Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania » Habari za Uchunguzi http://www.thehabari.com Habari Tanzania | Online Newspaper Sun, 07 Feb 2016 22:09:51 +0000 en-US hourly 1 http://wordpress.org/?v=4.2.7 JK Ateuwa Mkurugenzi Mkuu TEA http://www.thehabari.com/jk-ateuwa-mkurugenzi-mkuu-tea/ http://www.thehabari.com/jk-ateuwa-mkurugenzi-mkuu-tea/#comments Mon, 26 Oct 2015 22:47:46 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63262 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu ...

The post JK Ateuwa Mkurugenzi Mkuu TEA appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA). Uteuzi huo umeanza rasmi tangu Oktoba 18, mwaka huu, 2015.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari imeeleza uteuzi huo umeanza tangu Oktoba 18 na kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi hiyo ya TEA na ndiye amekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post JK Ateuwa Mkurugenzi Mkuu TEA appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/jk-ateuwa-mkurugenzi-mkuu-tea/feed/ 0
FemAct Watoa Tamko Kuhusiana na Katiba Pendekezwa http://www.thehabari.com/femact-watoa-tamko-kuhusiana-na-katiba-pendekezwa/ http://www.thehabari.com/femact-watoa-tamko-kuhusiana-na-katiba-pendekezwa/#comments Tue, 11 Nov 2014 20:31:43 +0000 http://www.thehabari.com/?p=53007 TAMKO LA FEMACT KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA MDAHALO KUHUSU KATIBA PENDEKEZWA KATIKA ...

The post FemAct Watoa Tamko Kuhusiana na Katiba Pendekezwa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
katiba

TAMKO LA FEMACT KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA MDAHALO KUHUSU KATIBA PENDEKEZWA KATIKA HOTEL YA BLUE PERL UBUNGO DAR ES SALAAM TAREHE 2 NOVEMBER 2014.

Sisi Mashirika yapatayo 50 yanayotetea Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Demokrasia, Utawala bora, Maendeleo na Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi ( FemAct ) tumekuwa tukifuatilia kwa karibu mchakato wa katiba unavyokwenda tangu ulipoanza. Pamoja na changamoto nyingi zilizojitokeza , bado kuna fursa ambazo wananchi wameweza kushirikishwa na kuleta matumaini ya kupata katiba mpya.
Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kwamba wakati mchakato ukikaribia kufikia mwisho , kumeanza kujitokeza matukio ya aibu na ya kusikitisha ambayo yanaweza kuchafua kabisa au kuharibu kazi nzuri ambayo ilikuwa imeanza kufanyika.
FemAct imesikitishwa na vurugu za hivi karibuni zilizosababisha kukatishwa kwa mdahalo wa kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa. Watu hao ni pamoja na mwandishi wa habari wa BBC aliyeumizwa, mwanamke moja aliyepigwa na kuangushwa pamoja na kuzingirwa kwa mlemavu wa macho aliyekuwa akishiriki katika mjadala huo.
Mdahalo huo uliokuwa ukirushwa mojakwamoja na redio na televisheni ulivurugika kutokana na kundi la vijana kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha hoja zake. Zomeazomea hiyo ilifuatiwa na vurugu ambazo zilisababisha mtafaruku na bugdha kubwa kwa washiriki wa mjadala huo.
Hali hii ni tishio kwa uhuru na haki kwa wananchi kujieleza, kutoa maoni na kujumuika katika kujadili masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa nchi yao. FemAct ikiwa ni muungano wa mashirika na asasi mbalimbali za kiraia, inalaani vikali vurugu hizo kwani zinaweza kusababisha machafuko nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na mchakato wa kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa.
Vurugu kama hizo zina ashiria tishio kwa wananchi hasa makundi yaliyoko pembezoni, wakiwemo wanawake, wazee, walemavu , wagonjwa , watoto , na makundi mengineyo. Ni dhahiri kuwa, makundi hayo na Watanzania kwa ujumla watagubikwa na hofu ya kushiriki katika kujadili katiba inayopendekezwa ambayo ndio msingi wa mustakabali wa nchi yao. Hali hii inaweza kusababisha watu au makundi yanayopenda kushiriki katika kujadili katiba pendekezwa kutojitokeza tena kwa hofu ya kufanyiwa fujo.
Aidha, kuhusu kufanyiwa fujo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji mstaafu Joseph Warioba, na watu wengine akiwemo mwanamke na mlemavu wa macho waliokuwa wanashiriki katika mjadala huo, kitendo hicho ni cha kidhalilishaji kinacholenga kufifisha maoni ya wananchi. FemAct ikiwa ni muungano wa watetezi wa haki za kijamii tunaamini kuwa mtu yeyoye ana uhuru wa kutoa maoni yake na kusikilizwa na watu wengine bila kufanyiwa vurugu, kudhalilishwa au kudhuriwa kwa namna yoyote.
Hofu yetu ni kwamba matukio kama haya yanawatisha wanawake , makundi yaliyoko pembezoni, na hasa walemavu kushiriki katika hatua zinazofuata ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa, kura za maoni na uchaguzi mkuu 2015 kikamilifu kwasababu watahofia kufanyiwa vurugu.
Kwa takribani miaka 10 iliyopita tumeshuhudia idadi ya wapiga kura nchini ikizidi kushuka badala ya kuongezeka licha ya kuwa idadi ya watu nchini kuongezeka. Sababu kama hizi za kuvuruga amani katika mikusanyiko ya wananchi, na mikutano ambayo wananchi wanapashana taarifa inafifisha ari ya wananchi kujitokeza na kutoa michango yao kidemokrasia.
Ili kuhakikisha mchakato huu unafanyika katika hali stahiki, na wananchi kushiriki kikamilifu chaguzi zinazokuja, FemAct inapendekezakuzingatiwa kwa masuala yafuatayo;
1. Uhuru wa wananchi wa Tanzania wa kujieleza na kutoa maoni yao , uheshimiwe katika kujadili mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yao ikiwemo katiba inayopendekezwa na makundi yote yakiwemo yaliyoko pembezoni yapewe nafasi na kuhakikishiwa usalama.
2. Vyombo vya usalama vihakikishe kuwa, usalama unakuwepo kwa wananchi muda wote wanaposhiriki katika mchakato wa kujadili na kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa pamoja na chaguzi zijazo.

3. Vijana ambao ni zaidi ya asilimia 65% ya idadi ya watu/watanzania nchini, waepuke kutumiwa na watu binafsi, vyama vya siasa au makundi fulani katika jamii ili kuepukana na kuharibika kwa hali ya usalama katika nchi yetu.

4. Vyama vya siasa au makundi yoyote kuacha mara moja kushiriki katika vitendo vya kiuchochezi au vinavyoweza kusababisha vurugu katika nchi yetu.

5. Wananchi waachwe wajadili kwa mapana maudhui ya Katiba inayopendekezwa bila kuwekewa mipaka au ukomo ili waielewe kabla ya kushiriki upigaji kura kama ilivyopendekezwa.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post FemAct Watoa Tamko Kuhusiana na Katiba Pendekezwa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/femact-watoa-tamko-kuhusiana-na-katiba-pendekezwa/feed/ 0
Tangazo Msiba wa Amin Elias Mbaga wa TTCL http://www.thehabari.com/tangazo-msiba-wa-amin-elias-mbaga-wa-ttcl/ http://www.thehabari.com/tangazo-msiba-wa-amin-elias-mbaga-wa-ttcl/#comments Wed, 15 Oct 2014 05:32:42 +0000 http://www.thehabari.com/?p=52050 MENEJIMENTI ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi ...

The post Tangazo Msiba wa Amin Elias Mbaga wa TTCL appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Amin Elias Mbaga

Amin Elias Mbaga


MENEJIMENTI ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao, Amin Elias Mbaga aliyekuwa Meneja Uhusino kilichotokea tarehe 13.10.2014 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Kumekucha
Ibada ya kumuombea marehemu itafanyika tarehe 15/10/2014 katika Kanisa la KKKT Sinza Kumekucha kuanzia saa saba mchana na baada ya ibada safari ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Same kwa maziko itaanza.
Maziko yanatarajia kufanyika katika kijiji cha Muhezi Mwembe Mlimali Same siku ya Alhamisi tarehe 16/10/2014.
Amin tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi pumzika kwa Amani. Amen
Imetolewa na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Tangazo Msiba wa Amin Elias Mbaga wa TTCL appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/tangazo-msiba-wa-amin-elias-mbaga-wa-ttcl/feed/ 0
Elimu ya Awali Tunduru na Changamoto Zake http://www.thehabari.com/elimu-ya-awali-tunduru-na-changamoto-zake/ http://www.thehabari.com/elimu-ya-awali-tunduru-na-changamoto-zake/#comments Sun, 05 Oct 2014 05:51:43 +0000 http://www.thehabari.com/?p=51661 Na Joachim Mushi, Tunduru WADAU wa elimu nchini Tanzania wanaamini kwa kiasi ...

The post Elimu ya Awali Tunduru na Changamoto Zake appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mwalimu wa darasa la awali wa Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi (kulia) akiwa na wanafunzi wake eneo ambalo hutumika kama darasa la wanafunzi hao.

Mwalimu wa darasa la awali wa Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi (kulia) akiwa na wanafunzi wake eneo ambalo hutumika kama darasa la wanafunzi hao.

Na Joachim Mushi, Tunduru

WADAU wa elimu nchini Tanzania wanaamini kwa kiasi kikubwa kwamba endapo elimu ya awali (chekechea) nchini Tanzania itatolewa katika misingi inayostahiki itakuwa ni njia moja wapo madhubuti ya kuimarisha ubora wa elimu. Hii ndiyo maana wanaendelea kupaza sauti wakiitaka serikali kupitia vyombo husika kuboresha kwanza elimu ya awali kabla ya kupanda ngazi nyingine za juu.

Huenda kilio hiki cha wadau wa elimu kimeanza kusikika serikalini. Kwani tayari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliagiza tangu mwaka 2010 kuwa kila shule zake za msingi ni lazima lianzishwe darasa la awali ili kuwenza kuwaandaa wanafunzi kuingia na darasa la kwanza. Awali elimu hii ilikuwa ikitolewa kwa kiasi kikubwa na taasisi na vikundi mbalimbali na hata watu binafsi nje ya shule za msingi, tena kwa hiyari. Kwa sasa sera na miongozo ya elimu inatamka wazi kuwa nilazima kila shule ya msingi iwe na darasa la awali kwa ajili ya elimu hiyo muhimu.

Changamoto kubwa iliyoibuka kwa sasa baada ya utekelezaji wa agizo hilo ni namna elimu hiyo inavyoendeshwa kwa kusuasua kwenye baadhi ya shule za Serikali. Hivi karibuni mwandishi wa makala haya alitembelea baadhi ya shule za msingi zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuangalia hali ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Uchunguzi ulibaini zipo shule ambazo licha ya kusajili wanafunzi wa awali kila mwaka hazina madarasa ya kusomea kwa watoto hao, hali ambayo inafanya wanafunzi hao wadogo kufundishwa katika mazingira magumu na kudhohofisha lengo zima la utoaji wa elimu hiyo. Wapo wanafunzi ambao hulazimika kufundishiwa nje, yaani chini ya mti ama kwenye magofu (majengo ya shule ambayo hayajakamilika) iwe madarasa au nyumba za walimu.

Teckla Milanzi ni mwalimu wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya. Anasema kimsingi wanafunzi wa darasa la awali shuleni hapo wanasomea chini ya mti kwa kuwa hawana darasa maalum kwa wanafunzi hao. Anasema wakati wa mvua ama jua kali mara nyingine hulazimika kuhairisha masomo kwa siku kutokana na hali ya hewa.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko wakiwa darasani kama walivykutwa na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko wakiwa darasani kama walivykutwa na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

Anasema anashukuru kwa sasa wanajihifadhi kwenye jengo moja ambalo linaendelea na ujenzi shuleni hapo, jengo ambalo hata hivyo mara baada ya ujenzi kukamilika na wahusika kukabidhiwa darasa watarudi kusomea chini ya mti kama ilivyo ada. Hata hivyo, anasema licha ya changamoto hiyo darasa hilo halina vitabu kwa ajili ya kufundishia wanafunzi, bali kuna nakala moja moja kwa baadhi ya masomo ambavyo vilitafutwa kwa jitihada za mwalimu mwenyewe.

“Mfano kwa vitabu vya Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Hisabati kuna nakala moja moja tu, ambazo hutumiwa na mwalimu mwenyewe. Anasema darasa hilo licha ya kuwa na changamoto kedekede hata kwenye mgao wa fedha zinazoletwa shuleni kila mara halimo hivyo hakuna kinacholetwa tofauti na wanafunzi wengine,” anasema Bi. Teckla Milanzi.

Kwa upande wake, Mwalimu Christina Komba wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko anasema madarasa ya elimu ya awali Wilayani Tunduru yanakabiliwa na changamoto nyingi. Anabainisha kuwa madarasa mengi likiwemo lake hawana vitabu wala miongozo ya namna ya ufundishaji kabisa zaidi ya kila mwalimu anayefundisha kubuni nini afundishe kila uchao.

“…Kwanza licha ya kutokuwa na vifaa vingine hatuna chumba maalumu cha wanafunzi hawa (darasa) kwa sasa tunatumia jengo la darasa ambalo bado linaendelea na ujenzi na hata hivyo jengo hili halijengwi kwa ajili ya wanafunzi wa awali,” anasema mwalimu Christina Komba.

Wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya, wakiwa katika darasa lao.

Wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya, wakiwa katika darasa lao.

“Madarasa ya elimu ya awali hayana vitabu, hayana miongozo…huwa tunaanzima au ukipata hela yako wewe binafsi unaenda kununua kitabu kimoja au viwili ili uweze kuwasaidia watoto. Na baadhi ya masomo hayana vitabu kabisa hata ukienda madukani katika Wilaya yetu (Wilaya ya Tunduru) vitabu kama Haiba na Michezo, pamoja na Sanaa hazipo kabisa madukani. Anasema uongozi wa juu wilayani unalitambua hilo.

Batadhari Mkwela ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nanjoka anasema usajili wa wanafunzi wa awali kila mwaka huongezeka japokuwa bajeti ya kuendesha elimu hiyo ni changamoto. “…Darasa la awali linahitaji vitendea kazi lakini havipo, hatuna vifaa kama vitabu vya kutosha, vyenzo za kufundishia, hakuna bajeti hata ya vifaa hivi toka Serikalini, hatuna madawati maalum kwa ajili ya wanafunzi wa awali,” anasema Mkuu huyo wa Shule ya Nanjoka.

Hadija Makamla ni mwalimu wa darasa la awali Shule ya Msingi Majengo. Mwalimu huyu ambaye amehitimu kozi ya kufundisha darasa hilo, anasema anavyo baadhi tu ya vitabu vinavyoitajika katika darasa hilo. Anabainisha kuwa darasa hilo lina jumla ya wanafunzi 48 lakini hutumia darasa la wanafunzi wa kawaida maana hawana darasa lililojengwa maalum kwa wanafunzi wa awali.

“…Ninazo nakala chache kwa ajili ya mwalimu tu ila wanafunzi hawana hata kimoja…lakini kuna masomo mengine sina vitabu kabisa kama vile Sanaa na Haiba ya Michezo sina kabisa hata mimi,” anasema mwalimu Makamla. “…Unajua watoto kwa kiasi kikubwa wanajifunza kwa vitendo, picha na uhalisia, sasa huenda tunavyowapa ni vikubwa zaidi au vidogo sana kwa sababu ya kubuni mada kwa baadhi ya masomo.

Dorothea George ni mwalimu wa darasa la awali shule ya Msingi Nanjoka Wilayani Tunduru. Yeye anasema japokuwa hakuwahi kufanya kozi ya ualimu wa awali kwa sasa amekabidhiwa darasa hilo kulifundisha katika shule yake. Anasema darasa hilo kwa sasa lina wanafunzi 98 ambao wanasomea darasa moja chini ya mwalimu mmoja.

Anasema licha ya darasa hilo kuwa na madawati kadhaa lakini si maalum kwa ajili ya wanafunzi wa awali bali ni ya wanafunzi wa kubwa, hata hivyo bado kuna watoto wanalazimika kukaa chini kwa kile kukosa madawati ya kutosha katika shule hiyo. Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali anasema uendeshaji wa darasa la awali shuleni hapo ni wa kusuasua kutokana na changamoto anuai zinazowakabili. Hakuna bajeti inayoingia kuisaidia elimu hiyo, ispokuwa mwaka huu waliletewa madawati kumi kwa ajili ya elimu ya awali.

Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, Abdul Kazembe akizungumza na mwandishi wa makala haya (hayupo pichani) ofisini kwake hivi karibuni.

Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, Abdul Kazembe akizungumza na mwandishi wa makala haya (hayupo pichani) ofisini kwake hivi karibuni.

“…Uendeshaji elimu ya awali hapa ni wa wastani kwa kweli kutokana na changamoto zinazotukabili, kwanza vifaa vya kuwafundishia watoto hawa ni tatizo na wazazi kwa eneo hili wamekuwa hawana mwamko wa elimu hii kabisa. Kwanza hawachangii michango ya chakula kama inavyotakiwa ili mtoto apate chochote awapo shuleni,” anasema mwalimu Mkali.

Anabainisha kuwa watoto pia wanatakiwa kupata uji wawapo shuleni lakini uchangiaji kwa wazazi nao umekuwa tatizo kubwa. “…Wapo wanaochangia wengine wanagoma tunasukumana hivyo hivyo na mambo yanasonga mbele…lakini kutokana na uchangiaji duni kuna baadhi ya siku wanapata uji na sikunyingine hawanywi kutokana na ugumu wa michango,” anasema mwalimu George.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko, Adam Hausi katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya anasema uendeshaji wa elimu ya awali katika shule hiyo ni juhudi binafsi za mwalimu wa darasa hilo. Anasema darasa hilo halina bajeti yoyote kutoka serikalini hivyo hakuna vitabu na vitendea kazi vingine vinavyohitajika.

“…Vitendea kazi ndio tatizo kabisa, ila mwalimu anafundisha kwa jitihada zake na darasa linaendelea. Alafu lina idadi kubwa sana ya wanafunzi (84) na anafundisha peke yake…,” anasema Hausi. Anasema uboreshaji elimu ya msingi ni suala la ushirikiano kati ya Serikali na jamii yenyewe lakini wakati mwingine Serikali inakwamisha juhudi hizo kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo baadhi ya maeneo.

“…Mfano sisi tulijenga madarasa mawili kwa nguvu za wananchi hadi yamekamilika ilipofika suala kuezekwa tokaomba msaada wa Serikali pamoja na kumaliziwa ili yaanze kutumika ilikuwa kazi kweli tulizunguzwa sana hadi tukaanza kuyatumia hivyo hivyo,” alisema.

Bi. Thabita Farara ni Mkazi wa Kata ya Mringoti Mashariki anasema bado mwamko wa elimu ya awali kwa wazazi ni mdogo, maana wazazi wengi wamekuwa wakijiandaa na darasa la kwanza tu kumuandikisha mtoto. Kwa upande wake Asha Komba Mkazi wa Tunduru Stendi anasema yeye anaitambua elimu ya awali na kuikubali lakini ni ile inayotolewa na shule binafsi kama za taasisi. Lakini ile inayotolewa kwenye shule za Serikali ni tatizo kubwa maana hazizingatii ubora wa elimu zaidi ya kuwalundika watoto tu darasani.

“…Mimi naitambua elimu ya awali na watoto wangu wote wamepitia lakini huwa tunawapeleka kwenye chekechea za taasisi mbalimbali kama zinazomilikiwa na makanisa majeshi na zinginezo maana huku ndiyo kidogo mtoto anaandaliwa…kule Serikalini kwanza unakuta darasani wapo kibao alafu muda wote wanacheza tu si kujifunza,” anasema Bi. Komba.

Abdul Kazembe ni Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, anasema kwa sasa kila shule ya msingi sera inaelekeza lazima iwe na darasa la awali. Anasema hata katika usajili wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa sasa watoto wa mwanzo kusajiliwa ni wale waliopata elimu ya awali katika shule husika.

“…Kwa hiyo kuna umuhimu wa kila shule kuwa na darasa la awali…changamoto sasa inakuja kwenye vitendea kazi, kwa mwaka 2013 na kurudi nyuma uwepo wa ‘capitation’ ulikuwa pia unaelekeza watoto wa awali wapo mule na hata tunapotoa takwimu za awali tulianza na ‘pre-primary’ (wanafunzi wa awali) hivyo wenyewe wapo, tatizo hapa ni ujaji wa pesa yenyewe ya ‘capitation’ haitimii kama inavyo elekeza, yaani ile wastani ya kwamba kila mtoto apate shilingi 10,000 kwa mwaka hautimii,” anasema.

Anatolea mfano mwaka 2013/14 kiwango cha fedha ambacho kilitakiwa kuja katika halmashauri ya wilaya hiyo ni zaidi ya milioni 366.7. Kiwango hiki ni kile kilichoidhinishwa katika bajeti tu lakini ukirudi kwenye mahitaji halisi ni zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa. Anasema kilichokuja ni zaidi ya milioni 196.5 fedha ambayo ni karibia nusu ya kiasi kilichopitishwa kwenye bajeti. Anabainisha hilo ndilo tatizo kubwa kwani hata fedha ambazo zimepitishwa haziji kama ilivyopitishwa kwenye bajeti.

“…Kwa hiyo unaweza kuona kwamba ni ngumu kuigawa fedha hii katika matumizi maana kwanza haitoshi na pili hata kilichotegemewa kuja ni pungufu zaidi tena sana, sasa sijui unaweza kugawa kila shule ipate shilingi ngapi…kwani haitoshelezi,” anasema.

Anasema kwa upande mwingine miundombinu ya madarasa ni changamoto kubwa. Kwa mwaka 2013 idadi ya mahitaji ya madarasa kwa wilaya nzima ilikuwa ni 1,715 lakini ukiangalia vyumba vya madarasa vilivyopo ni kama 900 na kitu na mengine ni ya muda mrefu sana kiasi ambacho yanaelekea kuchakaa jambo ambalo pia yanapungua.

Aidha anaeleza kuwa ukienda kwenye bajeti ya ujenzi wa madarasa mapya milioni 171 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na miundombinu mbalimbali kiasi hiki cha fedha waweza kuta kinauwezo wa kujenga madarasa kama nane tu. Kiasi hicho cha fedha ni pamoja na ujenzi wa nyumba tano za walimu. Na kiasi hicho cha fedha za ujenzi ni pamoja na kumalizia miradi viporo za nyumba za walimu na vyumba vya madarasa. Anasema upungufu wa vyumba vya madarasa eneo hilo ni karibia madarasa 800.

“Sasa kwa ujumla unaweza kuona kuwa miundombinu pale shuleni haitoshelezi, ni jambo la kawaida kuona walimu wakiacha ofisi itumike kama darasa au darasa litumike kama ofisi. Huku kwa awali ni changamoto zaidi maana licha ya upungufu wa vyumba hata wazazi hasa vijijini wanashindwa kuchangia chakula (uji) kwa watoto wao unaweza kukuta wameandikishwa wengi Januari lakini kila muda unavyozidi kwenda watoto wanapungua na unaweza kukuta hadi mwezi Juni darasa linapotea kabisa kwa utoro,” anasema.

Kazembe anabainisha kuwa kuna jumla ya shule za msingi 144 katika wilaya hiyo, huku shule zilizo na vyumba maalumu vya madarasa ya awali zikiwa 16 tu. Anasema shule nyingine zote hazina vyumba vya madarasa ya awali na matokeo yake ama wanatumia madarasa ya msingi kwa kupishana.

Anaongeza kuwa uhamasishaji wa ujenzi wa madarasa ya awali na umuhimu wa elimu hiyo unatolewa kwa walimu, wazazi na kamati za shule kupitia vikao mbalimbali ambapo mara nyingi uongozi uhimiza wazazi kuchangia zaidi nguvu zao katika kukamilisha ujenzi wa madarasa ya awali, utengenezaji wa madawati na upatikanaji wa chakula cha mchana na uji shuleni.

“…lakini tunaangalia sana chakula maana watoto hata kwenye mti wanaweza kukaa wakasoma endapo wanamadawati pale au wamekaa chini kwenye kivuli, japokuwa si mazingira mazuri sana shuleni…lakini wakiwa na chakula hata utoro unapungua,” anasema.

Anasema kwa mwaka 2013 serikali ilikumbuka kuleta fedha kwa ajili ya ununuzi madawati ya wanafunzi wa awali, fedha ambazo tulizigawa na kununua baadhi ya vitabu vya awali na madawati kwenye shule ambazo zinamadarasa hai ya awali. Shule zilizonufaika na mgao huo ni shule za mjini Tunduru tu ambazo nyingi ndizo zenye madarasa hai ya awali. Anasema ili kukabiliana na hali ya upungufu wa walimu wa awali; imepitishwa walimu wa gredi ‘A’ kufundisha madarasa hayo kwa kuwa wao mafunzo yao katika kozi hujumuisha ufundishaji darasa la awali, tangu walioitimu mwaka 2013.

“…sasa wakati mwingine unaweza kukuta mwalimu ni gradi A na kimsingi yeye anao uwezo wa kufundisha darasa la awali, lakini wengine hawakubali hadi aone ana cheti kabisa maalumu cha kufundisha darasa la awali…ukimuuliza huyu atakwambia yeye hana taaluma ya kufundisha awali jambo ambalo si sawa,” anasema Ofisa Elimu huyo wa Msingi.

“..Kwa suala la vitabu kweli hii ni changamoto, hapo nyuma tulikuwa tunanunua vitabu wenyewe wakini kwa sasa TAMISEMI wenyewe moja kwa moja wananunua na kuvileta. Sasa huku kwetu ni nadra sana kuona wazabuni wetu wanaleta vitabu vya awali kwa sababu soko lake ni dogo sana kutokana na idadi ndogo ya uwepo wa elimu hii ya awali eneo husika,” anasema.

Hata hivyo umeona unafuu maeneo ya mjini mzazi anatambua umuhimu wa elimu hivyo anaweza kuchonga dawati kwa ajili ya mtoto wake lakini kwa vijijini hali ni mbaya zaidi. Mzazi ukimwambia achangie dawati anakushangaa na pia haoni umuhimu huo.

“…Nikwambie unajua Wilaya ya Tunduru mzazi mtoto wake akifeli anafurahi sana…tena baadhi wanaona kama ni sherehe, kwanza wakifanya mtihani tu wa la saba barabarani akina mama wanashangilia wanaona wametua mzigo, unaweza kujiuliza wazazi wanaoshangilia inamaana walikuwa wakiona ni adhabu watoto wao kuwa shule? Lakini pia mtoto akisha faulu kwenda shule hapelekwi hadi DC aunde kamati, atembee na hakimu na polisi kukamata wazazi wanaogoma kusomesha watoto watishiwe ndo wanakubali kusomesha…lakini kitendo cha wazazi kukamatwa kushikiliwa kwa kushindwa kuwapeleka watoto shule wamegeuka na kuwarubuni watoto wao wasifaulu,” anasema.

Anabainisha kuwa ni kweli Serikali ina jukumu la elimu, lakini mzazi kwa upande wake anajukumu zaidi, kuangalia mtoto wake anapata elimu gani na ya kiwango gani na kama mzazi hayupo tayari basi haiwezekani na wakati mwingine inakuwa ngumu. Kimsingi jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia watoto wa awali zipo, lakini upatikanaji wa fedha ndio.

Salum Mtutula ni Mbunge wa Tunduru Kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge huyu katika mahojiano anakiri kuwa elimu ya awali ni muhimu na msingi mzuri wa mtoto kielimu. Anasema mtoto anapopata elimu nzuri ya awali huwa na msingi mzuri kielimu katika masomo yake ya mbele.
“…Ili mtoto apate elimu bora ni lazima apate elimu ya awali inayostahiki…hakiwa na msingi mbaya wa elimu ya awali kuna uwezekano mkubwa way eye kufanya vibaya pia,” anasema Mtutula.

Hata hivyo anaishauri Serikali kuingiza suala hili katika sheria na kanuni zake kuwa kila shule ya msingi inapoanzishwa ianze na darasa la awali kwanza ndipo madarasa mengine yafuate. “…Mimi nitafurahi kama suala hili tutaliweka kwenye sheria au kanuni zetu kuwa kila shule ya msingi inapoanzishwa basi lazima ianze na darasa la awali ndipo madarasa mengine yafuate iwe shule za Serikali au binafsi,” anasema Mbunge Mtutula.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Elimu ya Awali Tunduru na Changamoto Zake appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/elimu-ya-awali-tunduru-na-changamoto-zake/feed/ 0
Askari Mtunza Silaha Dodoma Akamatwa Akiwinda Haramu na Silaha ya Kivita http://www.thehabari.com/askari-mtunza-silaha-dodoma-akamatwa-akiwinda-haramu-na-silaha-ya-kivita/ http://www.thehabari.com/askari-mtunza-silaha-dodoma-akamatwa-akiwinda-haramu-na-silaha-ya-kivita/#comments Tue, 26 Aug 2014 04:52:41 +0000 http://www.thehabari.com/?p=50093 *Akutwa na silaha ya kivita Na Mwandishi Wetu, Dodoma ASKARI wa Jeshi ...

The post Askari Mtunza Silaha Dodoma Akamatwa Akiwinda Haramu na Silaha ya Kivita appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Silaha aina ya G3

Silaha aina ya G3


*Akutwa na silaha ya kivita

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

ASKARI wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma ambaye ni mtunza silaha wa Wilaya ya Dodoma mjini, Meja George Andala pamoja na raia sita wamekamatwa katika pori la Hifadhi ya Taifa lililopo wilaya ya Chamwino wakiwinda wanyama bila kibali kwa kutumia sila ya kivita.

Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu umezipata, Meja Andala ambaye alikamatwa na silaya kubwa ya Jeshi la Polisi, aina ya G3 alikamatwa na kikosi maalumu cha kuzuia uhalifu nchini akiwa katika pori hilo. Taarifa zaidi zinasema Meja Andala ambaye pia kimajukumu ni Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Wilaya ya Dodoma na amekamatwa akifanya kosa hilo akiwa katika likizo ya kustaafu aliyoianza tangu Juni, 2014.

“…Tumemkamata akiwa na vijana wengine sita ambao walikuwa pamoja wakifanya uhalifu huo, wote bado tunawashikilia kwa uchunguzi zaidi,” kilisema chanzo chetu cha habari japokuwa kiligoma kutaja eneo ambalo kwa sasa watuhumiwa wanashikiliwa.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu mjini hapa umegunduwa Meja Andala na raia wenzake 6 wako mahabusu ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Chamwino na juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi kuzungumzia tukio hilo ziligonga mwamba. Hata hivyo bado mwandishi wetu anaendelea kumtafuta kwa ufafanuzi zaidi.

Matukio ya uwindaji haramu yamekuwa yakiendelea kushamiri katika hifadhi mbalimbali za taifa huku yakiteketeza wanyama na uharibifu mkubwa katika hifadhi hizo. Hata hivyo vitendo vya uwindaji haramu vimekuwa vikihusishwa na viongozi na watendaji wa Serikali ambao wanafadhili mitandao hiyo ya uwindaji. Taarifa zaidi juu ya tukio hilo endelea kufuatilia hapahapa Thehabari.com.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Askari Mtunza Silaha Dodoma Akamatwa Akiwinda Haramu na Silaha ya Kivita appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/askari-mtunza-silaha-dodoma-akamatwa-akiwinda-haramu-na-silaha-ya-kivita/feed/ 0
Mwanafunzi Miaka 13 Msingi Abebeshwa Mimba, Afaulu Sekondari…! http://www.thehabari.com/mwanafunzi-miaka-13-msingi-abebeshwa-mimba-afaulu-sekondari/ http://www.thehabari.com/mwanafunzi-miaka-13-msingi-abebeshwa-mimba-afaulu-sekondari/#comments Fri, 08 Aug 2014 21:01:34 +0000 http://www.thehabari.com/?p=49442 Na Joachim Mushi, Newala MIMBA za umri mdogo ambazo zimekuwa zikiwakatisha wanafunzi ...

The post Mwanafunzi Miaka 13 Msingi Abebeshwa Mimba, Afaulu Sekondari…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mwanafunzi huyo akiwa na mwanaye akizungumza na mwanahabari Joachim Mushi, Kijijini Newala

Mwanafunzi huyo akiwa na mwanaye akizungumza na mwanahabari Joachim Mushi, Kijijini Newala

Na Joachim Mushi, Newala
MIMBA za umri mdogo ambazo zimekuwa zikiwakatisha wanafunzi masomo Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara bado ni tatizo. Matukio ya mimba hizi kwa wanafunzi mbali ya kuwakatisha masomo yao zimekuwa zikitishia afya zao pia. Fatuma Rashid, 14(si jina lake halisi) ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kipimi, Kata ya Makote Wilayani Newala ambaye alimaliza elimu ya darasa la saba Septemba 2013 huku akiwa mjamzito pasipo walimu kujua.
Baada ya matokeo kutoka Fatuma amejikuta amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Makote Day iliyopo Kata ya Makote, lakini ameshindwa kuendelea na shule baada ya mimba kumkatisha masomo yake. Uchunguzi unaonesha Farida alipata ujauzito tangu mwezi Agosti 2013 na alianza kuhudhuria kliniki kwa siri huku akiendelea na masomo yake ya msingi hadi alipofanya mitihani yake ya mwisho shule ya msingi iliyofanyika Septemba 19 na 20, 2013.
Taarifa zinaonesha farida alisajiliwa katika daftari la wajawazito Zahanati ya Makote tangu mwezi wa Agosti 2013 ambapo alieleza kuwa ana umri wa miaka 13. Hata hivyo baada ya kurudi nyumbani alibadili umri wake kwenye kadi ya kliniki ya waja wazito na kuandika kwa wino mweusi kuwa alikuwa na miaka 15 badala ya 13 aliyotaja mwenyewe siku ya kwanza kliniki.
Hata hivyo akiwa anaenda katika mahudhurio ya kliniki akilea mimba yake alifanikiwa kubadili tena umri wake katika kitabu cha zahanati na kuandika umri wa miaka 15. Haikujulikana alimshawishi nini nesi hadi kumbadilishia umri na kumuongezea miaka miaka miwili.
Mwandishi wa makala haya alifanikiwa kupata kadi ya kliniki ya mama ambayo ilionesha wazi kuwa umri ulioandikwa awali ilikuwa ni miaka 13 kwa wino wa bluu lakini sasa umebadilishwa na kwenye tatu kuandikwa 5 kwa wino mweusi. Mtoto Farida amefanikiwa kujifungua mtoto wa kiume Aprili 24, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Newala na kwa sasa analea mtoto akiwa nyumbani kwa shangazi yake Kijiji cha Kipimi.
Mazungumzo ya Fatuma na mwandishi wa makala haya yaliyofanyika mwezi Mai, 2014 kijijini Kipimi anaeleza kuwa ana umri wa miaka 17 na anasema alizaliwa 1995 jambo ambalo kiuhalisia haliendani. Kama kweli Farida alizaliwa mwaka anaoutaja yeye (1995) alipaswa kuwa na miaka 19 na si 17 kama anavyosema.
Kimsingi inaonesha wazi kuwa taarifa anazozitoa juu ya umri wake ni za uongo, na yaelekea anafanya hivyo kwa makusudi kuficha umri mdogo alionao yaani miaka 14 tena akiwa mwanafunzi kubeba mimba. Fatuma akifafanua zaidi katika mazungumzo yake anaweka wazi kuwa alianza uhusiano wa kingono na Ramadhani Zawadi (26) ambaye ndiye baba wa mtoto aliyekatisha masomo ya Farida, tangu mwaka 2012 akiwa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kipimi.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi Kipili waliozungumza na mwandishi wa makala haya.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi Kipili waliozungumza na mwandishi wa makala haya.

Taarifa iliyopatikana kutoka katika shule ya msingi aliyomaliza Fatuma zinathibitisha kuwa mwanafunzi huyo ni miongoni mwa mabinti waliochaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Makote Day, licha ya yeye kushindwa kuendelea na masomo kutokana na hali aliyonayo kwa sasa.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Makote Day, Said Ntinika akizungumza na mwandishi wa makala haya alithibitisha kuwa Farida ni miongoni mwa wanafunzi waliochaguliwa katika shule hiyo kuendelea na masomo ya sekondari, lakini anasema hadi kufikia mwezi Mei mwishoni, 2014 alikuwa hajaripoti shuleni na shule haina taarifa zozote juu ya mwanafunzi huyo.
Matukio ya mimba utotoni hayajamuathiri Fatuma pekee wilayani Newala. Wapo wasichana wengi kama yeye ambao wanakatishwa masomo wakiwa shule za msingi au sekondari kutokana na matukio ya mimba katika umri mdogo.
Faudhia Hashim, 14 (si jina lake halisi) ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Makote Day, lakini mwanafunzi huyu ameshindwa kuendelea na masomo yake baada ya kupata ujauzito akiwa katika harakati za usajili kuingia shuleni.
Maimuna Said (30) ni Mkazi wa Kata ya Makote Wilaya ya Newala na miongoni mwa wazazi ambaye mtoto wake naye aliwahi pata mimba shule ya msingi. Mama huyu akizungumza, anasema alibaini mwanaye ni mjamzito akiwa katika mchakato wa kumsajili kuingia kidato cha kwanza Sekondari ya Makote Day baada ya kufaulu akitokea Shule ya Msingi Kipimi.
Anasema alikuwa katika hatua za mwisho kumsajili kujiunga na sekondari ndipo alibaini kuwa ni mjamzito baada ya majirani kumshauri kuwa akampime.
“…Walianza kumshitukia majirani zangu wakaniambia kabla ya kumpeleka huko sekondari alipochanguliwa nikampime mimba maana wao wanaona huenda akawa mjamzito kulingana na mabadiliko ambayo anayaonesha, nilimchukua na kumpeleka zahanati na baada ya kumpima waliniambia ni mjamzito…tangu nimeambiwa nimeshindwa nifanye nini lakini tayari nimemjulisha mjomba wake,” anasema Bi. Maimuna.
Katika mazungumzo na Faudhia anajaribu kuficha umri wake halisi kwa mwandishi, yeye anadai anaumri wa miaka 15 kauli ambayo inapingana na mmoja wa ndugu wa familia hiyo, ambaye anasema binti huyo ana miaka 14. Sijui ni kwanini binti huyu anajiongezea miaka. Huenda hii ni tabia ya mabinti wengi wa eneo hili wanaopata mimba utotoni kwa kile kuhalalisha wao kubeba ujauzito. Faudhia si wa kwanza, kuficha miaka yake halisi maana hata Fatuma alidanganya umri mwanzo wa makala haya.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Newala, Dk. Yudas Ndungile anasema tatizo la mimba za umri mdogo au mimba utotoni ni kubwa kwa wastani eneo hilo. Anasema idadi ya wateja (wagonjwa) wanaokuja kujifungua hospitalini hapo chini ni umri wa miaka 18 ni wengi.
“…Kimsingi tatizo la mimba katika umri mdogo lipo na ni kubwa kwa wastani, idadi ya wanaokuja kujifungua wakiwa na umri wa chini ya miaka 18 ni wengi, wapo wengi na kwa utaratibu ambao tumejiwekea kwamba mama yeyote aliyepata ujauzito chini ya miaka 20 anapazwa kujifungulia katika hospitali ya wilaya au kwenye kituo cha afya. Tunafanya hivi maana endapo mtu huyu atapata matatizo wakati wa kujifungua kutokana na umri wake atafanyiwa upasuaji wa dharura,” anase Dk. Ndungile.
Anasema wajawazito wengi chini ya umri unaostahili wanaokuja kujifungua hupata tatizo la kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida, pia wanashindwa kuwajibika katika kutunza mtoto kama mama hasa siku za mwanzo na wengine hata kusababisha mtoto mchanga kupata maambukizi na hata kufariki. Anaongeza kuwa hata wanaofanikiwa kujifungua kwa njia ya kawaida nao hupata tatizo la kuchanika na kutokwa na damu nyingi wakati wakijifungua jambo ambalo anasema ni hatari kiafya.
Anasema ili kukabiliana na mimba za umri mdogo idara yake imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na malezi kwa njia ya ushauri katika zahanati, vituo vya afya na hospitali zoezo ambalo linafanyika muda wote wa huduma katika vitengo husika.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Newala, Bi. Christina Kambuga akizungumza na mwandishi wa makala haya (hayupo pichani)

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Newala, Bi. Christina Kambuga akizungumza na mwandishi wa makala haya (hayupo pichani)

Anasema mimba za umri mdogo eneo hilo zinachangiwa na mambo mengi ikiwemo hali ya kiuchumi (duni) kwa familia husika, elimu duni kwa jamii ambapo idadi kubwa ya wanaopata mimba za umri mdogo hawajafika sekondari na pia wazazi wanashindwa kutimiza wajibu wao kwa familia. Anabainisha idara yake pia inaendelea kutoa elimu kupitia majukwaa mbalimbali vikiwemo vikao vya wadau anuai wa elimu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Newala, Bi. Christina Kambuga katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya ofisini kwake, anakiri ukubwa wa tatizo la mimba utotoni hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika eneo hilo.
“…Tatizo la mimba za utotoni hili limekuwa ni tatizo kubwa hasa kwa shule zetu za msingi na sekondari lakini hata na kwa jamii kwa ujumla, watoto waliowengi huku wanazaa chini ya umri unaostahili mpaka imefikia mahali kuna watoto wanazaa chini ya miaka 12, hili ni tatizo kubwa ambalo lipo hapa (Newala),” anasema.
Bi. Kambuga anasema tatizo kubwa linalochangia hali hiyo ni mmomonyoko wa maadili ambalo ni tatizo kubwa, likifuatiwa na suala la uendelezaji mila na desturi za watoto kushiriki katika jando wakiwa na umri mdogo. Kuanza kwa unyago na jandoni huko nyuma ilikuwa ni ujenzi wa maadili, na watoto walikuwa wanapelekwa huko wakiwa na umri mkubwa jambo ambalo kwa sasa linafanyika kinyume, hivyo watoto kupelekwa wakiwa na umri mdogo. Sasa unakuta uwezo wa kushika wanayofundishwa na kuyatafakari na hata kuyatumia wakati mwingine inakuwa ni tatizo. Yaani badala ya kuyatumia yanavyotakiwa yawe na kwa wakati wake watoto wamekuwa wakiyajaribu muda mfupo baada ya kutoka jandoni na unyagoni.
Anasema tatizo jingine ni jamii yenyewe kulea maovu ya mimba za utotoni. Wapo wazazi ambao hawatoi ushirikiano sheria zichukue mkondo wake pale inapotokea wanafunzi hawa wanabebeshwa mimba, na wazazi wengine wamekuwa hata wakiwashauri waliowapa mimba wanafunzi kutoroka mara baada ya kuona vyombo husika vinafuatilia.
Anasema wakati mwingine hata vyombo vya dola vinapojitahidi kufanya kazi yake na kufikisha kesi hizo mahakamani watoa ushahidi ambao ni watoto na wazazi wao wamekuwa wakigoma kuja mahakamani na kukwamisha ushaidi hivyo kushindwa kufanikiwa.
“…Binafsi naamini kama wangepatikana watu wa kutolewa mfano kila wanapofanya makosa haya ya kuwabebesha mimba wanafunzi watu wangeogopa kufanya vitendo hivi,” anasema mtendaji huyu mkuu wa wilaya ya Newala.
Anasema pamoja na hali hiyo sababu nyingine inayochangia kukithiri kwa mimba za utotoni ni pamoja na kufunjika kwa ndoa holela eneo hilo. Anasema ndoa zimekuwa zikifunjika hasa msimu wa mavuno ya korosho na watoto kubaki ama kwa bibi au kwa mama ambaye mara baada ya ndoa yake kuvunjika anaweza kuolewa tena na kuwaacha watoto wa awali bila uangalizi wa kutosha.
“…Unakuta watoto wanabaki kwa bibi ambapo wanakosa mahitaji ya msingi kutokana na uwezo mdogo wa bibi, mtoto analazimika kutafuta mwenyewe jambo ambalo linachangia kujikuta anapata mimba za umri mdogo kiurahisi kutokana na mazingira anayoishi huku akiwa hana uangalizi wa kutosha,” anabainisha Kaimu Mkurugenzi,” Bi. Kambuga.
Anasema ili kukabiliana na hali hiyo Serikali wilayani Newala imekuwa ikipambana kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na idara anuai eneo hilo.
“…Suala la elimu kwetu imekuwa ni ajenda ya kudumu katika gazi zote, kuanzia ngazi ya halmashauri za vijiji, kamati za maendeleo za kata na katika ngazi nyingine ni lazima tuwe na ajenda ya kuzungumzia suala hili. Wakati huo huo pia bado tunayo mabaraza ya kata ambayo tatizo kama hilo linapo tokea wajumbe hulishughulikia…na anapobainika mtia mimba huanza kufikishwa kwenye mabaraza haya,” anasema.
Hata hivyo takwimu kutoka Dawati la Jinsia na Watoto la Wilaya la Jeshi la Polisi linaonesha kuwa kuanzia Januari hadi Machi 2014 kuna jumla ya kesi nne (4) za wanafunzi kutiwa mimba na kukatishwa masomo na makosa mawili (2) ya watu walioshtakiwa kwa kuwaweka kinyumba wanafunzi. Ikiwa ni tafsiri ya kumzorotesha mwanafunzi masomo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TAMWA

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mwanafunzi Miaka 13 Msingi Abebeshwa Mimba, Afaulu Sekondari…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mwanafunzi-miaka-13-msingi-abebeshwa-mimba-afaulu-sekondari/feed/ 0
Watoto Nkasi Waajiriwa kwa Ujira wa Ndama kwa Mwaka http://www.thehabari.com/watoto-nkasi-waajiriwa-kwa-ujira-wa-ndama-kwa-mwaka/ http://www.thehabari.com/watoto-nkasi-waajiriwa-kwa-ujira-wa-ndama-kwa-mwaka/#comments Tue, 27 May 2014 08:31:29 +0000 http://www.thehabari.com/?p=47206 Na Joachim Mushi, Nkasi BAADHI ya watoto Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa ...

The post Watoto Nkasi Waajiriwa kwa Ujira wa Ndama kwa Mwaka appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mmoja wa watoto akirudisha nyumbani ng'ombe wanaotumiwa kwa kilimo Wilayani Nkasi.

Mmoja wa watoto akirudisha nyumbani ng’ombe wanaotumiwa kwa kilimo Wilayani Nkasi.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye.-1

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye.-1

Mifugo Wilayani Nkasi.

Mifugo Wilayani Nkasi.

Na Joachim Mushi, Nkasi

BAADHI ya watoto Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa hasa maeneo ya vijijini wamekuwa wakiajiriwa na familia za kifugaji kwa ujira wa ndama mmoja kwa mwaka mmoja.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi watoto hao wengi wao ni wa kabila la Wafipa na wamekuwa wakitumikishwa kazi ya kuchunga ng’ombe za wafugaji wa kabila la Kisukuma. Kibaya zaidi baadhi yao huamua kuacha kabisa masomo ya msingi na wengine masomo ya sekondari na kwenda kufanya kazi hiyo, ambayo mkataba wake huwa ni malipo ya ndama hufanywa kati ya familia ya mtoto na mfugaji.

Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa mbali na ukatili huo kwa watoto kutumikishwa, baadhi yao wamekuwa wakijikuta wakiangushiwa kipigo kikali kutoka kwa wamiliki wa mifugo hiyo hasa pale wanapopoteza mifungo wakiwa kazini. Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni maeneo hayo, ulibaini kuwa mtoto anayetumikishwa hutakiwa kuhamia katika familia ya mfugaji na kuanza kuchunga ng’ombe za mfugaji kila uchao na baada ya kukamilisha mwaka familia yake/wazazi wake hupewa ndama na mmiliki wa mifugo ikiwa ni kama ujira wa mtoto huyo.

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Lunyala nje kidogo ya Mji wa Namanyere wilayani Nkasi alisema baadhi ya wazazi wanalazimika kuwaingiza watoto wao katika ajira hizo kutokana na ugumu wa maisha, hata hivyo alidai wapo watoto ambao ukimbia shule na kwenda kufanya kazi hizo.

Akizungumzia matukio hayo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye alikiri uwepo wa ajira hizo kwa baadhi ya vijiji jambo ambalo alisema wanapambana nalo na kuitaka jamii maeneo hayo ibadilike na kuacha ukatili huo.
“…Ni kweli hali hii ipo, zipo familia na wafugaji ambao wamekuwa na tabia hii ya kikatili ya kuajiri watoto wadogo na kuwatumikisha katika shughuli za kuchunga mifugo ya wafugaji hasa maeneo ya vijijini wilayani Nkasi, kibaya zaidi baadhi yao huacha masomo na kufanya kazi hizi,” alisema Mdenye.

Alisema Ofisi ya Ustawi wa jamii eneo hilo kwa kushirikiana na dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi Wilaya ya Nkasi limekuwa likijitahidi kuzunguka vijiji mbalimbali na kutoa elimu ili kuhakikisha vitendo hivyo vya kikatili kwa watoto vinakoma mara moja.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TAMWA.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Watoto Nkasi Waajiriwa kwa Ujira wa Ndama kwa Mwaka appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/watoto-nkasi-waajiriwa-kwa-ujira-wa-ndama-kwa-mwaka/feed/ 0
Maisha ya ‘Geto’ Changamoto kwa Wanafunzi Sekondari za Kata Tanga http://www.thehabari.com/maisha-ya-geto-changamoto-kwa-wanafunzi-sekondari-za-kata-tanga/ http://www.thehabari.com/maisha-ya-geto-changamoto-kwa-wanafunzi-sekondari-za-kata-tanga/#comments Tue, 25 Mar 2014 02:52:31 +0000 http://www.thehabari.com/?p=44287 UJENZI wa Sekondari za Kata katika mikoa mbalimbali umesogeza huduma za elimu ...

The post Maisha ya ‘Geto’ Changamoto kwa Wanafunzi Sekondari za Kata Tanga appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Moja ya kibanda ambacho hutumiwa na wanafunzi wa Sekondali za Kata kama makazi jirani na shule moja Wilaya ya Lushoto.

Moja ya kibanda ambacho hutumiwa na wanafunzi wa Sekondali za Kata kama makazi jirani na shule moja Wilaya ya Lushoto.

UJENZI wa Sekondari za Kata katika mikoa mbalimbali umesogeza huduma za elimu kwa baadhi ya maeneo. Ipo mikoa ambayo awali ilikuwa na shule chache za sekondari hali ambayo ilifanya wanafunzi wachache kupata fursa ya kujiunga na sekondari. Kwa sasa hali si hivyo tena, mikoa mingi imeongeza idadi ya shule hizo licha ya changamoto kibao inazozikabili shule hizi.

Zipo baadhi ya shule za sekondari zimejengwa mbali kidogo na makazi ya wahitaji kitendo ambacho huwalazimu wanafunzi kutembea muda mrefu asubuhi wakielekea shuleni na baadaye jioni wakirejea nyumbani, hali ambayo ni changamoto kwa wengi wao.

Hata hivyo baadhi ya maeneo shule hizo zimejengwa mbali zaidi na makazi ya watu kutokana na kile kuhudumia vijiji ama vitatu hadi vinne, na hazina mabweni jambo ambalo wanafunzi wanashindwa kuvumilia umbali uliopo kutoka kijiji kimoja hadi kingine hivyo kutafuta mbinu mbadala ya kusogea jirani na shule wanazokuwa wamepangiwa.

Wanafunzi wanaamua kutafuta vyumba vilivyopo jirani na maeneo ya shule walizopangiwa na hivyo kupanga (kukodi chumba). Wenyewe vyumba hivi huviita mageto. Vyumba hivi huwa vidogo na vingine mithili ya vibanda, ambapo bei huwa ya chini zaidi kwa mwezi. Wanafunzi wengine huamua kujikusanya wawili ama zaidi na kuishi pamoja kwenye geto ili kupunguza gharama.

Vyumba hivi ni baadhi ya mageto ya wanafunzi wilayani Lushoto, Tanga.

Vyumba hivi ni baadhi ya mageto ya wanafunzi wilayani Lushoto, Tanga.

Mkoa wa Tanga katika Wilaya ya Lushoto baadhi ya maeneo aina hii ya maisha ya wanafunzi ni kitu cha kawaida. Wanafunzi wameamua kupanga kwenye mageto (vyumba mitaani) na kuishi kwa makundi huku wakikabiliwa na changamoto lukuki zinazohatarisha safari yao ya elimu ya sekondari.

Mbwambo Conrad ni Mkazi wa Kata ya Bungu wilayani Lushoto, eneo ambalo lina idadi kubwa ya wanafunzi waliopanga kutoka vijiji vya mbali huku wakihudhuria masomo yao ya sekondari. Anasema eneo hilo kuna wanafunzi wengi ambao wametoka vijiji vya mbali na wamepanga jirsni na shule kwenye kata hiyo kuhudhuria masomo.

Anasema wanafunzi hao wamepangiwa na wazazi wao ili waweze kuhudhuria masomo yao kuepuka umbali wanaotoka kwenye vijiji vyao. “Wanafunzi hawa wamepanga katika baadi ya vyumba na wanaishi kwa tabu sana…wengi wanaingia katika majaribu kutokana na aina ya maisha wanayoishi,” anasema Mzee Conrad.

Anasema wavulana wengi huishia kuwa wahuni maana uangalizi wa wazazi hawana, mara nyingi utawakuta wamekaa vikundi kwa vikundi nyakati za jioni hadi usiku unaweza kufikiri sio wanafunzi. Wanachelewa kulala muda mwingi wanazunguka kwenye majumba ya sinema (vibanda vinavyo onesha picha za video) hivyo wanaishi kwa kujitawala utazani si wanafunzi.

Willson N’gwamizi ni Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Muungui wilayani Lushoto, anasema licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali katika shule hiyo suala la wanafunzi kuishi kwenye mageto ni changamoto kubwa kwa shule kwani linaathiri maendeleo ya shule kitaaluma. Anasema wanafunzi hulazimika kuishi katika vyumba hivyo vya kupanga kutokana na shule nyingi za kata zilizojengwa kutokuwa na mabweni huku zikichukua wanafunzi kutoka vijiji vya mbali.

“…Kifupi suala la wanafunzi kuishi katika mageto linaathiri maendeleo ya shule kitaaluma…wanafunzi hawa wanapoishi huko hukosa usimamizi wa wazazi na wengine hata hela ya kumudu maisha hayo huwa ni tatizo maana wanatoka vijiji vya mbali na uwezo wa familia zao wakati mwingine hushindwa kuwatimizia mahitaji yote,” anasema N’gwamizi.

Anasema kutokana na uhuru huo wa kukaa kwenye mageto wanafunzi wengine hutoroka na kwenda kufanya vibarua kwenye mashamba ya chai na sehemu nyingine wasichana nao huwa huru zaidi kitendo ambacho hushindwa kukabiliana na changamoto za vishawishi mitaani.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Komnyang'anyo wilaya ya Handeni  wakitembea barabarani kuelekea kwenye makazi yao vijiji mbalimbali vinavyoizunguka shule hiyo, baadhi ya wanafunzi hawa hulazimika kutembea kati ya kilometa 10 au zaidi toka makazi yao kutokana na umbali wa shule.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Komnyang’anyo wilaya ya Handeni wakitembea barabarani kuelekea kwenye makazi yao vijiji mbalimbali vinavyoizunguka shule hiyo, baadhi ya wanafunzi hawa hulazimika kutembea kati ya kilometa 10 au zaidi toka makazi yao kutokana na umbali wa shule.

“Ukizunguka katika baadhi ya kata unaweza kukuta wanafunzi wa kidato cha pili wamepanga kwenye chumba kimoja, ndani ya chumba hicho wapo wawili hadi watatu…wengine wanatoka katika familia duni hawapewi mahitaji ya kutosha, wengine hujikuta wanashawishika na kuingia mitaani na kujikuta wanakatizwa masomo kwa kutiwa ujauzito,” anasema.

“Kwa kweli mageto ni tatizo, wapo baadhi ya walimu hujitahidi kuwafuatilia huko wanakoishi ili kuhakikisha wanajenga nidhamu ya kiuanafunzi, hata hivyo zoezi hili bado ni changamoto maana na walimu wamejikuta wakikaa mbali na shule kutokana na ukosefu wa nyumba za walimu jambo ambalo ni tatizo pia…,” anasema mwalimu huyo.

Suala la ukosefu wa mabweni kwa shule za kata na kuwalazimu wanafunzi kupanga mitaani (mageto) halipo kwa wilaya ya Lushoto pekee. Wilaya ya Handeni nayo inakabiliwa na changamoto hiyo ya wanafunzi kupanga uswahilini wenyewe karibu na shule walizopangiwa.

Ester Frank ni mmoja wa wanafunzi wa sekondari za kata wilayani Handeni anasema changamoto kwa wanafunzi kukaa kwenye mageto ni kubwa hasa wa kike. Anasema wengi wanakosa uangalizi na usimamizi hivyo kujikuta wanajiingiza kwenye vishawishi hivyo kuishia kupata mimba na kukatizwa masomo yao. “…Usema kweli mageto yanatuathiri wanafunzi hapa wilayani Lushoto,” anasema mwanafunzi huyo.

Afidha Said ni mkazi wa Kijiji cha Kidereko, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. Said anasema katika mahojiano na mwandishi wa makala haya kijijini Kidereko wilayani Handeni, aliyekuwa akifuatilia vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo hufanyiwa baadhi ya wanafunzi na wanawake eneo hilo kwa ushirikiano na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa). Anasema matukio ya mimba kwa wanafunzi eneo hilo si kwamba hulazimishwa kimahusiano, bali huingia wenyewe katika mahusiano kingono kutokana na mazingira halisi.

Anasema ukiachilia mbali uduni wa kipato kwa familia nyingi eneo hilo, ambao wengi ndio wazazi/walezi wa wanafunzi, shule nyingi za kata Wilaya ya Handeni zipo mbali na makazi ya wanafunzi. Zimejengwa hivyo ili kuweza kuhudumia vijiji vingi, ambavyo pia kuna umbali mkubwa kutoka kijiji kimoja hadi kingine.

Wapo wanafunzi ambao hulazimika kutembea kilometa 12 hadi 20 kwenda na kurudi shuleni kila siku jambo ambalo linawaumiza wengi, hivyo kulazimika ama kutafuta urahisi wa kupata usafiri hasa kwa wanafunzi wanaotoka vijiji vya mbali au kulazimika kupanga katika mageto jirani na shule walizopangiwa. kwa usafiri maarufu ambao hutumika na jamii maeneo mengi ya vijiji hivi ni pikipiki (bodaboda), ambao wazazi hawawezi kuumudu kwa wanafunzi wao kutokana na gharama za juu.

Mmoja wa walimu katika moja ya shule za kata wilaya ya Handeni (jina tunalihifadhi kwa kuwa si msemaji) anasema shule yao inawanafunzi wanatoka katika vijiji kama Kidereko ambacho ni takribani kilomita 6 kwenda na Kijiji cha Bangu ambacho ni karibu kilomita 10 kwenda tu. Anasema umbali kama huu ukiuunganisha mwanafunzi analazimika kwenda na kurudi kila siku unakuta ni tatizo.

Anasema na wengi wanatoka katika familia duni unakuta hawapewi chochote wanapotoka nyumbani kama matumizi ya siku (kula), sasa katika hali kama hii inakuwa tabu. Wapo ambao wanaamua kukata tamaa ya kuendelea na shule hivyo kujiingiza katika mambo ambayo yanawaharibu kitabia kabisa.

Rais Jakaya Kikwete akihutubia wananchi Januari 7, 2013 mjini Igunga aliwahi kusema kuwa serikali inajitahidi kukabiliana na changamoto za elimu. “Kwa upande wa elimu tumeendelea kupata mafanikio katika kupunguza tatizo la upungufu wa walimu wa shule za msingi na sekondari. Mwaka huu (2013) tuliajiri walimu 28,666. Kwa ajili hiyo upungufu wa walimu ni 57,755 kati yao 20,625 wa shule za msingi na 37,130 wa shule za Sekondari.

Rais Kikwete anasema kwa mwaka 2014 Serikali itaajiri walimu wapya 36,100 kati yao 18,100 wa shule za msingi na 18,000 wa sekondari. Kufanya hivyo kutafanya pengo lililopo liwe dogo zaidi. Kwa upande wa shule za sekondari, tatizo la walimu wa masomo ya sanaa tunakaribia kulimaliza. Changamoto yetu kubwa itakuwa kwa walimu wa masomo ya sayansi.

Rais Kikwete anasema upungufu ni walimu 26,998 na uwezo wa vyuo vya ualimu nchini ni kutoa walimu wa sayansi 2,300 kwa mwaka. Anaongeza kuwa mapema mwaka 2014 Serikali itakutana na wadau wa elimu nchini kujadiliana juu ya mkakati wa haraka wa kulikabili tatizo hilo.

Hata hivyo licha ya juhudi hizi kwa upande wa changamoto ya walimu hasa kwa shule za kata kuna haja ya Serikali kuangali namna ya kulipa kipaumbele suala la kupambana na changamoto za umbali wa shule za kata na makazi ya wananchi na kuhakikisha ujenzi wa mabweni ili kupunguza adha wanazopata wanafunzi wa kike na kiume kutokana na changamoto hiyo inamalizima kama si kupungua kwa kiasi fulani. Tukiamua tunaweza kukabiliana na changamoto hizi.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TAMWA

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Maisha ya ‘Geto’ Changamoto kwa Wanafunzi Sekondari za Kata Tanga appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/maisha-ya-geto-changamoto-kwa-wanafunzi-sekondari-za-kata-tanga/feed/ 0
Mapya Yaibuka Ndoa Iliyovunjwa na Mahakama Nkasi, Yadaiwa Mume ‘Alimbaka’ Mwanafunzi…! http://www.thehabari.com/mapya-yaibuka-ndoa-iliyovunjwa-na-mahakama-nkasi-yadaiwa-mume-alimbaka-mwanafunzi-2/ http://www.thehabari.com/mapya-yaibuka-ndoa-iliyovunjwa-na-mahakama-nkasi-yadaiwa-mume-alimbaka-mwanafunzi-2/#comments Tue, 14 Jan 2014 21:41:27 +0000 http://www.thehabari.com/?p=42020 Na Joachim Mushi, Nkasi-Rukwa SAKATA la ndoa iliyovunjwa na mahakama ya Mwanzo ...

The post Mapya Yaibuka Ndoa Iliyovunjwa na Mahakama Nkasi, Yadaiwa Mume ‘Alimbaka’ Mwanafunzi…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Ndebile Kazuri anayedaiwa kumpa mimba mwanafunzi darasa la saba

Ndebile Kazuri anayedaiwa kumpa mimba mwanafunzi darasa la saba

Na Joachim Mushi, Nkasi-Rukwa

SAKATA la ndoa iliyovunjwa na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa limeingia katika sura mpya baada ya uchunguzi zaidi kubainika kuwa mume aliyeiomba mahakama ivunje ndoa yake, Ndebile Kazuri alimkatisha mke masomo ya elimu ya msingi mkewe baada ya kumtia ujauzito akiwa darasa la sita.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ambazo mwandishi wa habari hii amevipata vinaeleza kuwa Kazuri ambaye hivi karibuni ameiomba mahakama hiyo kuvunja ndoa yake na Bi. Maria Tarafa kwa madai mke wake anakiburi na mdokozi wa vitu ndani ya nyumba yao, alimkatisha masomo na baadaye kumuoa mwaka 2004.

Taarifa zinaeleza kuwa Kazuri alimkatisha masomo Bi. Tarafa, mwezi Machi akiwa Shule ya Msingi Isale iliyopo Wilayani Nkasi huku akiwa na umri wa miaka 15 na alijifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 16.

Taarifa zinasema baada ya kutiwa ujauzito Bi. Tarafa wazazi wa mumewe walizungumza kifamilia na kukubaliana wasimshtaki kwa kuwa atafungwa na mama na mtoto kukosa huduma za baba. Baada ya hapo walikubaliana amuoe hivyo mume huyo alilipa mahari na kumuoa binti huyo wa darasa la sita akiwa na umri wa miaka 16.

Akizungumza na Thehabari.com, kuzungumzia madai hayo Bi. Tarafa amekiri kuwa ni kweli kwamba alikatishwa masomo na Kazuri mwaka 2003 akiwa darasa la saba, lakini kwa kuwa baba yake mzazi na baba mzazi wa Kazuri walikuwa marafiki sana waliyamaliza wenyewe na kukubaliana watoto wao waoane. Alisema aliunganishwa na mumewe Kazuri mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 16 baada ya mumewe huyo kulipa mahari (ng’ombe) kwa familia ya mzee Tarafa.

“…Inaniuma sana kwa kitendo ambacho ananifanyia kwa sasa kwani alinikatisha masomo, kanipotezea muda wangu na kaniongezea mzigo wa watoto wane na anataka niende kuishi nao peke yangu baada ya kwenda kuongopa mahakamani,” alisema Bi. Tarafa.
Alisema sababu alizozitoa mahakamani si za kweli kwani amekuwa akimpiga na kumnyanyasa ndani ya ndoa yake na kumtaka aondoke kwake na kwenda kuishi kwao. Alisema kuna kipindi mtalaka wake huyo aliwahi kumfukuza akiwa na watoto wawili na kurudi nyumbani kwao lakini baadaye alikuja kuomba radhi na kutaka apewe mke wake aende kuishi naye.

Kazuri alifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo, Namanyere Wilaya ya Nkasi Oktoba 28, 2013, kesi namba 26/2013 iliyosikilizwa na Hakimu aliyetajwa kwa jina la B. Stanley; na Novemba 18, 2013 hakimu huyo baada ya kuisikiliza kesi aliamuru ndoa ivunjwe. Mahakama ilivunja ndoa hiyo na kuamuru Bi. Tarafa aondoke na watoto wawili kati ya wanne waliozaa na mumewe kipindi wakiishi kama mke na mume bila kueleza namna watoto hao watakavyo pata huduma toka kwa baba yao.

Katika hukumu yake mahakama iliamuru watoto wa miaka 7 na 9 watabaki kwa baba yao na wenye miaka chini ya saba kubaki na mama yao. Mahakama hiyo ya mwanzo pia iliamuru mke apewe magunia 9 ya mahindi kati ya 10 ambayo walizalisha wote na bati 7 zilizokuwa nyumbani kwao.

Hata hivyo alipotafutwa Kazuri kuzungumzia madai hayo kwa njia ya simu hakuweza kupatikana kwani taarifa ambazo zimetufikia ni kwamba, kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Nkasi kwa kitendo cha kuvunja nyumba ya mtalaka wake na kumtishia kumdhuru huku akimtaka aondoke kwake.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mapya Yaibuka Ndoa Iliyovunjwa na Mahakama Nkasi, Yadaiwa Mume ‘Alimbaka’ Mwanafunzi…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mapya-yaibuka-ndoa-iliyovunjwa-na-mahakama-nkasi-yadaiwa-mume-alimbaka-mwanafunzi-2/feed/ 0
Mahakama Nkasi Yalalamikiwa Kuvunja Ndoa Yenye Mgogoro Bila Kugawanya mali http://www.thehabari.com/mahakama-nkasi-yalalamikiwa-kuvunja-ndoa-yenye-mgogoro-bila-kugawanya-mali/ http://www.thehabari.com/mahakama-nkasi-yalalamikiwa-kuvunja-ndoa-yenye-mgogoro-bila-kugawanya-mali/#comments Wed, 08 Jan 2014 07:41:12 +0000 http://www.thehabari.com/?p=41899 Na Joachim Mushi, Nkasi MAHAKAMA ya Mwanzo Namanyere wilayani Nkasi imelalamikiwa kwa ...

The post Mahakama Nkasi Yalalamikiwa Kuvunja Ndoa Yenye Mgogoro Bila Kugawanya mali appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Maria Tarafa (wa kwanza kushoto) akiwa na watoto wake wanne aliozaa na Ndebile Kazuri akiwa amekaa kwenye kifusi cha sehemu ya nyumba anayokaa, mumewe ameibomoa nyumba hiyo ili kumfukuza eneo hilo.

Maria Tarafa (wa kwanza kushoto) akiwa na watoto wake wanne aliozaa na Ndebile Kazuri akiwa amekaa kwenye kifusi cha sehemu ya nyumba anayokaa, mumewe ameibomoa nyumba hiyo ili kumfukuza eneo hilo.


Na Joachim Mushi, Nkasi
MAHAKAMA ya Mwanzo Namanyere wilayani Nkasi imelalamikiwa kwa kitendo cha kuvunja ndoa iliyokuwa na mgogoro kwa wanandoa bila kugawanya mali iliyochumwa kipindi cha wanandoa wakiishi kama mke na mume. Bi. Maria Tarafa (25) mkazi wa Kijiji cha Isale ambaye ni mmoja wa wanandoa hao ametoa malalamiko hayo hivi mjini hapa alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, huku akiituhumu mahakama hiyo haijampa nafasi ya kujitetea kama akiwa kama mlalamikiwa.

Alisema mumewe, Ndebile Kazuri (31) alikuwa akitaka kumtelekeza yeye na watoto wao wanne kwa muda mrefu kwa kutaka kuivunja ndoa yao halali kinyemela, lakini alikuwa akimshinda kila alipoitisha vikao vya wazazi na viongozi wa vijiji na kata akitaka kuivunja ndoa hiyo bila kutoa haki kwa mama na watoto (huduma).

Alisema mume huyo wameishi naye kama mtu na mke wake tangu mwaka 2003 na kufanikiwa kupata watoto wanne ambao walikuwa wakiishi eneo moja na baba yao huku Kazuri naye akiishi na mwanamke mwingine eneo hilo ambaye pia wamezaa naye.
“…Licha ya kuishi naye amekuwa akinipiga na kunifukuza niondoke kwake na watoto wangu nirudi kwetu, lakini mimi nimekataa mara zote na kumwambia nitakuwa tayari kuondoka baada ya kupata haki zangu na watoto kuhakikisha wako katika malezi mazuri,” alisema Bi. Tarafa.

Alisema mumewe aliamua kwenda baraza la kata na kuomba barua ili aende mahakamani kuiomba mahakama ivunje ndoa yake na mkewe aondoke na kurudi kwa wazazi wake. Kazuri alifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo, Namanyere Wilaya ya Nkasi Oktoba 28, 2013, kesi namba 26/2013 iliyosikilizwa na Hakimu aliyetajwa kwa jina la B. Stanley.

Alisema mahakama ilimwita kwa mara ya kwanza na kumsomea maelezo ya mdai (mumewe) ya kuomba ndoa yao ivunjwe yeye alipinga na kutaka awasilishe maelezo yake lakini mahakama iligoma kwa madai ilichoitaji kwa mlalamikiwa ni kujibu kama yupo tayari au la na si kupata maelezo. “…Niliomba niliomba nipewe nafasi ya kuzungumza upande wangu lakini walikataa na kuniambia; mama tumekuja kusikiliza kesi ya talaka na si maelezo mengine, we sema kama upo tayari au la…,” alisema.

Aliongeza kuwa Novemba 18, 2013 baada ya yeye kukiri kuwa yupo tayari kuachana na mume huyo iwapo atapata haki zake na watoto, mahakama ilivunja ndoa hiyo na kuamuru aondoke na watoto wawili bila kueleza namna watakavyo pata huduma toka kwa baba yao.
Alisema mahakama iliamuru watoto wa miaka 7 na 9 watabaki kwa baba yao nay eye kuondoka na wawili wenye miaka miaka chini ya saba. Aliongeza kuwa Mahakama iliamuru apewe magunia 9 ya mahindi kati ya 10 ambayo tulilima pamoja na bati 7.
“…Mume wangu alidanganya kuwa hatuna mali pale mahakamani, mimi nikaeleza ni uongo kwani tuna ng’ombe zaidi ya 127, buzi 30, nyumba mbili pale kijijini Isale pamoja na hekari zaidi ya 70 za ardhi…hawakunisikiliza pale mahakamani. Ukweli ni kwamba tunamali hizo ambazo tulichuma tukiwa wote,” alisema Bi. Tarafa.

Mwandishi wa habari hii amebahatika kupata nakala ya hukumu ya kesi hiyo, ambayo kweli haikuonesha namna watoto wanaobaki kwa mama watahudumiwaje licha ya kuamuru kuwa watabaki na mamayao. Akizungumzia sakata hilo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya, Ramadhan Rugemalira alisema mama huyo anahaki ya kufungua kesi ya madai kuomba mgawanyo wa mali na matunzo kwa watoto endapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa kwa shauri hilo. “…Anachotakiwa kuomba mahakamani kwa sasa ni mgawanyo wa mali, kwamba katika kesi yao ambayo mahakama ilivunja kuna mali ambazo mahakama haikuzizungumzia kabisaa lakini na mimi (mke) ninahaki na mali hizo, unaona…ataleta ushahidi kama ng’ombe hao wapo kama kuna ardí na nini…hivyo huyo mwanaume ataitwa na kesi kusikilizwa,” alisema Rugemalira.

Hata hivyo, Hakimu Rugemalira alisema huenda mtoa hukumu wa mwanzo aliteleza kwa kitendo cha kutoainisha namna watoto wanaobaki kwa mama watalelewa vipi. Alisema pamoja na hayo bado mama huyo anahaki ya kufungua madai mengine kudai haki hizo. Tulipo zungumza na Kazuri juu la mali ambazo mke anazilalamikia, yaani ng’ombe 127, nyumba 2, mbuzi 30 na ardhi hekari 70 alisema mali hizo alipewa na babayake wakati anaanza maisha hivyo bado ni mali ya babayake ambaye alidai yupo hadi sasa. Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini baba yake na Kazuri (yaani Kazuri Moshi) ni marehemu alifariki tangu Machi 2004 na mali zake kugawiwa kwa watoto wake.

Hata hivyo mtalaka wake Kazuri anasema walipewa ng’ombe za urithi toka kwa baba yake na Kazuri zikiwa 65 lakini wamezizalisha hadi kufikia idadi zilipo sasa pamoja na mashamba na nyumba lakini anashangaa mzazi mwenzake anamdhulumu kila kitu.
-Imeandaliwa na Thehabari.com kwa kushirikiana na TAMWA

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mahakama Nkasi Yalalamikiwa Kuvunja Ndoa Yenye Mgogoro Bila Kugawanya mali appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mahakama-nkasi-yalalamikiwa-kuvunja-ndoa-yenye-mgogoro-bila-kugawanya-mali/feed/ 0
Mume Amuua Mkewe kwa Kipigo Tanga http://www.thehabari.com/mume-amuua-mkewe-kwa-kipigo-tanga/ http://www.thehabari.com/mume-amuua-mkewe-kwa-kipigo-tanga/#comments Wed, 09 Oct 2013 20:14:35 +0000 http://www.thehabari.com/?p=38692   Hili ndilo kaburi la marehemu, Bi. Rahima.   Kitambulisho cha Bi. Rahima.   ...

The post Mume Amuua Mkewe kwa Kipigo Tanga appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
rahima2

 

Hili ndilo kaburi la marehemu, Bi. Rahima.

rahima

 

Kitambulisho cha Bi. Rahima.

untitled

 

Super Woman Joyce Kiria (kulia katika mahojiano na shuhuda)

KESI za unyanyasaji dhidi ya wanawake zinazidi kuwa nyingi. Wanawake wameendela kuumizwa na ubabe wa waume zao. Hivi karibuni, katika kijiji cha Kizanda wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Bi. Rahima alifariki dunia baada ya kupigwa na mumewe mateke ya tumboni angali mja mzito.

Taarifa za awali kutolewa zinasema kuwa mwanamke huyo alifariki kutokana na homa, lakini ndugu wa marehemu wamedai kuwa kifo cha ndugu yao kimetokana na kipigo. Bi Rahima ambaye alikuwa ni mja mzito, alifariki mwezi wa saba mwaka huu.

Taarifa za awali ambazo zilifikia Wanawake Live na Super Woman Joyce Kiria kufuatilia zilionekana kupita EATV usiku wa jana, na pia unaweza kufuatilia kwenye YouTube kupitia linki hii hapa chini ili ufahamu kile wanasheria wamekizungumza katika kutafuta haki kufuatia suala hili ambalo hata viongozi w a kijiji hicho wameshindwa kulitatua.

Kuangalia Zaidi ingia hapa; Link: https://www.youtube.com/watch?v=3Pxs98h5jw0&feature=c4-overview&list=UUO-pOZN6prC9mweX949IRmA

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mume Amuua Mkewe kwa Kipigo Tanga appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mume-amuua-mkewe-kwa-kipigo-tanga/feed/ 0
Haya Ndio Madudu ya Baadhi ya Wanafunzi Waliofaulu Kidato cha Kwanza 2012 Rombo http://www.thehabari.com/haya-ndio-madudu-ya-wanafunzi-waliofaulu-kidato-cha-kwanza-2012-rombo/ http://www.thehabari.com/haya-ndio-madudu-ya-wanafunzi-waliofaulu-kidato-cha-kwanza-2012-rombo/#comments Mon, 07 Oct 2013 06:12:03 +0000 http://www.thehabari.com/?p=38562 Mtihani wa majaribio ambao mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza 2012 alijaribiwa wilaya ...

The post Haya Ndio Madudu ya Baadhi ya Wanafunzi Waliofaulu Kidato cha Kwanza 2012 Rombo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mtihani wa majaribio ambao mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza alijaribiwa kujua uwezo wake baada ya kufaulu, lakini cha ajabu wapo  ambao walishindwa hata kuandika majina yao, Wilaya zao na hata mkoa wao. Angalia mitihani hii iliyofanywa Wilaya ya Rombo.

Mtihani wa majaribio ambao mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza alijaribiwa kujua uwezo wake baada ya kufaulu, lakini cha ajabu wapo ambao walishindwa hata kuandika majina yao, Wilaya zao na hata mkoa wao. Angalia mitihani hii iliyofanywa Wilaya ya Rombo.

Mtihani wa majaribio ambao mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza alijaribiwa9
Mtihani wa majaribio ambao mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza 2012 alijaribiwa wilaya ya Rombo.

Mtihani wa majaribio ambao mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza alijaribiwa10
Mtihani wa majaribio ambao mtoto aliyefaulu kidato cha kwanza alijaribiwa.

Safari Rombo 107

Wapo walioshindwa hata kuandika imla na hata kujazia maneno kwenye sentesi zilizo wazi. Hii ni changamoto kwelikweli..!

Safari Rombo 103

 

Mtihani wenyewe ulisomoka hivi…!

Safari Rombo 105Wapo walioshindwa hata kuandika jina la shule aliyokuwa akisoma, Wilaya, Mkoa na hata majina yao kiusahihi. Hata hivyo habari za kina ambazo mtandao huu ulizipata na kuzifanyia uchunguzi wanafunzi hawa bado wanaendelea na masomo ya Sekondari mikoa tofauti. Tafakari..Chukua Hatua..

 

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Haya Ndio Madudu ya Baadhi ya Wanafunzi Waliofaulu Kidato cha Kwanza 2012 Rombo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/haya-ndio-madudu-ya-wanafunzi-waliofaulu-kidato-cha-kwanza-2012-rombo/feed/ 0
Mzee Kingunge Asiturudishe Nyuma Kwenye Hoja ya Uraia Pacha! http://www.thehabari.com/mzee-kingunge-asiturudishe-nyuma-kwenye-hoja-ya-uraia-pacha/ http://www.thehabari.com/mzee-kingunge-asiturudishe-nyuma-kwenye-hoja-ya-uraia-pacha/#comments Sun, 01 Sep 2013 13:31:04 +0000 http://www.thehabari.com/?p=37117 Mzee Kingunge Ngombare Mwiru Babu yetu mzee Kingunge Ngombare Mwiru amenukuliwa kwenye ...

The post Mzee Kingunge Asiturudishe Nyuma Kwenye Hoja ya Uraia Pacha! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
20130901-153041.jpg

Mzee Kingunge Ngombare Mwiru

Babu yetu mzee Kingunge Ngombare Mwiru amenukuliwa kwenye vyombo vya habari Leo akipinga hoja ya Tanzania kuruhusu raia wake kuwa na Uraia Pacha (Dual Citizenship). Namshukuru mzee Kingunge kwa kujitokeza hadharani na kupinga, maana ni vizuri tukawajua wazi wale wanaopinga na wale wanaounga mkono hoja hii muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu. Vita vya kuviziana au vya chini kwa chini huwa vina madhara makubwa sana, ndio maana pia nampongeza waziri wa mambo ya nje, Mh. Bernard Membe kwa kujitokeza na kuitetea hoja hii mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba hivi karibuni. Kitu ambacho nahisi ndio kimemshinikiza mzee Kingunge nae kujitokeza na kueleza dukuduku lake. Nasema haya yote ni muhimu wakati tunajadili hoja hii.

Mzee Kingunge hakufafanua kwa kina anachopinga, ila kwa nukuu niliyoisoma kwenye gazeti la The Gurdian, Kingunge alisema,

“‘The matter of dual citizenship is really disappointing me considering that we were fighting to get nationality from the British and we were not freely given,” he said, expressing surprise at the ruling party’s decision of supporting dual citizenship in the constitution. “I strongly reject this proposal’ ” (The Gurdian, 2013).

Pia, The Gurdian lilimnukuu Kingunge akisema kuwa, “those who propose dual citizenship have their interest because they want that nationality for financial interest”

Cha kusikitisha zaidi, Kingunge alinukuliwa kupinga hoja kwamba uraia pacha utasaidia Watanzania waliopo ughaibuni kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi yao (Tanzania) kupitia uwekezaji kwa kusema kwamba “kuna nchi nyingi zisizoruhusu uraia pacha na bado raia wake wanasaidia nchi zao”(The Gurdian, 2013). Nafikiri mzee wetu Kingunge inabidi afanye uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na atambue dunia ilipo na inapoelekea kabla hajaendeleza jitihada za kuturudisha nyuma kwenye hoja ya uraia pacha. Nasema hivyo kwasababu ningependa Mzee Kingunge na Watanzania wenzangu tukumbuke masuala kadhaa yafuatayo.

Karibia kila mtu anashuhudia jinsi dunia sasa inavyokuwa kijiji komoja, ambapo kila nchi sasa inabidi iwe na mikakati maalum ya kukaribisha na kukabili mabadilko haya. ukuaji wa teknolojia kama ya intaneti na vifaa vyepesi vya mawasiliano (mobile devices), ukichanganya na urahisi wa uhamaji wa watu katika kila pembe za dunia hii, kunatimiza ndoto za watu wengi haraka zaidi kuliko ilivyodhaniwa.

Nchi yingi zikikabiliwa na mitihani hii ya maendeleo haya ya kidunia, zimeamua kujidhatiti kwa kutumia rasilimali zake za utamaduni na watu, ili kukabiliana kikamilifu na mabadiliko haya ya kidunia. Kukubali na kuhalalisha Uraia pacha ni moja ya njia, ambayo nchi nyingi zimeamua kutumia, ili kuhakikisha zinaendelea kunufaika na michango ya raia wake, ambao wapo sehemu mbalimbali duniani kutokana na sababu nyingi, zikiwemo fursa za elimu, ajira, na usalama. Raia hao wamelazimika kuendelea kuishi nje ya nchi zao, bila kupoteza mapenzi kwa nchi zao za asili na siku zote wameendelea kutambulika kama Watanzania, wakenya, waganda, wanaijeria, na kadhalika….kwanza, kabla ya kuitwa Wamarekani, Waingereza au Wajerumani.

Kwa mfano, kama walivyo “African American” (kutambua asili yao ya Uafrika) wapo pia “Tanzanian American”, Kenyan American, Nigerian American, na kadhalika. Waliitwa “African American” kwasababu ukisoma historia ya Marekani utagundua kwamba vizazi vilivyofuata baada ya watumwa halisia kufa, hawakujua haswa wametoka nchi gani Afrika. Ndio maana vizazi vya watumwa hawa leo hii wameanzisha kampeni maalum ya kujua kule watokako. kampeni hizi kwa marekani zinaongozwa na mwanahistoria mahiri, Dr. Henry Luis Gates kupitia vipindi vyake maalum vya runinga “PBS African American Lives” (finding your roots).

Wengi wa Waafrika hawa huwa wanatoa machozi pindi wanapofahamishwa kwamba huenda(sio hata asilimia 100) wakawa wanatokea nchi fulani na wengine uamua kufunga safari na kuitembelea nchi husika. Sasa ndugu zangu inasikitisha sana kumsikia mzee Kingunge akisema “The issue of dual citizenship will completely take out the patriotism as each country has its own policies toward patriotism ” (The Gurdian, 2013). Hili sio suala la kuchukulia kiurahisirahisi na kutumia hoja ya “uzalendo” (patriotism) kwamba ni kigezo cha kumzuia mtu asiwe a pasi mbili, Je kwa kuzingatia yale machungu yanayowakumba wamarekani weusi sasa, tunafikiri kwamba asili ya mtu, mapenzi na uzalendo vitatoweka kwa kuwa tu eti mtu anakaratasi ya nchi nyingine?

Baadhi ya nchi zimeshabadilisha sheria zao baada ya kazingatia kwa kina mabadiliko ya dunia, na baadhi zimeweka masharti maalum katika sheria zao za uraia pacha, ili kulinda maslahi ya nchi. kwa mfano, kuanzia mwaka 2004, raia wa South Afrika wanaweza wakawa na pasi ya nchi nyingine, ukizingatia kwamba wametimiza miaka 18 na wameomba suksa maalum kabla ya kuchukua pasi ya nchi nyingine. Na waustralia na wa New Zeland hawajali una pasi ngapi, almuradi umetimiza masharti ya kuwa raia wao kwa vigezo vya kuzaliwa(by birth) au vya kuomba(by naturalization). Kwahiyo, hii inaonyesha kwamba jibu hapa sio kukataa hoja moja kwa moja kwamba haifai kama anavyodai Mzee Kingunge, bali tuangalie mifano ya wenzetu waliokwisha fanya wamefanya vipi na wanaendelea kunufaika vipi.

Itakuwa ni kosa kubwa kama nitaendelea kuzitaja nchi hizi, bila kuitaja nchi ya Kenya, ambayo ni jirani yetu wa karibu na tunashahabiana na kushirikiana katika masuala mengi tu. Wakenya waliliangalia suala hili kwa kina wakati wa mchakato wa mabadiliko ya katiba yao hivi karibuni, na hatimaye kukubaliana kwamba linafaa kwa maendeleo ya nchi yao, na hivyo kuliweka kwenye katiba.

Wakati Wakenya wanapambana kuhusu suala la uraia pacha, walizingatia faida kadhaa (zipo nyingi), ambazo Kenya ingezipata. Faida hizi ndio faida, ambazo Tanzania pia itazipata endapo tutakuwa makini katika suala hili. Ningependa kuzitaja baadhi ya faida hizo kama ifuatavyo:

Kwanza, Watanzania ambao wana uraia wa nchi nyingine, kwasasa wanalazimika kuomba viza ya ugeni (visitor’s visa) kuingia Tanzania na pia kuomba ruksa ya kukaa na kufanya kazi Tanzania kama wanataka kufanya hivyo. Uraia pacha, utaboresha suala hili, na kurahisisha mizunguko baina ya Tanzania na nchi husika (nchi ya pasi ya pili ya Mtanzania) na kuongeza chachu ya uwekezaji wa Watanzania katika nchi yao ya asili. Kujibu hoja ya mzee wetu Kingunge katika suala hili la uwekezaji, ni kwamba kwasasa watanzania na waafrika wengine, ambao nchi zao haziruhusu uraia pacha, wanawekeza sana (ikiwemo kutuma pesa za misaada mbalimbali), lakini katika mazingira magumu kutokana na kwamba michango yao haitambuliki kisheria.

Pia, kwa ufafanuzi zaidi, tofauti ya muwekezaji mzalendo(Mtanzania mwenye pasi mbili) na muwekezaji mgeni, ni kwamba Wawekezaji wageni mara nyingi huwa na hofu sana ya kuwekeza kwenye nchi za “Dunia ya Tatu”, lakini Mtanzania asili hana hofu hiyo (labda nyakati za vita) kutokana na mahusiano yake ya kiudugu (kinship) na ufahamu wa utamaduni wa uendeshaji wa mambo nchini mwake, hivyo basi kuwa rahisi kwake kujitosa bila hofu kwenye fursa za kibiashara.

Pili, Watanzania asili, ambao wanaishi ughaibuni wataendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii nchini Tanzania kutokana na uzoefu wao wa kipekee wanaoupata kwa kuishi kwao kwenye nchi hizi zilizoendelea, hivyo basi ni muhimu kutengeneza mazingira mazuri kwa wao kuendelea kushiriki na kunufaisha nchi. Hapa nazungumzia pia wale wasomi wengi ambao wameloea ughaibuni kutokana na sababu ambazo nimezitaja hapo awali.

Hili sio suala geni, ndio maana tunaona hata hizi nchi kubwa kama Marekani, Ujerumani na Wingereza wanautaratibu maalum wa kukaribisha wageni, na baada ya muda kuwapa uraia, ili wachangie maendeleo zaidi kwa kutumia elimu zao na uzoefu waliokuwa nao kutoka kwenye nchi zao. “USA Diversity visa program” maaarufu kama “Green Card” ni maalum kwa kufanikisha hili na hata Wamarekani na nchi nyingine kubwa hawana ugomvi na suala la uraia pacha (wengi wakishatoa uraia, hawamlazimishi mtu kuukana uraia wa nchi yake ya asili), ili mradi mtu havunji sheria za nchi zao kwa kigezo cha uraia wake wa nchi nyingine.

Sasa kama nchi kubwa zinatumia fursa hii, iweje sisi leo kuwekeana masharti magumu, wakati bado tupo katika mapambano ya kuiendeleza nchi yetu? Tuna hitaji Kila kichwa kishiriki popote kilipo wakati wowote ule. Vinginevyo, wale maadui watatu aliotutajia Baba wa taifa miaka takribani 40 iliyopita, yaani, Ujinga, Maradhi, na Umasikini vitaendelea kututesa.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Naomba kuwasilisha,

Hashim Rungwe Jr.
www.thehabari.com
Info@thehabari.com
1/9/2013

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mzee Kingunge Asiturudishe Nyuma Kwenye Hoja ya Uraia Pacha! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mzee-kingunge-asiturudishe-nyuma-kwenye-hoja-ya-uraia-pacha/feed/ 0