Blogs Tanzania | News | Michuzi ya Habari leo » Habari za Vijijini

TGNP Yaendesha Warsha Mbeya Juu ya Namna ya Kuanzisha na Kutumia Vituo vya Taaifa na Maarifa
Wanawake wa Kata ya Mshewe Wilaya ya Mbeya vijijini wakijadiliana namna ya kuanzia na kuendesha vituo vya taarifa na maarifa katika warsha iliyo endeshwa kwa siku mbili na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kumalizika jana.

Na Pendo Omary, Mbeya Vijijini

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeendesha warsha ya siku mbili kuhusu namna ya kuanzisha na kutumia vituo vya taarifa na maarifa katika kata ya Mshewe, wilaya Mbeya Vijijini yaliyomalizika jana. Mafunzo hayo  kwa vikundi vya wanawake yalikuwa ni mwendelezo wa mafunzo ya  uraghbishi yaliyofanyika hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kuendeleza harakati za ujenzi wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi lililojikita katika ngazi za jamii.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo toka TGNP Kenny Ngomuo alisema, malengo ya mafunzo hayo ni pamoja na kushirikishana  katika kujenga uelewa wa dhana ya kituo cha taarifa na maarifa, kuoanisha yaliyojiri katika zoezi la uraghibishi na uanzishwaji wa kituo cha taarifa na maarifa.

“Malengo mengine ni kujifunza namna ya kuanzisha na kuendeleza vituo vya taarifa na maarifa na kuoanisha fursa zilizopo na kutengeneza mpango kazi wa kituo pamoja na ufuatiliaji,” alisema Kenny.

Alisema Vituo vya maarifa na taarifa vitaleta chachu ya kuzidi kukita harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika ngazi ya jamii. Vituo hivi vitachochea ujenzi wa nguvu za pamoja  Katika jamii ya kata ya Mshewe kwa kutumia mikakati kama  kukusanya, kutumia na kusambaza maarifa na taarifa.

Pia kuendesha mijadala ya wazi na kuweka kumbukumbu kuhusu mijadala hiyo, kuendesha mafunzo mbali mbali na kuweka kumbukumbu kuhusu mafunzo hayo, kufanya uchambuzi na ufuatiliaji wa masula au kero zinazoikabili jamii ya Mshewe; na kuchukua hatua za pamoja  kukabiliana na kero hizo.

“Kutokana na uzoefu uliojitokeza katika vituo tulivyovianzisha mwaka jana katika kata Sogwa, wilaya ya Kishapu, kata ya Mkambarani, wilaya ya Morogoro Vijijini na kata ya Ijombe wilaya Mbeya Vijijini, imeonyesha kuwa vituo tulivyovianzisha wanawake wamevitumia katika kuibua mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya, afya, maji na umiliki ardhi na vimekuwa mkombozi wa wanawake katika kufuatilia masuala yanayowagusa,” aliongeza Kenny.

Aidha washiriki wa warsha hiyo walisema, wamejifunza namna ambavyo watatumia vituo hivyo katika kupashana habari na kubadilishana uzoefu wa shughuri wanazozifanya ikiwemo uzalishaji mali ili kuongeza ozoefu.

“Kupitia kituo cha taarifa na maarifa, nitaweza kujua namna ya kudai haki zangu na za wengine hasa walioko pembezoni na kuhamasisha jamii na uongozi kuitisha mikutano na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazotukabili hasa sisi wanawake,” alisemaMelise Nkembo kutoka kijiji cha Mshewe, kata ya Mshewe.

Aidha Witness Sikayanga kutoka kijiji cha Mshewe, kata ya Mshewe alisema kupitia mafunzo hayo watahamasisha jamii na kuwapa elimu itakayowasaidia kuunda vikundi mbalimbali na kuanzisha vituo hivyo ili kusambaza vuguvugu la ukombozi wa wanawake na makundi yaliyoko pembezoni.

“Tunapaswa kwenda kwenye jamii na kuwapa haya mafunzo ili kuendeleza harakati za ukombozi wa wanawake na wote waliopembezoni. Tunaiomba TGNP Kuendelea kutoa mafunzo haya kwa watu wengine,” alisema Witness.

Shule za Kata Zajiendesha kwa Fedha za Walimu Wakuu
Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Nduweni, Venance Mramba

Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango

Na Thehabari.com, Rombo

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Rombo kimesema shule nyingi za Sekondari za Kata wilaya hiyo na maeneo mengine nchini zinajiendesha kwa kutegemea fedha za mifukoni kwa walimu wakuu wanaoziongoza shule hizo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa CWT Wilaya ya Rombo, Erasmo Mwingira alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi. Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hivi karibuni kwa kutembelea shule kadhaa za sekondari wilayani hapa umebaini kuwepo na mazingira magumu ya uendeshaji wa shule hizo kutokana na ugao wa fedha za uendeshaji shule hizo kutokuwa wa uhakika huku hata kiasi kinachozifikia hakitoshelezi gharama za uendeshaji.

Akifafanua Mwingira alisema fedha zinazotolewa kuziendesha shule hizo ‘capitation’ licha ya kuwa hazitoshi huwa hazifiki kabisa shuleni hali ambayo huwafanya walimu wakuu kubuni mbinu mbalimbali za uendeshaji wa shule zao ikiwemo kuweka utitiri wa michango kwa wazazi ili kuhakikisha mambo yanakwenda shuleni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya

“Sasa hivi shule za msingi na sekondari (za serikali) zinaendeshwa na mifuko ya walimu wakuu…capitation haifiki kabisa shuleni, fedha inayowafikia ni kidogo sana na haiwezi kuendesha zile shule, walimu wanatumia mbinu zao kuziendesha shule ndio maana unaona michango inakuwa mingi shuleni,” alisema Mwingira.

Alisema licha ya serikali kusema ada ya sekondari ni shilingi 20,000 kwa sasa michango katika shule hizo ni mingi kiasi cha kufikia 120,000 jambo ambalo limewafanya baadhi ya wazazi kuelemewa na mzigo wa michango na wengine kushindwa kabisa kuimudu.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi katika shule za Sekondari za Tanya, Nduweni, Urauri, Holili na Ngaleku na nyinginezo zote za wilayani Rombo umebaini uwepo wa utitiri wa michango jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya wazazi na wadau wa elimu wilayani hapa. Mfano shule ya Sekondari Tanya jumla ya michango yake imefikia sh. 115,000; mgawanyiko wake ukiwa kama ifuatavyo:- Ada sh 20,000, Madawati sh 15,000, Chakula sh 60,000, Tahadhari sh 5,000, Ulinzi 5,000, Taaluma sh 5,000 na Kitambulisho sh 5,000.

Aidha uchunguzi zaidi umebaini shule nyingi za sekondari za kata hazina walimu wa masomo ya sayansi jambo ambalo huwalazimisha walimu wakuu kutafuta walimu wa kukodi hasa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kuja kuwafundisha wanafunzi masomo ya sanyansi kama Hisabati, Fizikia, Kemia, Baiolojia na mengineyo huku wakitumia mbinu anuai kukusanya michango kuwalipa walimu hao wa kukodi.

“Nashauri Serikali iongeze fungu la uendeshaji wa fedha shuleni maana fedha za michango zinazotolewa na wazazi hazitoshi kuendesha shule…huwa tunakodi walimu (wanafunzi waliomaliza kidato cha sita) kuja kutufundishia masomo ya sayansi kwa muda unakuta gharama zinakuwa kubwa za uendeshaji shule,” alisema Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango.

“Sisi tumelazimika kuajiri kwa muda wanafunzi sita waliomaliza kidato cha sita kufundisha masomo ya sayansi kwa fedha za shule…tunajibanabana kwa michango pamoja na wazazi na kuhakikisha tunapata chochote kuwalipa walimu hawa wa muda bila hivyo mambo hayaendi,” alisema Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Nduweni, Venance Mramba akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Kwa upande wake Mwingira alisema vijana wa kidato cha sita ambao hutumiwa na shule nyingi kuokoa jahazi ya masomo ya sayansi wamekuwa wakiwakaririsha wanafunzi kujibu mitihani na sio kuwafundisha jambo ambalo alisema ni hatari kwa elimu ya Tanzania. “Kujua kusoma na kuandika si kigezo cha kumfundisha mtu…vijana hawa wa kidato cha sita hawana mbinu za ufundishaji wanachokifanya ni kuwakaririsha wanafunzi. Pamoja na hayo aliishauri serikali kutojitoa katika jukumu la kuendesha shule za kata na kuwaachia wazazi kwani shule hizo ziko katika hali mbaya na zinahitaji kuongezewa fedha za uendeshaji.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya alikiri kuwepo na tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi katika shule nyingi za wilaya yake, hivyo walimu kulazimika kuajiri kwa muda vijana wa kidato cha sita kusaidia wanafunzi huku jitihada zikiendelea kufanya kukabiliana na tatizo hilo.

“Walimu wa sayansi ni tatizo Rombo hawatoshi…mwaka huu tumejitahidi na kuajiri takribani walimu 134 wakiwemo wachache wa masomo ya sayansi lakini tatizo bado lipo,” alisema Mboya kikilitolea ufafanuzi suala hilo ofisini kwake wilayani Rombo hivi karibuni.

Imeandaliwa na www.thehabari.com

Wilaya ya Rombo Kutumia Nyuki Kupambana na Tembo Wavamizi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya akizungumza na mtandao wa www.thehabari.com hivi karibuni wilayani Rombo.

Pichani ni baadhi ya majengo ya Shule ya Msingi Rongai, wilayani Rombo. Shule hii ni miongoni mwa maeneo yanayoathiriwa na uvamizi wa tembo waharibifu ambao huathiri taaluma shuleni hapo.

Baadhi ya mashamba ya wananchi eneo la Rongai, wilayani Rombo ambayo mara kadhaa huvamiwa na tembo waharibifu.

Na Thehabari.com, Rombo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Rombo imeanza mipango ya kutumia ufugaji wa nyuki kukabiliana na tembo waharibifu ambao mara kadhaa huvamia baadhi ya makazi ya wananchi maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kufanya uharibifu wa mazao pamoja na kuua au kujeruhi wakazi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Judethadeus Mboya alisema tayari halmashauri hiyo imetengeneza mizinga ya nyuki ambayo imesambazwa maeneo kadhaa ili kukabiliana na tembo waharibifu eneo hilo.

“Unajua nimetembea mbuga mbili za Kenya ikiwemo Tsavo ambazo tumepakana nazo eneo hili sehemu ambayo tembo hutokea huko na kuvamia maeneo yetu, sehemu hizi wao wamedhibiti uvamizi wa tembo…wamefuga nyuki wengi sana na maeneo mengine wametumia hadi teknolojia kuwazuia tembo kuvamia makazi ya raia hivyo hawapati madhara kama yetu,” alisema Mboya akifanya mazungumzo na gazeti hili ofisini.

Alisema kwa sasa tayari wametengeneza mizinga 50 ya nyuki na kuifunga ukanda wa chini wa vijiji kama Chala, Ibukoni, Ngoyoni na maeneo mengine ambayo tembo huyatumia kama njia kipindi cha uvamizi na kwa sasa mizinga mingine 100 ya nyuki inaandaliwa kuenezwa maeneo mengine kukabiliana na tembo hao hatari.

Alisema viongozi wa halmashauri hiyo pia wametoa elimu kwa wanakijiji maeneo husika ya kuhamasisha uvugaji nyuki katika vikundi ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tembo hao waharibifu ambao idadi kubwa hutokea nchi jirani ya Kenya na kufanya uharibifu pamoja na kutishia maisha ya wanavijiji upande wa Tanzania.

Aidha kiongozi huyo alisema tembo hao mbali na kufanya uhalibifu mkubwa wa mazao ya wanavijijini kipindi cha uvamizi wakati mwingine wamekuwa wakiuwa raia jambo ambalo ni hatari zaidi kiusalama.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini uvamizi wa wanyama hao umekuwa kero kwa maeneo mbalimbali ya vijiji vya wilaya hiyo, kiasi ambacho unatishia shughuli za maendeleo ya wananchi kama kilimo pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla.

Akizungumzia hali ya uvamizi wa tembo na athari za elimu, Mwalimu wa Taaluma Shule ya Sekondari Tanya, Shuma Himidiel alisema miezi ambayo tembo huanza kufanya uvamizi huingilia ratiba za masomo na mara kadhaa kusimama kutokana na hofu ya wanafunzi na usalama wao hasa wanapotoka na kuja shuleni.

“Kimsingi wanyama hawa wanapoanza usumbufu kijiji kizima huwa na heka heka na wakati mwingine hata wanafunzi wanashindwa kuja shule kuhofia maisha yao…hata wazazi huwazuia watoto wao kutoka hadi hali ya hatari inaporejea kuwa ya kawaida.

Akifafanua zaidi mwalimu Himidiel alisema mara ya mwisho tembo kufanya uvamizi katika Kijiji cha Tanya waliua mtu mmoja walipokuwa wakidhibitiwa na askari wa wanyamapori eneo hilo.

Room to Read Wajenga Madarasa 60 Wilayani Mvomero
Jengo lililokamilika la shule ya msingi Kanga Wilayani Mvomero tarafa ya Turiani ambalo limejengwa na shirika la Kimataifa la Room to Read.

Moja ya madarasa katika  Shule ya Msingi Dihinda iliyopo kata ya Mvomero ambalo limejengwa na Shirika la Room to Read.

*Ni shirika pekee lenye mradi wa kuimarisha uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto.

*Tayari limefanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 60 katika shule za msingi 15 wilayani Mvomero.

*Sasa laelekeza nguvu zake wilayani Bagamoyo na kukusudia kujenga madarasa 40 na maktaba 20.

Room to Read ni Shirika la Kimataifa lisilo la kibiashara linalojishughulisha na kuboresha na kuinua elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa na maktaba pamoja na kusambaza vitabu vya kujisomea wanafunzi sambamba na kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa kuwasaidia wanafunzi wa kike waliopata masomo na kuwainua kitaaluma katika nchi kadhaa duniani.

Kwa sasa shirika hili limefungua tawi hapa nchini Tanzania likiwa na program kadhaa za kusaidia kuboresha na kuinua kiwango cha elimu katika shule za msingi.

Mo blog ilipata fursa ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo nchini Tanzania, ambaye alitoa maelezo ya kina kuanzia historia ya shirika hilo, kuanza kwa shughuli zake hapa nchini, mafanikio yaliyopatikana na hatimaye mikakati ya shirika hilo katika siku za usoni.

Theodory Mwalongo ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room To Read ambalo ni Shirika la Kimataifa lenye Makao yake makuu huko San Francisco nchini Marekani ambako lilianzishwa mwaka 2000.

Baadhi ya Wanafunzi wilayani Mvvomero wakijisomea katika moja ya Maktaba iliyojengwa na Shirika la Room to Read Tanzania.

Akizungumzia shirika hilo Theodory Mwalongo anasimulia…………………!!

Lilianzia huko nchini Nepal na mwanzilishi wake alikuwa anaitwa John Wood ambaye alikuwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Microsoft na katika shughuli zake aliweza kupita Nepal akaona mahitaji makubwa ya watoto ya vitabu.

Akaamua kuacha kazi yake ya kutangaza biashara ya kompyuta huko Asia akaamua kurudi Marekani akawa anakusanya vitabu na kuvipeleka Nepal, lakini alipopeleka vitabu vile ikawa hakuna mahali pa kuviweka kwa sababu hakukuwa na madarasa hali ilikuwa ni mbaya sana.

Basi akaanzisha wazo la kujenga kwanza madarasa, kujenga vyumba vya maktaba na baadae kupeleka vitabu.

Basi hatimaye shirika limeena katika nchi nyingi ambapo kwa sasa Room To Read inafanya kazi zake katika nchi 10 duniani na kwa hapa Afrika ipo katika nchi 3 ambazo ni Afrika Kusini, Zambia na Tanzania.

Hapa Tanzania shirika limepata usajili wake mwezi wa 9 mwaka 2010 lakini rasmi limeanza shughuli zake mwaka 2011 kwa kazi za kuboresha elimu ya msingi.

Shirika lina programs nne (4);  ya kwanza ni kuboresha miundo mbinu ya shule tukimaanisha ujenzi au ukarabati wa vyumba vya madarasa, kuwawezesha watoto kupata mahali pazuri pa kujifunzia lakini waalimu pia mahali pazuri pa kufundishia.

Sambamba na program hiyo ni uanzishaji wa maktaba katika shule za msingi. Maktaba hizi zinawekwa vitabu vya hadithi vya watoto na vitabu vya maarifa mengine kama vile mazingira, jinsia, afya, haki za binadamu na kadhalika.

Kwa hiyo katika uanzishaji wa maktaba tuna program ya tatu ambayo inalenga uchapaji wa vitabu vya hadithi. Kwa hiyo tunagundua watunzi mahiri na wachoraji wanatunga vitabu vya hadithi za watoto na kuviweka katika maktaba hizo.

Pia katika program hii ya kuboresha elimu ya msingi, tuna program ya kushirikiana na walimu katika shule za msingi, waratibu kata na maafisa elimu wa shule za msingi kuimarisha uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto.

Mwanafunzi akijisomea katika maktaba mpya ya kisasa na yenye hewa safi iliyojengwa na shirika la Room to Read.

Hivyo hizi program 4 nilizozitaja yaani kuboresha miundo mbinu katika shule za msingi, uanzishwaji wa maktaba, kuboresha kusoma, kuandika na kuhesabu na kuchapisha vitabu kunalenga katika shule za msingi tu. Lakini tuna program moja kubwa ambayo inalenga kuwawezesha wasichana waliokosa kwenda elimu ya sekondari kuendelea na masomo.

Tuna maeneo matatu, kwa kuwasaidia wasichana ambao wametoka katika familia ambazo zina kipato cha chini kuwalipia ada na mahitaji mengine. Lakini pia kusaidiana na shule husika kuwasaidia wasichana kuwainua kitaaluma, wale ambao uwezo wao wa kufanya vizuri katika masomo uko chini, basi Room To Read inashirikiana na waalimu kuweka mikakati ya namna ya kuwainua kufanya vizuri katika masomo.

Na tatu kuna program ya kuwasaidia Stadi za maisha kuwawezesha wajitambue, waweze kufanya maamuzi sahihi na wajue ni kwa nini wako shuleni. Hivyo basi tungesema tuna program kuu mbili, kuimarisha elimu ya msingi na program ya wasichana katika sekondari.

Pichani ni  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania Bw. Theodory Mwalongo akizungumza na baadhi ya wanafunzi wilayani Mvomero wakati wa kukabidhi majengo ya Maktaba za kujisomea pamoja na madarasa.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania Bw. Theodory Mwalongo akisoma hotuba yake katika sherehe za kukabidhi majengo ya madarasa na Maktaba katika Wilaya ya Mvomero tarafa ya Turiani.

Mwalongo anaendelea kutueleza Room to Read kwa Tanzania limefanya nini…………………?

Sasa katika Tanzania baada ya kupata usajili tulianza katika katika wilaya ya Mvomero katika tarafa ya Turiani.

Katika kukamilisha hizo program tulizozitaja hapo juu, kwa mwaka 2012 tuliweza kujenga madarasa 60 katika shule za msingi 15. Katika madarasa hayo 60, vyumba 45 ni vya kusomea darasa la kwanza, la pili hadi la tatu na vyumba 15 vilijengwa maalum kwa ajili ya kuanzishwa maktaba.

Mradi huu mkubwa ambao uligharimu karibu shilingi bilioni moja na laki tano (1.5bn) tulishaka kabidhi serikalini, kwa serikali ya wilaya ya Mvomero tarehe 22 mwezi Machi katika sherehe kubwa ya kufana ambapo Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Ndugu Anthony Mtaka ndio alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo.

Madarasa hayo yameaanza kutumika tayari na maktaba hizo zinatumika na wananchi wamefurahia sana kitendo hiki. Kwanza tumepunguza msongamano mkubwa sana katika madarasa yale kwa sababu kabla ya hapo unakuta chumba kimoja cha darasa kina wanafunzi zaidi ya 60 lakini sasa angalao tumepunguza msongamano huo.

Wanafunzi wa shule ya msingi wilayani Mvomero tarafa ya Turiani wakiimba na kufurahia baada ya kukabidhiwa rasmi darasa zuri lenye hewa safi pamoja madawati mapya lililojengwa na shirika la Room to Read.

Lakini kikubwa ni kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya maeneo yale ni shule kuwa na maktaba, watoto wanafurahia sana kutumia vyumba vile vya kujisomea kwa sababu kuna vitabu vya hadithi na kadhalika. Walimu nao wamepata unafuu mkubwa wa kuwa na nafasi za kuweza kufundisha. Lakini pia halmashauri ya wilaya imelipokea vizuri kwamba kwa kweli tumepunguza mzigo mkubwa ambao halmashauri inapambana nao kujenga vyumba vya madarasa.

Naweza kusema Room To Read ipo hapa Tanzania kusaidiana na serikali na wadau wengine kuinua ubora wa elimu hapa Tanzania.

Sasa hivi tumeanza katika mkoa wa Pwani ambako tutaanza na wilaya ya Bagamoyo, ambako mwaka huu tunategemea kuzifikia shule 20 ambapo tunategemea kujenga vyumba vya madarasa 40 na vyumba vya maktaba 20.

Tutakuwa na program ya kuboresha wasichana na huo mradi wa kusaidia watoto kujua kusoma na kuandika.

Hii ndio hali halisi ya baadhi ya madarasa katika shule za wilayani Mvomero tarafa ya Turiani hapo awali.

Mkurugenzi Mwalongo wa Room to Read hakusita kutoa rai kwa serikali………………..!!!

Rai yangu ni kuiomba serikali kushirikiana na sisi kuhamasisha wananchi waweze kuchangia fursa ambazo ziko ndani ya uwezo wao, kama vile kuchangia mchanga, mawe, matofali hata nguvu kazi, lakini pia halmashauri ishirikiane na sisi kuhakikisha majengo yake yanakuwa katika ubora unaotakiwa na shirika liweze kufuata viwango vya serikali vilivyowekwa.

Naamini kwa mshikamano huo wa serikali, wananchi na sisi tunaweza tukasaidia kuboresha elimu katika Tanzania.

Amuua Baba Yake kwa Ushirikina
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamsaka Richard Jecap (30) mkazi wa kitongoji cha Matai A kwa tuhuma za kumuua baba yake kwa kumpiga mpini kichwani  akimtuhumu kuwa ni mshirikina.

Tukio hilo lilitokea Aprili 18 saa 4.50 asubuhi wakati baba huyo akiwa amekaa nyumbani kwake akiota jua. Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa kijiji hicho, Emmanuel Mwakibinga alisema kuwa mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya watoto wake kufariki ambapo mtoto wa kwanza mwenye umri wa miaka minne alifariki Januari mwaka huu na alikuwa akidai baba yake huyo ndiye aliyemloga.

Alisema kuwa Aprili 16 mtoto wake wa pili mwenye umri wa miaka miwili alifariki na alidai kuwa baba yake ndiye aliyemloga kwani amekuwa akiloga watoto wake hao na siku ya mazishi aliahidi kumfanyia kitu kibaya baba yake huyo licha ya kuwa hakueleza ni kitu gani.

Mwenyekiti huyo alisema siku ya tukio hilo alikuwa akipita karibu na nyumba hiyo akasikia kishindo kikubwa kutoka eneo la nyumba hiyo na kisha kufuatia vilio vya watu na aliposogea alikuta mtuhumiwa huyo amekwishampiga mpini kichwani baba yake huyo na kisha kuanguka na kupoteza fahamu.

Baada ya kuona hivyo, walisaidiana pamoja na wanafamilia wengine kumwahisha hospitali na alitundikiwa maji sambamba na kushonwa katika jeraha kubwa alilolipata kichwani na usoni na kisha kulazwa ili  kuendelea kupata matibabu.

Mwakibinga alisema kuwa wakati akiendelea kupatiwa matibabu alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi na maumivu makali aliyokuwa nayo katika jeraha alilolipata baada ya kupigwa na mpini wa shoka kichwani.

CHANZO: Gazeti Mwananchi

Ushahidi Kesi za Kubaka/Mimba ni Changamoto Handeni
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana

Na Joachim Mushi, Handeni

“KESI nyingi za tuhuma za kubaka na mimba kwa wanafunzi zinazotufikia zinashindwa kufikia hukumu maana mashahidi wanashindwa kuthibitisha pasipo shaka…nyingi zinaharibika sababu hawataki kusema ukweli, hivi karibuni nililazimika kuwaweka ndani wawili (mashahidi) kwa kuwa wanadanganya. Unakuta maelezo aliyotoa polisi ni mengine na akifika huku anageuka,” anasema Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana alipofanya mahojiano na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

Hakimu Maligana anasema licha ya takwimu zao kuonesha kesi za mimba/kubaka wanafunzi kwa sasa zinapungua bado suala la kuharibika kwa ushaidi wa kesi za mimba ni changamoto. Anasema kesi nyingi za wanafunzi zimekuwa zikishindwa kufanikiwa hadi hatua ya hukumu kutokana na mtindo wa kuvuruga ushahidi.

Anasema awali kikwazo kikubwa kwa kesi kama hizo ilikuwa ni upande wa wazazi na walimu kutotoa ushirikiano wa kutosha kwenye mchakato wa kesi. Lakini walimu na wazazi wameacha usumbufu huo hivyo imebaki kwa wanafunzi pamoja na watuhumiwa ambao mara kadhaa wanakuwa wapenzi wao. Anaongeza kuwa licha ya matukio hayo kupungua changamoto bado zipo.

Takwimu za kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2012 zinaonesha mahakama hiyo ilipokea kesi 10 za tuhuma za mimba/kubaka kwa wanafunzi, huku kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2013 ni jumla ya kesi sita tu zimepokelewa katika mahakama hiyo. Anasema kesi sita za mwisho kupokelewa zipo katika hatua anuai.

Zuber Chembera ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni (OCD), akizungumza na mwandishi wa makala haya ofisini kwake, anakiri kupungua kwa matukio ya kesi za mimba/kubakwa kwa wanafunzi Wilaya ya Handeni kutokana na takwimu zao.

Anasema kwa mwaka 2012 hadi mwezi Novemba walikuwa na jumla ya matukio ya kesi kama hizo 66, lakini kwa mwaka huu (Machi, 2013) kuna jumla ya matukio ya kesi kama hizo 14 tu yalioripotiwa.

Anasema elimu inayotolewa na Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Handeni imesaidia. “Kesi zinazotufikia hapa huku zikiwa na ushaidi wa kutosha tunazipeleka mahakamani, zile zinazokuwa hazina ushaidi wa kutosha tunajaribu kuzifuatilia kiuchunguzi kwa mujibu wa taratibu zetu. Lengo letu kupitia Dawati la Jinsia na Watoto ni kuhakikisha tunapunguza kama sio kumaliza kabisa vitendo hivyo.

Eliakimu Kapele ni Makamu wa Shule ya Sekondari Kivesa

Anasema maranyingi ushahidi wa kesi kama hizo pia umekuwa ukiharibiwa na wahusika kabla ya kufika mahakamani, wanaweza baada ya kesi kufunguliwa wakashawishiana na kukaa nje bila ya sisi kujua na hivyo kupotea wote.

Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama anasema idadi ya matukio ya mimba shuleni hapo inapungua kwa sasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali, lakini si kwamba matukio hayo yamekoma kabisa.

“Matukio ya mimba kimsingi kwa sasa yanapungua…lakini si kwamba yamekwisha kabisa, tatizo kubwa ni malezi katika familia pamoja na vishawishi vingine,” anasema mwalimu huyo akizungumza shuleni Komnyang’anyo.

Napingana kwa mtazamo mwingine kwamba umbali wa makazi kwa wanafunzi unachangia mimba…nasema hivyo kwa kuwa kwa mwaka jana mwishoni kuna mfano mzuri, shuleni kwetu yupo mwanafunzi (wa kidato cha pili ‘C’) ambaye anahudumiwa kila kitu na pia yu-karibu na shule lakini amejikuta akipewa mimba na kukatishwa masomo.

Mwanafunzi huyu pia huwezi kumuingiza katika kundi la wanafunzi wenye mazingira magumu ya maisha katika familia zao, nasema hivyo kwa kuwa huyu analipiwa kila kitu, anapewa matumizi yote yanayoitajika na shirika moja linalosaidia wanafunzi wa kike lakini ameshindwa kuendelea baada ya kupewa mimba.

Kesi hii tayari ipo kwenye Serikali ya kijiji kwa hatua zaidi baada ya sisi kutoa taarifa. Sasa watu wanachukulia hatua si kama ilivyokuwa hapo nyuma.Tangu amekuwa huyu Mkuu wa Wilaya mpya (Muhingo Rweyemamu) wananchi wanatoa ushirikiano kwa kesi kama hizi. Kimsingi ujenzi wa mabweni itakuwa hauweni kwa wanafunzi ambao kwa sasa wanatokea vijiji vya mbali kuja shuleni, vijiji hivyo ni pamoja na Bangu, Kwamagome na Kwakonje.

Ofisa Elimu Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa

Mazungumzo ya wanafunzi Hamad Ngomero kidato III, Salome Kalage kidato cha IV, Michael Richard kidato cha I, Mwajuma Munga kidato cha II, Mwajabu Fungo kidato I na Farid Iddy kidato cha IV – wote kutoka Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wanakubali kwa pamoja uwepo wa matukio ya mimba, japokuwa kwa sasa ni kwa kiwango kidogo.

Mwajuma Munga anasema matukio hayo bado yapo lakini yamepungua si kama ilivyokuwa hapo nyuma. Naye Salome Kalage anasema mfano kuanzia mwezi Januari 2013 anawajua wanafunzi watatu ambao wamepata mimba na kuachishwa shule. Anawataja wanafunzi hao ni pamoja na Kuruthumu Omar (IV), Elizabeth Hamis (IV) na Docas (III).

Kwa upande wake mwanafunzi Hamad Ngomero anasema tamaa za starehe na hali ngumu ya maisha katika familia kaadhaa wilayani Handeni ndiyo inayowaponza wanafunzi wa kike na hata kujikuta wakitiwa mimba na kukatishwa masomo.

Martin Mwingo ni Mwaliku Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Kileleni; ujio wa Mkuu wa Mkoa mpya Handeni umeanza kuonesha mafanikio kwa upande wa matukio ya mimba kwa wanafunzi. “DC (Mkuu wa Wilaya) wasasa anajitahidi sana kupitia kampeni yake ya “Niache Nisome” anafuatilia kesi za mimba na kuhakikisha wahusika wanapata adhabu kwa mujibu wa sheria…mfano sasa hivi tuna kesi moja tumeletewa hizi ni juhudi za Mkuu wa Wilaya,” anasema Mwingo.

Kesi zinapungua mfano mwaka jana tulikuwa na kesi mbili za mimba lakini mwaka huu (2013) hadi sasa hatujapata kesi ya mimba…lakini pamoja na hayo malezi ya watoto kwa wazazi bado ni tatizo, mtoto ananyenyekea kea mzazi wake tu dharau kwa watu wengine-haya si malezi. Zamani mtoto anaweza kuadhibiwa na mkubwa yeyote ilimradi awe amekosa, lakini sasa sivyo.

“Mi nashangaa kila uchao watu wanang’ang’ania haki za watoto wasiadhibiwe uweke utaratibu wa kutoa adhabu lakini nashangaa kwanini wasitaje na wajibu wa mtoto hili ni muhimu…tusing’ang’anie haki za mwananafunzi tu tuoneshe na wajibu wake pia,” anasema Mwalimu Mwingo.

Anasema pamoja na juhudi hizo bado utandawazi unaathiri nidhamu za wanafunzi, umiliki wa simu za mkononi matumizi mabaya ya mitandao kama tovuti nayo yanawaharibu wanafunzi, ipo haja ya Serikali kuingilia na kupiga marufuku wanafunzi kumiliki simu shuleni maana simu inamambo mengi sasa.

Hussen Kigoma ni mwanafunzi wa kidato cha III, katika moja ya shule za kata Wilaya ya Handeni ambazo ndizo zimezokuwa na changamoto anuai. Anasema ipo haja ya kuwa na utaratibu wa kuwapima vipimo vya ujauzito mara kwa mara wanafunzi wa kike.

“Sasa hivi wapo ambao wanapata na kutoa mimba hizo bila uongozi wa shule kujua…sasa hivi tunawajua wanafunzi wawili ambao walipata mimba mwaka huu shuleni kwetu. Mfano Joyce Gasper na Jesca Paul wote wa kidato cha nne wamepata mimba…huenda mwaka huu mimba zikaongezeka zaidi,” anasema Hussein Kigoma.

Eliakimu Kapele ni Makamu wa Shule ya Sekondari Kivesa; anasema linapungu tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma. Mfano mwaka jana tulikuwa na matukio mengi ya kesi za mimba kwa wanafunzi, lakini hadi muda huu kwa 2013 tunayo matukio mawili tu. Na hatu zinachukuliwa maana msukumo unaanzia kutoka kwa viongozi wa Serikali za Mitaa.

Hii inatokana na Mkuu wa Wilaya wa sasa Muhingo Rweyemamu ametia mkazo sana masuala ya mimba kwa wanafunzi, watu wamekuwa makini na wafuatiliaji.

“Mfano sasa mimba inapotokea kuanzia mzazi wa mtoto aliyetiwa mimba, mtoto mwenyewe na mtuhumiwa wote wanashikiliwa…mi naamini kama adhabu hizi zitaendelea kutolewa ipasavyo watu watanyooka tu,” anasema mwalimu Kapele.

Hata hivyo mwalimu huyo anashauri mabadiliko ya sheria na kanuni za utoro shuleni, anasema maamuzi yamekuwa na mkanganyiko. Mfano kanuni za shule zinaelekeza kuwa mwanafunzi asipo hudhuria shule kwa siku 90 afukuzwe shule. Hili kwa sasa halifanyiki maana limekaa kisiasa zaidi…wanafunzi wanatoroka hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa maelekezo lakini baadaye wanarejeshwa kuja kufanya mitihani, hili ni tatizo.

“Inatokea mwanafunzi anabeba mimba na baadaye anarudi shuleni baada ya kujifungua, mwanafunzi kama huyu ni tatizo hawezi kuwa na vurugu sana kinidhamu na wakati mwingine anawavuruga hata wenzake maana anakuwa hana maadili.”

Shule yetu inautaratibu mzuri wa kuhakikisha muda wote unaofaa wanafunzi wanakuwa darasani kupata kilichowaleta hapa shuleni. Lakini huwezi kuamini kuna baadhi ya wanafunzi muda wote wapo huku vichochoroni wanajificha hawaji shuleni, utoro umekithiri! Lakini hawa huenda wakaruhusiwa kuja kufanya mitihani hapo baadaye.

Kanuni za shule mara kadhaa zimewekwa pembeni na siasa kuingizwa kwenye kanuni hizo, hali hii inawapa wanafunzi kiburi na uhuru mkubwa-huwenda wanadhani kufanya hivi ni kuwasaidia lakini ukweli ni kwamba wanawaharibu.

Ofisa Elimu Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa anakiri kuwepo na mabadiliko makubwa ya utoro wa mimba ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka jana. “Kimsingi huko nyuma utoro hasa wa mimba ulikithiri kwa wanafunzi wa Sekondari na Msingi, lakini hali ya sasa ni tofauti. Kuna mabadiliko kampeni ya ‘Niache Nisome’ imesaidia sana…kwa sasa wengi wanaohusika na kuwatia mimba wanafunzi wanapelekwa mahakamani,” anasema Muchiwa.

Anasema zoezi la kamatakamata lililokwenda sambamba na kampeni ya ‘Niache Nisome’ na watu hufikishwa kwenye hatua mbalimbali limesaidia hivyo mambo yanabadilika. Kwa mantiki hiyo waweza kuona kuanzia Januari 2013 hadi sasa (Machi) sijapokea kesi hata moja ya mimba.

Tunachokifanya sasa ni kutoa elimu zaidi kwenye mikutanyiko ya jamii kupitia viongozi wa ngazi mbalimbali za halmashauri, ili kuhakikisha tunafanikiwa zaidi tumeanza mkakati wa kuwajengea uwezo wananchi na shule. Hii ni kukabiliana na baa la njaa ambalo limekuwa likijitokeza mara kadhaa.

“Unajua mtu anapokuwa na njaa kushawishika ni rahisi…na Handeni kuna njaa sasa hali kama hii yaweza kuathiri pia sekta ya elimu, tumejipanga kuimarisha kilimo cha mazao kama mahindi na mtama shuleni ili wanafunzi wawe na uhakika wa chakula wawapo shuleni,” anasema Ofisa Elimu huyo wa Wilaya ya Handeni.

Ofisa Elimu Taaluma, Basil Mrutu anasema kwa mwaka jana kwa mujibu wa takwimu zao walikuwa na ripoti za mimba 26 kwa Wilaya nzima, lakini tangu Oktoba 2012 hadi sasa hawajapata kesi za matukio ya mimba.

Simon Mdaki ni Mkuu wa Idara ya Sekondari Wilaya ya Handeni; anasema kuwa “Halmashauri imeandaa matrekta 7 ambayo shule zitapewa kipaumbele cha kuyatumia ili kuweza kuendesha kilimo kwa ajili ya lishe kwa wanafunzi.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TAMWA

Mwanafunzi Kidato cha Pili Abebeshwa Mzigo Kulea Familia
Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama akizungumza na mwandishi wa Thehabari.com

Mwanafunzi Mwenjuma Magalu (16), mstari wa pili kulia wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo

Na Joachim Mushi, Handeni

MWANAFUNZI wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Mwenjuma Magalu (16) amejikuta akibeba mzigo wa kulea familia baada ya familia hiyo kutelekezwa na babayake.

Mwanafunzi huyo anayeishi katika Kijini cha Msasa amejikuta katika hali hiyo ngumu baada ya mama yake mzazi, Hadija Magalu kufariki dunia ambaye ndiye aliyekuwa akiihudumia familia hiyo baada ya mzazi mwenzake (mumewe) kuitelekeza miaka minne iliyopita.

Mama huyo (Hadija Magalu) alifariki dunia Agosti, 2013 kwa matatizo ya uzazi na kuiacha familia hiyo ya watoto watatu aliyokuwa akiihudumia chini ya ulezi wa mamayake mzazi, Bibi Amina Mohamed.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni kijijini Msasa, mwanafunzi Magalu alisema amelazimika kuilea familia hiyo baada ya bibi yake aliyeachiwa familia hiyo kuugua ugonjwa wa TB na kushindwa kuendesha shughuli za kilimo na nyinginezo kuisaidia familia hiyo.

“Bibi ndiye aliyekuwa akitupikia, tutafutia chakula na tulikuwa tukishirikiana naye hata kulima…lakini kazi hizo zote kutokana na afya yake hawezi kuzifanya, ninalazimika kuzifanya mwenyewe. Japokuwa nipo shuleni lakini natakiwa kujua tutakula nini tunapata wapi pesa ya chakula na shughuli nyingine za familia,” alisema Magalu akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema familia yao hutegemea kilimo lakini wakati mwingine hulazimika kwenda kutafuta vibarua vya kufanya ili kupata pesa ya kula yeye pamoja na bibi yake. Aidha aliongeza kuwa wadogo zake wawili ambao awali alikuwa akikaa nao amelazimika kuwapeleka kwa mjomba wake baada ya kuona hali ni ngumu. Hata hivyo alisema wajomba zake nao hali yao ni ngumu hivyo wanashindwa kuhudumia familia hiyo.

Akizungumzia hali ya maisha ya familia hiyo Bibi. Amina Mohamed ambaye kwa sasa ni mgonjwa wa TB alikiri mwanafunzi huyo kuwa na majukumu mazito ya familia ambayo awali alikuwa ameyabeba yeye baada ya mwanaye kufariki dunia.

“Kweli mtoto huyu anaelemewa na malezi ya familia hii lakini sina cha kufanya kwa kuwa mimi ni mgonjwa wa TB na nimeshauriwa nisifanye kazi kwa sasa, hivyo kuanzia kupika, kulima shambani na hata kutafuta cha kula anafanya yeye baada ya kurudi shuleni,” alisema bibi huyo.

Mwanafunzi huyo ambaye anasomeshwa na msamaria mmoja aliyejitokeza baada ya familia yao kushindwa kumlipia ada amewaomba watu walioguswa na maisha ya familia hiyo kumsaidia.

Akizungumza hivi karibuni Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama alikiri hali ngumu kwa kijana huyo kutokana na mazingira ya familia yao na kuongeza anahitaji kusaidiwa hata fedha za kujikimu na gharama zingine za masomo, kwani mfadhili humlipia ada pekee.

Mwenjuma Magalu: TAMWA Imerejesha Ndoto Zangu Kielimu
Mwanafunzi, Mwenjuma Magalu

Na Joachim Mushi, Handeni

“BAADA ya kumaliza darasa la saba nilichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakini sikufanikiwa kuendelea na elimu hiyo kutokana na uwezo wa mzazi wangu mmoja (mama) ambaye alishindwa kumudu gharama zilizokuwa zikihitajika kwa wakati…,”ndivyo anavyoanza kusimulia Mwenjuma Magalu akizungumza Kijijini Msasa, Wilaya ya Handeni.

Magalu anasema furaha zote alizokuwa nazo mwaka 2011 baada ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, iliyopo kijijini Msasa Wilaya ya Handeni zilikuwa zikiyeyuka kadri siku zilivyokuwa zikikaribia kufunguliwa kwa shule za sekondari.

Anasema hadi shule zinafunguliwa mama yake alikuwa hajakamilisha vitu vilivyokuwa vikihitajika shuleni ikiwa ni pamoja na fedha ya ada ya kuanzia shule. Kijana huyo ambaye alikuwa akiishi na mama yake pamoja na wadogo zake wawili walitelekezwa na babayao miaka kadhaa iliyopita kijijini hapo baada ya baba huyo kudai anakwenda kutafuta maisha nje ya kijiji chake.

Hata hivyo kwa kuonesha ana uchu na elimu kijana Magalu hakumuachia mamayake jukumu la kuitafuta ada peke yake, naye alifanya vibarua huku na kule kijijini Msasa kwa kuamini huenda angelipata kitu na kufanikiwa kuingia shuleni. Lakini ilishindikana kwake kutokana na uduni wa kipato kwa mamayake, kwani fedha ambayo mara nyingine Magalu aliipata kwenye vibarua ililazimika kununua chakula. Hii ilikuwa ni changamoto nyingine kwa familia ya kijana huyo mdogo.

Baada ya ndoto za kujiunga na shule kutoweka bila mafanikio, Magalu aliamua kufanya vibarua na kampuni ya Kichina iliyokuwa ikitengeneza barabara ipitayo karibu na kijijini chao. Magalu anasema ndoto yake ya shule ilikuja kurejeshwa na utafiti wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 kwa kushirikiana na waandishi wa habari.

Bibi Amina Mohamed (kulia) mlezi wafamilia ya mwanafunzi Mwenjuma Magalu akifanya mahojiano na  mwanahabari Joachim Mushi, kijijini Msasa,wilayani Handeni.

“Baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari aliyekuja kijijini kwetu Msasa na kumweleza hali halisi, kilio change kilisikika kwawasamaria na kujitokeza kuisaidia familia yetu…kwa sasa nimepata ufadhili wa kusomeshwa hadi kidato cha nne,” anasema Magalu.

Mwenjuma Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo muda mfupi baada ya kupata ufadhili wa masomo akiwa bado na furaha alijikuta anaingia katika mtihani mwingine wa maisha baada ya mamayake mzazi kufariki dunia.

Hata hivyo baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya Handeni na taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa kile mamayake (kwa sasa marehemu) kutokuwa na uwezo kuripotiwa, alijitokeza mfadhili wa kugharamia masomo yake ambaye hadi sasa anafanya hivyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni Komnyang’anyo, mwanafunzi huyo aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa umma na kupatikana kwa mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya familia yao kutelekezwa.

Kwa upande wake bibi wa mtoto huyo (Amina Mohamed) ambaye aliachiwa familia hiyo baada ya kufariki kwa mwanaye, anamshukuru mfadhili wa mjukuu wake. “Binafsi nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi shuleni…hii kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa amekata tamaa kabisa kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua mitaani huku wenzake wakiendelea na shule,” anasema bibi huyo.

Bibi huyo anafafanua kuwa kwa sasa bado familia hiyo inahitaji msaada wa huduma hasa baada ya mwanaye (mama wa familia hiyo) kufariki dunia mwaka jana na kumuachia watoto wake.

Anasema yeye ndiye aliyebaki kulea familia hiyo baada ya mtoto wake kufariki. Lakini kwa sasa hali ya afya yake si nzuri, licha ya uzee alionao amepimwa na kubainika ni mgonjwa wa TB ambapo ameanza kutumia dawa hivyo kwa hali yake ameshauriwa kupumzika.

Anasema baada ya kushauriwa na daktari kupumzika, mzigo wa malezi ya familia sasa umejikuta ukielekea kwa mjukuu wake Mwenjuma ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo.  Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa katika uchunguzi uliofanywa tena juzi na mwandishi wa makala haya bibi huyo anabainisha kuwa mjukuu wake anamzigo mkubwa.

“Nasema anamzigo mkubwa kwa kuwa sasa anatakiwa kutekeleza majukumu ya shule na nyumbani kama yeye ndiye mlezi wa familia…namuhurumia sana lakini sina cha kufanya. Anaporudi shuleni anatakiwa kutafuta chakula cha familia, yeye pia ndiye mpishi, mchota maji na ndiye mkulima,” anamzigo mzito kweli ndiyo maana wakati mwingine nalazimika kuingilia licha ya afya yangu.

Muhingo Rweyemamu ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, anasema tatizo la uduni wa maisha kwa familia katika wilaya hiyo lipo kwa kiasi kikubwa. Anabainisha kuwa kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni haina mfumo maalumu kwa ajili ya kusaidia moja kwa moja familia kama hizo.

Anasema kinachofanyika ni kuhamasisha ndugu, jamaa na marafiki kuendelea kutoa msaada kwa familia ambazo zimekuwa katika wakati mgumu kimaisha na kuitaji msaada. “Kwa ujumla tunatoa elimu ya kuhakikisha wazazi wanazaa watoto ambao wanaweza kuwamudu kimatunzo…wajua wakati mwingine umasikini katika familia hizi huchangiwa na wanaume kuzaa bila mpangilio, unakuta mwanaume anakuwa na familia zaidi ya moja wakati hana kipato cha kumudu familia hizo,” anasema Rweyemamu.

Anasema kwa kuwa hili limesha jitokeza wamejipanga kuziwezesha shule kufanya uzalishaji wa kilimo ili wanafunzi waanze kupata chochote wawapo shuleni, halmashauri imepata vocha takribani 300 ambazo zitasaidia upatikanaji wa pembejeo kwa shule zitakazokuwa zikizalisha mazao kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi kama chakula wawapo shuleni mchana.

Halmashauri pia imejipanga katika uhamasishaji kilimo kwa familia pamoja na uwezeshaji katika nyanja anuai ili kukabiliana na janga la njaa pamoja na ugumu wa maisha kiujumla.

Utafiti wa TAMWA Wamrudisha Mwanafunzi shuleni Handeni
Bibi wa mwanafunzi Mwenjuma Magalu, Amina Mohamed akizungumza na Mhariri wa mtandao wa Thehabari, Joachim Mushi (kulia) kijijini Msasa, wilayani Handeni juzi.

Mwenjuma Magalu (wa kwanza kulia mstari wa pili) ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo akiwa darasani na baadhi ya wanafunzi wenzake alipotembelewa na mwandishi wa habari hizi.

Na Thehabari.com, Handeni

UTAFITI wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 umefanikisha kumrudisha shuleni mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa ametelekezwa yeye pamoja na familia yao.

Mwenjuma Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo alitelekezwa na babayake yeye pamoja na mamayake mwaka jana, hivyo kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo licha ya kuchanguliwa kuendelea na masomo.

Hata hivyo baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya Handeni na taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na sekondari baada ya mamayake (kwa sasa marehemu) kukosa uwezo kuripotiwa, alijitokeza mfadhili wa kumsomesha ambaye anagharamia masomo yake hadi sasa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni Komnyang’anyo, mwanafunzi huyo aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa umma na kupatikana kwa mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya familia yao kutelekezwa.

“Binafsi nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi shuleni…hii kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa amekata tamaa kabisa kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua mitaani huku wenzake wakiendelea na shule,” alisema bibi wa mtoto huyo, Amina Mohamed akizungumza.

Bibi huyo akizungumzia maisha ya sasa ya familia hiyo alisema bado wanahitaji msaada wa huduma hasa baada ya mwanaye kufariki dunia mwaka jana na kumuachia watoto wake.

Aliongeza kwa sasa yeye ni mgonjwa wa TB anayetumia dawa hivyo kwa hali yake ameshauriwa kupumzika jambo ambalo limempa mzigo mkubwa kimajukumu mwanafunzi (Mwenjuma), kufanya kazi za nymbani kama kupika kulima na shughuli nyingine.

Hata hivyo mama wa mtoto huyo (Hadija Magalu) ambaye alitelekezwa na mzazi mwenzake alifariki dunia mwaka jana kwa tatizo la uzazi na kuiacha tena familia hiyo ya watoto watatu katika hali ngumu zaidi chini ya malezi ya bibi mzaa mama.

Wanafunzi wala mlo mmoja
Vyema viongozi wetu wakatumia muda mwingi kutafuta namna ya kutatua matatizo ya umasikini

Na Mwandishi wa Daraja

MOJA ya changamoto inayowakabili wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kipagalo na Shule ya Msingi Mahulu, zilizopo Makte Njombe ni kutopata chakula cha mchana wakiwa shuleni.

Akizungumza na Shirika la Daraja, Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kipagalo, Ayoub Honelo anaeleza kusikitika kwake kwa hali hiyo huku akieleza; “inaumiza sana kuona mwanafunzi wa bweni anapata mlo mmoja tu kwa siku, wakati ana tumia muda mwingi darasani na baadaye anahitaji muda mwingi wa kujisomea.

“Mwanafunzi akisha kula chakula cha usiku basi ni hadi tena usiku, wakati mwingine wanasinzia darasani kwa sababu ya njaa na hata wanapokosa kuwaadhibu ni kama kuwaonea tu” anasema mwalimu huyo.

Aidha, anaendelea kusema kuwa kuna kipindi wazazi na walimu walikutana na kujadili suala hilo na wakakubaliana kutoa mahindi katika kipindi cha mavuno, mwezi wa saba mwaka jana, lakini zoezi hilo liligonga mwamba kwa sababu wazazi baadaye walihisi walimu wana nia ya kuiba chakula chao

“Wazazi ni wazito sana hata kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto, kufuatilia afya zao pia ni kazi, kwa kweli serikali ya kijiji inapaswa kufanya kitu na kuchukua uamuzi juu ya hili” anasema Honelo

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahulu, Estobery Kimetelo anaeleza kuwa sababu kubwa inayofanya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mahulu kutokula chakula cha mchana ni wazazi kushindwa kuchangia chakula kutokana na kutokuwa na nguvu za kuzalisha ziada.

Pamoja na hayo imeelezwa kuwa madarasa yaliyopo katika shule hiyo yamechakaa kiasi kwamba hayafai kutumiwa kwa kuhofia kuwadondokea wanafunzi wakati wowote. Hata hivyo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuanza ujenzi wa madarasa mapya