaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na kusifiwa na watu mbalimbali duniani kutokana na hotuba yake nzuri.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Dk Kigwangalla Kumsomesha Mtoto Aliyeiwakilisha Tanzania UN appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/dk-kigwangalla-kumsomesha-mtoto-aliyeiwakilisha-tanzania-un/feed/ 0
Antoine Griezmann Aipeleka Atletico Madrid Fainali ya UEFA http://www.thehabari.com/antoine-griezmann-aipeleka-atletico-madrid-fainali-ya-uefa/ http://www.thehabari.com/antoine-griezmann-aipeleka-atletico-madrid-fainali-ya-uefa/#comments Tue, 03 May 2016 21:15:58 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71317 Licha ya Klabu ya Bayern Munich Kushinda katika mchezo wa nusu fainali ...

The post Antoine Griezmann Aipeleka Atletico Madrid Fainali ya UEFA appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
a

Licha ya Klabu ya Bayern Munich Kushinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya ligi ya Mabingwa kwa bao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid ndani ya dimba la Allianz Arena, Vijana wa Diego Semione wamesonga mbele kwa bao la ugenini

b

Katika mchezo huo vijana wa Guardiola ndio walikua wa kwanza kupata bao kupitia kwa Xabi Alonso dakika ya 31 kabla ya Griezman kusawazisha dakika ya 54, na la pili likifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 74

c

Timu zote zilikosa Penati ambapo wenyeji Buyern wakosa penati yao iliyopigwa na Thomas Muller dakika ya 34 huku Torres naye akikosa dakika ya 84 shukrani zikienda kwa magolikipa wa timu hizo ambao walizipangua

d

Katika mchezo wa kwanza Atletico ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 katika Uwanja wa Vicente Calderon, shukrani za Pekee zikienda kwa Saul Niguez aliyefunga bao dakika ya 11 baada ya kuichambua ngome ya Bayern

222

Atletico sasa wanamsubili mshindi wa leo katika Mchezo mwingine utapigwa Kati ya Man City wakialikwa na Real Madrid katika nusu na Kushuhudia mchezo wa kwanza timu hizo zilimaliza dakika 90 bila ya kufungana. Fainali ya Michuano ya hii itapigwa jumamosi tarehe 28

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Antoine Griezmann Aipeleka Atletico Madrid Fainali ya UEFA appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/antoine-griezmann-aipeleka-atletico-madrid-fainali-ya-uefa/feed/ 0
NSSF Wahamasisha Uandikishaji Wanachama wa Hiyari Temeke http://www.thehabari.com/nssf-wahamasisha-uandikishaji-wanachama-wa-hiyari-temeke/ http://www.thehabari.com/nssf-wahamasisha-uandikishaji-wanachama-wa-hiyari-temeke/#comments Tue, 03 May 2016 21:09:17 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71316 Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni kwa katika banda la NSSF kwa ajili ...

The post NSSF Wahamasisha Uandikishaji Wanachama wa Hiyari Temeke appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

Ofisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amani Marcel (kushoto) akiwakabidhi fulana wanachama wapya, Emmanuel Joseph na Prisca Mwamsojo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 waliandikishwa. 

Ofisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amani Marcel (kushoto) akiwakabidhi fulana wanachama wapya, Emmanuel Joseph na Prisca Mwamsojo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 waliandikishwa.

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni kwa katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
 Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akiwajazia fomu baadhi ya wanachama wapya katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 walijiunga na NSSF.
Ofisa Msajili wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Grace Mutegeki (kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha
na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia
  Wilayaya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango
akimjazia fomu ya kujiunga na NSSF mchuuzi wa mayai wakati wa  kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya
Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama wapya 214 walijiunga
na NSSF.
 
Baadhi ya wananchi wakisoma fomu
kabla ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama
wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Jijini
Dar es Salaam.
 Watu mbalimbali wakisubiri kujiandikisha.
Afisa Uandikishaji wa NSSF, Amina Kisawaga, kushoto akiwaelekeza jambo baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Zaidi ya wanachama 20 walijiandikisha.
Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post NSSF Wahamasisha Uandikishaji Wanachama wa Hiyari Temeke appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/nssf-wahamasisha-uandikishaji-wanachama-wa-hiyari-temeke/feed/ 0
Yanga Ubingwa Huooooooooo, Yapiga Mtu 3 http://www.thehabari.com/yanga-ubingwa-huooooooooo/ http://www.thehabari.com/yanga-ubingwa-huooooooooo/#comments Tue, 03 May 2016 15:58:23 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71312 Yanga imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuafutia ...

The post Yanga Ubingwa Huooooooooo, Yapiga Mtu 3 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
yanga

Yanga imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuafutia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United jioni ya leo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Ushindi huo ulitokana na mabao mawili ya washambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma na Amissi Tambwe wa Burundi, unaifanya Yanga ifikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 27.

Yanga sasa inaweza kutangaza ubingwa ndani ya mechi mbili zijazo kati ya tatu za mwisho, iwapo itaendeleza wimbi la ushindi.

Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, Yanga tayari walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma.

Ngoma alifunga bao la kwanza dakika ya pili kwa shuti kali, baada ya kuupitia mpira kwenye himaya ya mabeki wa Stand, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Assouman David.

Ngoma tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 45 kwa bao zuri akimlamba chenga kipa wa Stand United, Frank Muwonge baaada ya kutanguliziwa pasi nzuri na Mrundi, Amissi Tambwe.

Kipindi cha pili, Yanga ilikianza vizuri tena na kufanikuwa kupata bao la tatu lililofungwa na Tambwe dakika ya 63 akimalizia kona ya winga Simon Msuva.

Elias Maguri akaifungia bao la kufutia machozi Stand United dakika ya 82 baada ya kiungo wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kumchezea rafu kiungo wa Stand, Suleiman Kassim ‘Selembe.’

Yanga waliendelea kulisakama lango la Stand, lakini bahati yao leo ilikuwa ni 3-1.

Chanzo bin zubeiry.co.tz

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Yanga Ubingwa Huooooooooo, Yapiga Mtu 3 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/yanga-ubingwa-huooooooooo/feed/ 0
Maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Nidhamu Haya Hapa http://www.thehabari.com/maamuzi-ya-kamati-ya-rufaa-ya-nidhamu-haya-hapa/ http://www.thehabari.com/maamuzi-ya-kamati-ya-rufaa-ya-nidhamu-haya-hapa/#comments Tue, 03 May 2016 15:35:28 +0000 http://www.thehabari.com/?p=71309 Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo ...

The post Maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Nidhamu Haya Hapa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
tff

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo Mei 3, 2016 imetupilia mbali rufaa saba kati ya nane zilizowasilishwa mbele yake na viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016 maarufu kama StarTimes League.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati, Wakili Revocatus Kuuli ametangaza uamuzi mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo unatokana na kikao cha akidi iliyotimia ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati, Wakili Revocatus Kuuli pamoja na wajumbe wawili, Dk. Francis Michael na Abdallah Shaweji. Kadhalika warufani wote walihudhuria kikao hicho kilichojadili rufaa hizo Jumapili Mei mosi, 2016.

Kamati imemtoa hatiani Kipa wa Geita Gold, Denis Richard Dioniz baada ya kujiridhisha kuwa haikuwa jukumu lake kupanga muda wa mchezo kwa mujibu wa kanuni kutokana na kutumia muda mrefu maliwato baada ya kuugua tumbo kama ilivyoripotiwa na mwamuzi na kamisaa wa mchezo.

Dioniz alifungiwa miaka 10 kutojihusisha na mpira wa miguu sambamba na kulipa faini ya shilingi milioni kumi (10,000,000). Adhabu hiyo alipewa na pamoja na Kipa Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa. Mohamed hakukata rufaa baada ya kuadhibiwa Aprili 3, 2016.

Wadau hao wa soka walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza. Ambao rufaa zao zimetupwa ni:

Timu ya Geita Gold
Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma

Timu ya Soka ya Polisi Tabora

JKT Oljoro Fc ya Arusha
Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Katika adhabu hizo leo Kamati ya Rufaa ya Nidhamu imebariki adhabu kwa Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC aliyetiwa hatiani kwa kumshawishi Mohammed – kipa wa JKT Kanembwa FC kukaa golini ili penalti aliyogomea kabla ipigwe.

Awali, Kamati ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mchezo kati ya JKT Kanembwa FC v Geita Gold, Saleh Mang’ola Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma

Kuhusu Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora na Fatel Rhemtullah ambaye ni Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora hao imeamuriwa kuendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu kama Mwenyeakiti wa klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora, Bernad Fabian

Klabu za Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zilikutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao, hivyo kamati imeamuru adhabu hiyo iendelee.

Uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya TFF Aprili 3, 2016 ilitoa uamuzi wa shauri la upangaji wa matokeo wa kundi C kwa Ligi Daraja la Kwanza. Aliyesoma hukumu hiyo ni Wakili Jerome Msemwa ambako alisema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi.

Upande wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C sambamba na kumfungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu kamisaa wa mchezo wa Geita Gold na JKT Kanembwe, Moshi Juma baada ya kukutwa na hatia ya upagaji matokeo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita (GEREFA), Salum Kurunge, Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold, Cosntantine Moladi na Katibu wa klabu ya JKT Kanembwa Basil Matei waliachiwa huru na Kamati ya Nidhamu baada ya kutokutwa na hatia katika shauri hilo.

Mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde walifungiwa kwa muda wa miaka kumi kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni (10,000,000) kumi kila mmoja.

Katibu wa klabu ya Polisi Tabora, Alex Kataya, Katibu wa klabu ya JKT Oljoro, Hussein Nalinja, mtunza vifaa wa klabu ya Polisi Tabora, Boniface Komba, na Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Mrisho Seleman, waliachiwa huru na Kamati ya Nidhamu ya baada ya kutokutwa na hatia.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Nidhamu Haya Hapa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/maamuzi-ya-kamati-ya-rufaa-ya-nidhamu-haya-hapa/feed/ 0