Blogs Tanzania | News | Michuzi ya Habari leo » Habari za Uchunguzi

Thamani ya Fedha Kenya ‘Yawaachisha’ Shule Wanafunzi Rombo
Hizi ni baadhi ya njia zisizo rasmi kwenda nchini Kenya zilizopo eneo la Rongai, Rombo.

Na Joachim Mushi, Rombo

KUFANYA vizuri kwa thamani ya fedha ya Kenya (Kshs) tofauti na ile ya Tanzania (Tshs) kumechangia kwa namna moja kuiathiri Wilaya ya Rombo maeneo ya mpakani mwa Kenya na Tanzania kitaaluma kwa kile baadhi ya wanafunzi wa sekondari kuacha shule na kwenda kufanya vibarua vijiji vya jirani.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni mjini hapa kumebaini kuwepo na idadi kubwa ya wanafunzi wa sekondari wa shule za mpakani wanaotoroka shule, ama wengine kuacha shule kuendelea na shule baada ya kumaliza elimu ya msingi hata kama wamefaulu na kwenda kufanya vibarua mpakani kwa kuvutiwa na thamani ya fedha ya Kenya.

Uchunguzi uliofanywa katika sekondari za Ngaleku, Tanya, Holili, Nduweni na Urauri zote zilizopo maeneo ya mpakani mwa Kenya wilayani Rombo umebaini idadi kubwa ya wanafunzi huzikimbia shule kabisa na wengine kufanya utoro wa rejareja wawapo shuleni kwa malengo ya kufanya vibarua mpakani.

Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango akizungumza na mwandishi wa www.thehabari.com hivi karibuni wilayani Rombo.

Kwa shule ya Sekondari Urauri kati ya wanafunzi 238 waliopangiwa kujiunga na shule hiyo kwa mwaka huu ni wanafunzi 178 tu ndiyo walioripoti huku idadi kubwa ikidaiwa kukimbilia nchi jirani ya Kenya kufanya vibarua anuai zikiwemo kazi za ndani na mashambani kwa kuvutiwa na thamani ya fedha nchini humo.

Licha ya idadi hiyo kutojiunga na shule na kudaiwa kukimbilia Kenya, baadhi ya wanafunzi waliojiunga na shule nao huendelea na utoro wa rejareja hasa kipindi cha msimu wa kilimo, mavuno na palizi na kwenda kufanya vibarua hali ambayo huathiri maendeleo ya kitaaluma kwa shule na wanafunzi.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Holili, Benson Samizi alisema kati ya wanafunzi 140 waliofaulu na kupangiwa kujiunga na shule hiyo kwa mwaka huu ni wanafunzi 85 tu ndiyo walioripoti. Alifafanua kuwa 30 alipata taarifa waliamua kujiunga na shule nyingine huku idadi iliyobaki wakitokomea kusiko julika na shule inaendelea kuwatafuta.

Kwa upande wa Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango alibainisha kati ya wanafunzi 94 waliopangiwa kujiunga na shule hiyo kwa mwaka huu ni wanafunzi 79 tu ndiyo waliripoti shuleni. Aidha alisema utoro pia umeiathiri shule hiyo kitaaluma kwani matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana jumla ya wanafunzi 71 wamepata sifuri, hakukuwa na ufaulu wa daraja la kwanza wala la pili na wanafunzi wawili walipata daraja la tatu huku wanafunzi 18 wakipata daraja nne.

Mzazi mmoja aliyejitaja kwa jina la Protus Shirima alisema si wanafunzi pekee ambao huvutiwa na thamani kubwa ya fedha ya Kenya kwani hata wapo wazazi ambao hukimbilia kufanya vibarua Kenya vijiji vya mpakani kutokana na thamani ya fedha. Alisema kibaya zaidi wapo baadhi ya wazazi ambao huambatana na watoto wao katika vibarua hivyo ili kuongeza kipato cha familia.

“Mi nakushauri jaribu kuja msimu wa kilimo ukichanganya ukae eneo hili (Tarakea) utaona makundi makubwa ya wananchi wakivuka mpakani nyakati za asubuhi kuelekea Kenya kufanya vibarua na kurejea tena jioni…hali hii hufanyika vivyo hivyo wakati wa mavuno na palizi, fedha ya Kenya ipo juu na ndiyo inayotuvutia wengi,” alisema Shirima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rombo, Judethadeus Mboya akizungumzia hali hiyo alikiri kuwepo na wimbi la wananchi kujiushisha na shughuli za mpakani maeneo hayo, japokuwa alisema wameanza utaratibu wa kuwatoza faini baadhi ya wazazi wanaoshindwa kuwazibiti watoto wao kiutoro shuleni kwa kuwatumia viongozi wa vijiji.

Aidha aliongeza kuwa ni vigumu kuwadhibiti wanafunzi kufanya shughuli za mipakani kwa kuwa wanapokwenda maeneo hayo hawaendi na sare za shule, ukiachilia mbali kuwa wapo baadhi ya wanavijiji wa Tanzania pia huendesha shughuli za kilimo nchini Kenya katika vijiji vya jirani.

Shughuli za mpakani zaathiri elimu ya sekondari Rombo
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Holili, Benson Samizi akizungumza na mwandishi wa www.thehabari.com hivi karibuni wilayani Rombo.

Geti la mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Holili, Wilaya ya Rombo.

Na Joachim Mushi, Rombo

SHUGHULI za biashara zinazoendeshwa maeneo kadhaa ya mpakani mwa Tanzania na Kenya katika Wilaya ya Rombo zimeathiri maendeleo ya elimu hasa kwa shule za sekondari zilizopo pembezoni mwa maeneo hayo kwa kile wanafunzi kujiingiza katika biashara hizo.

Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni wilayani hapa na mwandishi wa habari hizi umebaini baadhi ya wanafunzi katika shule za sekondari kutumika katika biashara za mipakani jambo ambalo linachangia wilaya hiyo kufanya vibaya kielimu katika matokeo hasa ya kidato cha nne.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya walimu wakuu wa shule za Sekondari za Urauri, Holili, Tanya, Nduweni pamoja na baadhi ya wadau wa elimu maeneo hayo wamesema wapo baadhi ya wanafunzi  wanajiingiza katika shughuli hizo ambazo huathiri maendeleo ya taaluma.

Akizungumzia shule yake, Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Urauli, iliyopo Tarakea wilayani Rombo, Sim Silayo alisema shughuli za biashara zinazofanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo hilo zinaathiri taaluma kwani wapo wanafunzi ambao hujiingiza katika shughuli hizo na kusahau masomo kwa vipindi tofauti.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nduweni wakifanya mazungumzo na mwandishi wa www.thehabari.com (hayupo pichani) alippotembelea shule hiyo. Shule hii ni miongoni mwa sekondari zilizopo maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Kenya wilayani Rombo.

Alisema baadhi ya wanafunzi wanafanya biashara ndogo ndogo na wengine kufanya vibarua mpakani jambo ambalo limekuwa likichangia taaluma kushuka katika shule hiyo, hasa nyakati za kilimo na mavuno maeneo ya vijiji vya mpakani Kenya na Tanzania.

“Kuna kipindi mahudhurio yanakuwa mabaya kabisa hasa kipindi cha mavuno, kilimo na palizi…wanafunzi wanakimbilia kufanya shughuli hizo kwa kulipwa, pia si wanafunzi tu wanaofanya kazi hizi hata baadhi ya wazazi nao hujumuika kufanya vibarua upande wa pili (Kenya) kwa madai kule malipo ni mazuri zaidi ya nchini kwetu,” alisema Silayo.

Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha nne Shule ya Urauri mwaka jana, kati ya wanafunzi 92 waliofanya mtihani huo, ni wanafunzi sita tu ndiyo waliofanikiwa kufaulu huku wanafunzi 44 wakipata daraja la nne na wanafunzi 42 wakiambulia daraja sifuri.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Holili, Benson Samizi alisema pamoja na sababu nyingine shughuli za mpakani zimekuwa zikichangia shule hiyo kufanya vibaya kwa kile wazazi kushindwa kuwadhibiti wanafunzi wanaporudi nyumbani na kuwa huru kufanya shughuli nyingine zinazowaathiri kitaaluma.

Alisema matokeo ya kidato cha nne mwaka jana shule hiyo ilifanya vibaya kwani kati ya wanafunzi 94 waliofanya mtihani huo, hakukuwa na ufaulu wa daraja la kwanza, daraja la pili na la tatu lilikuwa na mwanafunzi mmoja mmoja huku 39 wakipata daraja la nne na wengine 50 kupata sifuri.

Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya alikiri shule nyingi kufanya vibaya hasa matokeo ya mwaka jana na kuongeza uongozi wake umeanza kuchukua hatua  kukabiliana na hali zote zinazoathiri maendeleo ya kitaaluma kwa shule zake.

Alisema kwa hatua ya kwanza halmashauri ilimgharamia mkaguzi wa shule ambaye alifanya ukaguzi katika shule mbalimbali zikiwemo zilizofanya vibaya na kutoa mapendekezo.

Aliongeza kuwa ili kukomesha utoro katika shule hizo viongozi wa serikali za vijiji waliagizwa kuwashughulikia wazazi wanaoshindwa kuwabana watoto wao katika kuhudhuria shuleni, ambapo baadhi walianza kutozwa faini mtoto anapokosa shule jambo ambalo alisema limeanza kuleta mabadiliko.

Wilaya ya Rombo Kutumia Nyuki Kupambana na Tembo Wavamizi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya akizungumza na mtandao wa www.thehabari.com hivi karibuni wilayani Rombo.

Pichani ni baadhi ya majengo ya Shule ya Msingi Rongai, wilayani Rombo. Shule hii ni miongoni mwa maeneo yanayoathiriwa na uvamizi wa tembo waharibifu ambao huathiri taaluma shuleni hapo.

Baadhi ya mashamba ya wananchi eneo la Rongai, wilayani Rombo ambayo mara kadhaa huvamiwa na tembo waharibifu.

Na Thehabari.com, Rombo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Rombo imeanza mipango ya kutumia ufugaji wa nyuki kukabiliana na tembo waharibifu ambao mara kadhaa huvamia baadhi ya makazi ya wananchi maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kufanya uharibifu wa mazao pamoja na kuua au kujeruhi wakazi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Judethadeus Mboya alisema tayari halmashauri hiyo imetengeneza mizinga ya nyuki ambayo imesambazwa maeneo kadhaa ili kukabiliana na tembo waharibifu eneo hilo.

“Unajua nimetembea mbuga mbili za Kenya ikiwemo Tsavo ambazo tumepakana nazo eneo hili sehemu ambayo tembo hutokea huko na kuvamia maeneo yetu, sehemu hizi wao wamedhibiti uvamizi wa tembo…wamefuga nyuki wengi sana na maeneo mengine wametumia hadi teknolojia kuwazuia tembo kuvamia makazi ya raia hivyo hawapati madhara kama yetu,” alisema Mboya akifanya mazungumzo na gazeti hili ofisini.

Alisema kwa sasa tayari wametengeneza mizinga 50 ya nyuki na kuifunga ukanda wa chini wa vijiji kama Chala, Ibukoni, Ngoyoni na maeneo mengine ambayo tembo huyatumia kama njia kipindi cha uvamizi na kwa sasa mizinga mingine 100 ya nyuki inaandaliwa kuenezwa maeneo mengine kukabiliana na tembo hao hatari.

Alisema viongozi wa halmashauri hiyo pia wametoa elimu kwa wanakijiji maeneo husika ya kuhamasisha uvugaji nyuki katika vikundi ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tembo hao waharibifu ambao idadi kubwa hutokea nchi jirani ya Kenya na kufanya uharibifu pamoja na kutishia maisha ya wanavijiji upande wa Tanzania.

Aidha kiongozi huyo alisema tembo hao mbali na kufanya uhalibifu mkubwa wa mazao ya wanavijijini kipindi cha uvamizi wakati mwingine wamekuwa wakiuwa raia jambo ambalo ni hatari zaidi kiusalama.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini uvamizi wa wanyama hao umekuwa kero kwa maeneo mbalimbali ya vijiji vya wilaya hiyo, kiasi ambacho unatishia shughuli za maendeleo ya wananchi kama kilimo pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla.

Akizungumzia hali ya uvamizi wa tembo na athari za elimu, Mwalimu wa Taaluma Shule ya Sekondari Tanya, Shuma Himidiel alisema miezi ambayo tembo huanza kufanya uvamizi huingilia ratiba za masomo na mara kadhaa kusimama kutokana na hofu ya wanafunzi na usalama wao hasa wanapotoka na kuja shuleni.

“Kimsingi wanyama hawa wanapoanza usumbufu kijiji kizima huwa na heka heka na wakati mwingine hata wanafunzi wanashindwa kuja shule kuhofia maisha yao…hata wazazi huwazuia watoto wao kutoka hadi hali ya hatari inaporejea kuwa ya kawaida.

Akifafanua zaidi mwalimu Himidiel alisema mara ya mwisho tembo kufanya uvamizi katika Kijiji cha Tanya waliua mtu mmoja walipokuwa wakidhibitiwa na askari wa wanyamapori eneo hilo.

Ushahidi Kesi za Kubaka/Mimba ni Changamoto Handeni
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana

Na Joachim Mushi, Handeni

“KESI nyingi za tuhuma za kubaka na mimba kwa wanafunzi zinazotufikia zinashindwa kufikia hukumu maana mashahidi wanashindwa kuthibitisha pasipo shaka…nyingi zinaharibika sababu hawataki kusema ukweli, hivi karibuni nililazimika kuwaweka ndani wawili (mashahidi) kwa kuwa wanadanganya. Unakuta maelezo aliyotoa polisi ni mengine na akifika huku anageuka,” anasema Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana alipofanya mahojiano na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

Hakimu Maligana anasema licha ya takwimu zao kuonesha kesi za mimba/kubaka wanafunzi kwa sasa zinapungua bado suala la kuharibika kwa ushaidi wa kesi za mimba ni changamoto. Anasema kesi nyingi za wanafunzi zimekuwa zikishindwa kufanikiwa hadi hatua ya hukumu kutokana na mtindo wa kuvuruga ushahidi.

Anasema awali kikwazo kikubwa kwa kesi kama hizo ilikuwa ni upande wa wazazi na walimu kutotoa ushirikiano wa kutosha kwenye mchakato wa kesi. Lakini walimu na wazazi wameacha usumbufu huo hivyo imebaki kwa wanafunzi pamoja na watuhumiwa ambao mara kadhaa wanakuwa wapenzi wao. Anaongeza kuwa licha ya matukio hayo kupungua changamoto bado zipo.

Takwimu za kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2012 zinaonesha mahakama hiyo ilipokea kesi 10 za tuhuma za mimba/kubaka kwa wanafunzi, huku kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2013 ni jumla ya kesi sita tu zimepokelewa katika mahakama hiyo. Anasema kesi sita za mwisho kupokelewa zipo katika hatua anuai.

Zuber Chembera ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni (OCD), akizungumza na mwandishi wa makala haya ofisini kwake, anakiri kupungua kwa matukio ya kesi za mimba/kubakwa kwa wanafunzi Wilaya ya Handeni kutokana na takwimu zao.

Anasema kwa mwaka 2012 hadi mwezi Novemba walikuwa na jumla ya matukio ya kesi kama hizo 66, lakini kwa mwaka huu (Machi, 2013) kuna jumla ya matukio ya kesi kama hizo 14 tu yalioripotiwa.

Anasema elimu inayotolewa na Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Handeni imesaidia. “Kesi zinazotufikia hapa huku zikiwa na ushaidi wa kutosha tunazipeleka mahakamani, zile zinazokuwa hazina ushaidi wa kutosha tunajaribu kuzifuatilia kiuchunguzi kwa mujibu wa taratibu zetu. Lengo letu kupitia Dawati la Jinsia na Watoto ni kuhakikisha tunapunguza kama sio kumaliza kabisa vitendo hivyo.

Eliakimu Kapele ni Makamu wa Shule ya Sekondari Kivesa

Anasema maranyingi ushahidi wa kesi kama hizo pia umekuwa ukiharibiwa na wahusika kabla ya kufika mahakamani, wanaweza baada ya kesi kufunguliwa wakashawishiana na kukaa nje bila ya sisi kujua na hivyo kupotea wote.

Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama anasema idadi ya matukio ya mimba shuleni hapo inapungua kwa sasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali, lakini si kwamba matukio hayo yamekoma kabisa.

“Matukio ya mimba kimsingi kwa sasa yanapungua…lakini si kwamba yamekwisha kabisa, tatizo kubwa ni malezi katika familia pamoja na vishawishi vingine,” anasema mwalimu huyo akizungumza shuleni Komnyang’anyo.

Napingana kwa mtazamo mwingine kwamba umbali wa makazi kwa wanafunzi unachangia mimba…nasema hivyo kwa kuwa kwa mwaka jana mwishoni kuna mfano mzuri, shuleni kwetu yupo mwanafunzi (wa kidato cha pili ‘C’) ambaye anahudumiwa kila kitu na pia yu-karibu na shule lakini amejikuta akipewa mimba na kukatishwa masomo.

Mwanafunzi huyu pia huwezi kumuingiza katika kundi la wanafunzi wenye mazingira magumu ya maisha katika familia zao, nasema hivyo kwa kuwa huyu analipiwa kila kitu, anapewa matumizi yote yanayoitajika na shirika moja linalosaidia wanafunzi wa kike lakini ameshindwa kuendelea baada ya kupewa mimba.

Kesi hii tayari ipo kwenye Serikali ya kijiji kwa hatua zaidi baada ya sisi kutoa taarifa. Sasa watu wanachukulia hatua si kama ilivyokuwa hapo nyuma.Tangu amekuwa huyu Mkuu wa Wilaya mpya (Muhingo Rweyemamu) wananchi wanatoa ushirikiano kwa kesi kama hizi. Kimsingi ujenzi wa mabweni itakuwa hauweni kwa wanafunzi ambao kwa sasa wanatokea vijiji vya mbali kuja shuleni, vijiji hivyo ni pamoja na Bangu, Kwamagome na Kwakonje.

Ofisa Elimu Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa

Mazungumzo ya wanafunzi Hamad Ngomero kidato III, Salome Kalage kidato cha IV, Michael Richard kidato cha I, Mwajuma Munga kidato cha II, Mwajabu Fungo kidato I na Farid Iddy kidato cha IV – wote kutoka Shule ya Sekondari Komnyang’anyo wanakubali kwa pamoja uwepo wa matukio ya mimba, japokuwa kwa sasa ni kwa kiwango kidogo.

Mwajuma Munga anasema matukio hayo bado yapo lakini yamepungua si kama ilivyokuwa hapo nyuma. Naye Salome Kalage anasema mfano kuanzia mwezi Januari 2013 anawajua wanafunzi watatu ambao wamepata mimba na kuachishwa shule. Anawataja wanafunzi hao ni pamoja na Kuruthumu Omar (IV), Elizabeth Hamis (IV) na Docas (III).

Kwa upande wake mwanafunzi Hamad Ngomero anasema tamaa za starehe na hali ngumu ya maisha katika familia kaadhaa wilayani Handeni ndiyo inayowaponza wanafunzi wa kike na hata kujikuta wakitiwa mimba na kukatishwa masomo.

Martin Mwingo ni Mwaliku Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari Kileleni; ujio wa Mkuu wa Mkoa mpya Handeni umeanza kuonesha mafanikio kwa upande wa matukio ya mimba kwa wanafunzi. “DC (Mkuu wa Wilaya) wasasa anajitahidi sana kupitia kampeni yake ya “Niache Nisome” anafuatilia kesi za mimba na kuhakikisha wahusika wanapata adhabu kwa mujibu wa sheria…mfano sasa hivi tuna kesi moja tumeletewa hizi ni juhudi za Mkuu wa Wilaya,” anasema Mwingo.

Kesi zinapungua mfano mwaka jana tulikuwa na kesi mbili za mimba lakini mwaka huu (2013) hadi sasa hatujapata kesi ya mimba…lakini pamoja na hayo malezi ya watoto kwa wazazi bado ni tatizo, mtoto ananyenyekea kea mzazi wake tu dharau kwa watu wengine-haya si malezi. Zamani mtoto anaweza kuadhibiwa na mkubwa yeyote ilimradi awe amekosa, lakini sasa sivyo.

“Mi nashangaa kila uchao watu wanang’ang’ania haki za watoto wasiadhibiwe uweke utaratibu wa kutoa adhabu lakini nashangaa kwanini wasitaje na wajibu wa mtoto hili ni muhimu…tusing’ang’anie haki za mwananafunzi tu tuoneshe na wajibu wake pia,” anasema Mwalimu Mwingo.

Anasema pamoja na juhudi hizo bado utandawazi unaathiri nidhamu za wanafunzi, umiliki wa simu za mkononi matumizi mabaya ya mitandao kama tovuti nayo yanawaharibu wanafunzi, ipo haja ya Serikali kuingilia na kupiga marufuku wanafunzi kumiliki simu shuleni maana simu inamambo mengi sasa.

Hussen Kigoma ni mwanafunzi wa kidato cha III, katika moja ya shule za kata Wilaya ya Handeni ambazo ndizo zimezokuwa na changamoto anuai. Anasema ipo haja ya kuwa na utaratibu wa kuwapima vipimo vya ujauzito mara kwa mara wanafunzi wa kike.

“Sasa hivi wapo ambao wanapata na kutoa mimba hizo bila uongozi wa shule kujua…sasa hivi tunawajua wanafunzi wawili ambao walipata mimba mwaka huu shuleni kwetu. Mfano Joyce Gasper na Jesca Paul wote wa kidato cha nne wamepata mimba…huenda mwaka huu mimba zikaongezeka zaidi,” anasema Hussein Kigoma.

Eliakimu Kapele ni Makamu wa Shule ya Sekondari Kivesa; anasema linapungu tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma. Mfano mwaka jana tulikuwa na matukio mengi ya kesi za mimba kwa wanafunzi, lakini hadi muda huu kwa 2013 tunayo matukio mawili tu. Na hatu zinachukuliwa maana msukumo unaanzia kutoka kwa viongozi wa Serikali za Mitaa.

Hii inatokana na Mkuu wa Wilaya wa sasa Muhingo Rweyemamu ametia mkazo sana masuala ya mimba kwa wanafunzi, watu wamekuwa makini na wafuatiliaji.

“Mfano sasa mimba inapotokea kuanzia mzazi wa mtoto aliyetiwa mimba, mtoto mwenyewe na mtuhumiwa wote wanashikiliwa…mi naamini kama adhabu hizi zitaendelea kutolewa ipasavyo watu watanyooka tu,” anasema mwalimu Kapele.

Hata hivyo mwalimu huyo anashauri mabadiliko ya sheria na kanuni za utoro shuleni, anasema maamuzi yamekuwa na mkanganyiko. Mfano kanuni za shule zinaelekeza kuwa mwanafunzi asipo hudhuria shule kwa siku 90 afukuzwe shule. Hili kwa sasa halifanyiki maana limekaa kisiasa zaidi…wanafunzi wanatoroka hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa maelekezo lakini baadaye wanarejeshwa kuja kufanya mitihani, hili ni tatizo.

“Inatokea mwanafunzi anabeba mimba na baadaye anarudi shuleni baada ya kujifungua, mwanafunzi kama huyu ni tatizo hawezi kuwa na vurugu sana kinidhamu na wakati mwingine anawavuruga hata wenzake maana anakuwa hana maadili.”

Shule yetu inautaratibu mzuri wa kuhakikisha muda wote unaofaa wanafunzi wanakuwa darasani kupata kilichowaleta hapa shuleni. Lakini huwezi kuamini kuna baadhi ya wanafunzi muda wote wapo huku vichochoroni wanajificha hawaji shuleni, utoro umekithiri! Lakini hawa huenda wakaruhusiwa kuja kufanya mitihani hapo baadaye.

Kanuni za shule mara kadhaa zimewekwa pembeni na siasa kuingizwa kwenye kanuni hizo, hali hii inawapa wanafunzi kiburi na uhuru mkubwa-huwenda wanadhani kufanya hivi ni kuwasaidia lakini ukweli ni kwamba wanawaharibu.

Ofisa Elimu Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa anakiri kuwepo na mabadiliko makubwa ya utoro wa mimba ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka jana. “Kimsingi huko nyuma utoro hasa wa mimba ulikithiri kwa wanafunzi wa Sekondari na Msingi, lakini hali ya sasa ni tofauti. Kuna mabadiliko kampeni ya ‘Niache Nisome’ imesaidia sana…kwa sasa wengi wanaohusika na kuwatia mimba wanafunzi wanapelekwa mahakamani,” anasema Muchiwa.

Anasema zoezi la kamatakamata lililokwenda sambamba na kampeni ya ‘Niache Nisome’ na watu hufikishwa kwenye hatua mbalimbali limesaidia hivyo mambo yanabadilika. Kwa mantiki hiyo waweza kuona kuanzia Januari 2013 hadi sasa (Machi) sijapokea kesi hata moja ya mimba.

Tunachokifanya sasa ni kutoa elimu zaidi kwenye mikutanyiko ya jamii kupitia viongozi wa ngazi mbalimbali za halmashauri, ili kuhakikisha tunafanikiwa zaidi tumeanza mkakati wa kuwajengea uwezo wananchi na shule. Hii ni kukabiliana na baa la njaa ambalo limekuwa likijitokeza mara kadhaa.

“Unajua mtu anapokuwa na njaa kushawishika ni rahisi…na Handeni kuna njaa sasa hali kama hii yaweza kuathiri pia sekta ya elimu, tumejipanga kuimarisha kilimo cha mazao kama mahindi na mtama shuleni ili wanafunzi wawe na uhakika wa chakula wawapo shuleni,” anasema Ofisa Elimu huyo wa Wilaya ya Handeni.

Ofisa Elimu Taaluma, Basil Mrutu anasema kwa mwaka jana kwa mujibu wa takwimu zao walikuwa na ripoti za mimba 26 kwa Wilaya nzima, lakini tangu Oktoba 2012 hadi sasa hawajapata kesi za matukio ya mimba.

Simon Mdaki ni Mkuu wa Idara ya Sekondari Wilaya ya Handeni; anasema kuwa “Halmashauri imeandaa matrekta 7 ambayo shule zitapewa kipaumbele cha kuyatumia ili kuweza kuendesha kilimo kwa ajili ya lishe kwa wanafunzi.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na TAMWA

Mwanafunzi Kidato cha Pili Abebeshwa Mzigo Kulea Familia
Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama akizungumza na mwandishi wa Thehabari.com

Mwanafunzi Mwenjuma Magalu (16), mstari wa pili kulia wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo

Na Joachim Mushi, Handeni

MWANAFUNZI wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Mwenjuma Magalu (16) amejikuta akibeba mzigo wa kulea familia baada ya familia hiyo kutelekezwa na babayake.

Mwanafunzi huyo anayeishi katika Kijini cha Msasa amejikuta katika hali hiyo ngumu baada ya mama yake mzazi, Hadija Magalu kufariki dunia ambaye ndiye aliyekuwa akiihudumia familia hiyo baada ya mzazi mwenzake (mumewe) kuitelekeza miaka minne iliyopita.

Mama huyo (Hadija Magalu) alifariki dunia Agosti, 2013 kwa matatizo ya uzazi na kuiacha familia hiyo ya watoto watatu aliyokuwa akiihudumia chini ya ulezi wa mamayake mzazi, Bibi Amina Mohamed.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni kijijini Msasa, mwanafunzi Magalu alisema amelazimika kuilea familia hiyo baada ya bibi yake aliyeachiwa familia hiyo kuugua ugonjwa wa TB na kushindwa kuendesha shughuli za kilimo na nyinginezo kuisaidia familia hiyo.

“Bibi ndiye aliyekuwa akitupikia, tutafutia chakula na tulikuwa tukishirikiana naye hata kulima…lakini kazi hizo zote kutokana na afya yake hawezi kuzifanya, ninalazimika kuzifanya mwenyewe. Japokuwa nipo shuleni lakini natakiwa kujua tutakula nini tunapata wapi pesa ya chakula na shughuli nyingine za familia,” alisema Magalu akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema familia yao hutegemea kilimo lakini wakati mwingine hulazimika kwenda kutafuta vibarua vya kufanya ili kupata pesa ya kula yeye pamoja na bibi yake. Aidha aliongeza kuwa wadogo zake wawili ambao awali alikuwa akikaa nao amelazimika kuwapeleka kwa mjomba wake baada ya kuona hali ni ngumu. Hata hivyo alisema wajomba zake nao hali yao ni ngumu hivyo wanashindwa kuhudumia familia hiyo.

Akizungumzia hali ya maisha ya familia hiyo Bibi. Amina Mohamed ambaye kwa sasa ni mgonjwa wa TB alikiri mwanafunzi huyo kuwa na majukumu mazito ya familia ambayo awali alikuwa ameyabeba yeye baada ya mwanaye kufariki dunia.

“Kweli mtoto huyu anaelemewa na malezi ya familia hii lakini sina cha kufanya kwa kuwa mimi ni mgonjwa wa TB na nimeshauriwa nisifanye kazi kwa sasa, hivyo kuanzia kupika, kulima shambani na hata kutafuta cha kula anafanya yeye baada ya kurudi shuleni,” alisema bibi huyo.

Mwanafunzi huyo ambaye anasomeshwa na msamaria mmoja aliyejitokeza baada ya familia yao kushindwa kumlipia ada amewaomba watu walioguswa na maisha ya familia hiyo kumsaidia.

Akizungumza hivi karibuni Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Nadhiru Kinyama alikiri hali ngumu kwa kijana huyo kutokana na mazingira ya familia yao na kuongeza anahitaji kusaidiwa hata fedha za kujikimu na gharama zingine za masomo, kwani mfadhili humlipia ada pekee.

Mwenjuma Magalu: TAMWA Imerejesha Ndoto Zangu Kielimu
Mwanafunzi, Mwenjuma Magalu

Na Joachim Mushi, Handeni

“BAADA ya kumaliza darasa la saba nilichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakini sikufanikiwa kuendelea na elimu hiyo kutokana na uwezo wa mzazi wangu mmoja (mama) ambaye alishindwa kumudu gharama zilizokuwa zikihitajika kwa wakati…,”ndivyo anavyoanza kusimulia Mwenjuma Magalu akizungumza Kijijini Msasa, Wilaya ya Handeni.

Magalu anasema furaha zote alizokuwa nazo mwaka 2011 baada ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, iliyopo kijijini Msasa Wilaya ya Handeni zilikuwa zikiyeyuka kadri siku zilivyokuwa zikikaribia kufunguliwa kwa shule za sekondari.

Anasema hadi shule zinafunguliwa mama yake alikuwa hajakamilisha vitu vilivyokuwa vikihitajika shuleni ikiwa ni pamoja na fedha ya ada ya kuanzia shule. Kijana huyo ambaye alikuwa akiishi na mama yake pamoja na wadogo zake wawili walitelekezwa na babayao miaka kadhaa iliyopita kijijini hapo baada ya baba huyo kudai anakwenda kutafuta maisha nje ya kijiji chake.

Hata hivyo kwa kuonesha ana uchu na elimu kijana Magalu hakumuachia mamayake jukumu la kuitafuta ada peke yake, naye alifanya vibarua huku na kule kijijini Msasa kwa kuamini huenda angelipata kitu na kufanikiwa kuingia shuleni. Lakini ilishindikana kwake kutokana na uduni wa kipato kwa mamayake, kwani fedha ambayo mara nyingine Magalu aliipata kwenye vibarua ililazimika kununua chakula. Hii ilikuwa ni changamoto nyingine kwa familia ya kijana huyo mdogo.

Baada ya ndoto za kujiunga na shule kutoweka bila mafanikio, Magalu aliamua kufanya vibarua na kampuni ya Kichina iliyokuwa ikitengeneza barabara ipitayo karibu na kijijini chao. Magalu anasema ndoto yake ya shule ilikuja kurejeshwa na utafiti wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 kwa kushirikiana na waandishi wa habari.

Bibi Amina Mohamed (kulia) mlezi wafamilia ya mwanafunzi Mwenjuma Magalu akifanya mahojiano na  mwanahabari Joachim Mushi, kijijini Msasa,wilayani Handeni.

“Baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari aliyekuja kijijini kwetu Msasa na kumweleza hali halisi, kilio change kilisikika kwawasamaria na kujitokeza kuisaidia familia yetu…kwa sasa nimepata ufadhili wa kusomeshwa hadi kidato cha nne,” anasema Magalu.

Mwenjuma Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo muda mfupi baada ya kupata ufadhili wa masomo akiwa bado na furaha alijikuta anaingia katika mtihani mwingine wa maisha baada ya mamayake mzazi kufariki dunia.

Hata hivyo baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya Handeni na taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa kile mamayake (kwa sasa marehemu) kutokuwa na uwezo kuripotiwa, alijitokeza mfadhili wa kugharamia masomo yake ambaye hadi sasa anafanya hivyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni Komnyang’anyo, mwanafunzi huyo aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa umma na kupatikana kwa mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya familia yao kutelekezwa.

Kwa upande wake bibi wa mtoto huyo (Amina Mohamed) ambaye aliachiwa familia hiyo baada ya kufariki kwa mwanaye, anamshukuru mfadhili wa mjukuu wake. “Binafsi nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi shuleni…hii kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa amekata tamaa kabisa kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua mitaani huku wenzake wakiendelea na shule,” anasema bibi huyo.

Bibi huyo anafafanua kuwa kwa sasa bado familia hiyo inahitaji msaada wa huduma hasa baada ya mwanaye (mama wa familia hiyo) kufariki dunia mwaka jana na kumuachia watoto wake.

Anasema yeye ndiye aliyebaki kulea familia hiyo baada ya mtoto wake kufariki. Lakini kwa sasa hali ya afya yake si nzuri, licha ya uzee alionao amepimwa na kubainika ni mgonjwa wa TB ambapo ameanza kutumia dawa hivyo kwa hali yake ameshauriwa kupumzika.

Anasema baada ya kushauriwa na daktari kupumzika, mzigo wa malezi ya familia sasa umejikuta ukielekea kwa mjukuu wake Mwenjuma ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo.  Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa katika uchunguzi uliofanywa tena juzi na mwandishi wa makala haya bibi huyo anabainisha kuwa mjukuu wake anamzigo mkubwa.

“Nasema anamzigo mkubwa kwa kuwa sasa anatakiwa kutekeleza majukumu ya shule na nyumbani kama yeye ndiye mlezi wa familia…namuhurumia sana lakini sina cha kufanya. Anaporudi shuleni anatakiwa kutafuta chakula cha familia, yeye pia ndiye mpishi, mchota maji na ndiye mkulima,” anamzigo mzito kweli ndiyo maana wakati mwingine nalazimika kuingilia licha ya afya yangu.

Muhingo Rweyemamu ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, anasema tatizo la uduni wa maisha kwa familia katika wilaya hiyo lipo kwa kiasi kikubwa. Anabainisha kuwa kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni haina mfumo maalumu kwa ajili ya kusaidia moja kwa moja familia kama hizo.

Anasema kinachofanyika ni kuhamasisha ndugu, jamaa na marafiki kuendelea kutoa msaada kwa familia ambazo zimekuwa katika wakati mgumu kimaisha na kuitaji msaada. “Kwa ujumla tunatoa elimu ya kuhakikisha wazazi wanazaa watoto ambao wanaweza kuwamudu kimatunzo…wajua wakati mwingine umasikini katika familia hizi huchangiwa na wanaume kuzaa bila mpangilio, unakuta mwanaume anakuwa na familia zaidi ya moja wakati hana kipato cha kumudu familia hizo,” anasema Rweyemamu.

Anasema kwa kuwa hili limesha jitokeza wamejipanga kuziwezesha shule kufanya uzalishaji wa kilimo ili wanafunzi waanze kupata chochote wawapo shuleni, halmashauri imepata vocha takribani 300 ambazo zitasaidia upatikanaji wa pembejeo kwa shule zitakazokuwa zikizalisha mazao kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi kama chakula wawapo shuleni mchana.

Halmashauri pia imejipanga katika uhamasishaji kilimo kwa familia pamoja na uwezeshaji katika nyanja anuai ili kukabiliana na janga la njaa pamoja na ugumu wa maisha kiujumla.

Wasichana Wadogo Waongoza Kuambukizwa VVU Nchini
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akisoma ripoti ya viashiria vya Ukimwi nchini katika mwaka 2011/12 baada ya kuizinduwa.

RIPOTI ya viashiria vya Ukimwi nchini katika mwaka 2011/12 imeonyesha kuwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 23 na 24 wameambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 6.6, ikilinganishwa na wavulana wa umri huo ambao ni asilimia 2.8. Akisoma ripoti hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania, (Tacaids), Dk Fatuma Mrisho alisema kiwango cha wasichana wa umri huo wenye virusi ni mara mbili zaidi ya wavulana.

Akizindua ripoti hiyo, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza Watanzania na sekta zote zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi, zitilie mkazo umuhimu wa kukomesha unyanyapaa na kuhamasisha upimaji wa hiari.

“Watanzania zaidi ya milioni mbili wamefariki tangu Ukimwi ugundulike miaka 30 iliyopita, tunatakiwa tupambane kwa dhati kabisa,” alisema Rais Kikwete.

Alipongeza ongezeko la idadi ya watu waliopima kwa hiari na kuwataka wanaume kupima badala ya kuwaachia jukumu hilo wanawake.

Rais pia alizitaka taasisi za Ukimwi, kudhibiti kasi ya maambukizi katika miji mikubwa na katika barabara kuu zikiwemo za Chalinze na Njombe.

“Maeneo hayo yanahitaji nguvu zaidi, hata maeneo yenye kiwango kidogo cha maambukizi nayo yasibweteke yanahitaji tahadhari,” alisema.

Kuhusu tohara kwa wanaume, Rais Kikwete alisisitiza zaidi tohara kwa wanaume na kwamba wasiotahiriwa wanaongeza kasi ya maambukizi kwa asilimia 60 na wanaotahiriwa wanapunguza kwa asilimia 60 pia.

Kwa upande wake, Dk Kikwete alisema maambukizi kwa vijana wenye umri mdogo yanatokea wakati vijana hao wana umri wa kati ya miaka 15 na 19 na matokeo yake kuwa wazi katika umri wa miaka 23 na 24. Alisisitiza kuwa matokeo haya ni kama ya sensa na kwamba si kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 14 hadi 49 amepimwa.

“Kwa jumla asilimia 2.0 ya wasichana na wavulana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wana maambukizi ya virusu,” alisema. Hata hivyo ripoti hiyo ilionyesha kuwa kasi ya maambukizi kwa Tanzania nzima, imepungua kutoka asilimia 5.8 mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/2012.

Utafiti wa kwanza wa aina hii ulifanywa mwaka 2003 -2004 ambapo maambukizi yalikuwa asilimia 7.06. Utafiti mwingine ulifanyika mwaka 2009-2010 ambapo maambukizi yalishuka toka asilimia 7 hadi asilimia 5.8

Pia, ripoti hiyo ilionyesha kuwa asilimia tisa ya wasichana na 10 ya wavulana wenye umri wa miaka 15 na 24 walianza kujamiiana kwa mara ya kwanza kabla ya kutimiza miaka 15.

Ripoti hiyo ilionyesha kuwa Mkoa wa Njombe una maambukizi ya juu zaidi ya asilimia 14.8 ya maambukizo kuliko mikoa yote Tanzania.

Maeneo ya visiwani yana asilimia ndogo zaidi ya maambukizi ambapo Unguja ilikuwa na asilimia 1.2 na Pemba asilimia 0.5 tu

“Matokeo ya ripoti hii yatatupa mwanya zaidi wa kujua nini kifanyike na wapi nguvu iongezwe katika kupambana na maradhi haya hatari,” alisema Kikwete.

Takwimu za sasa zinaonyesha kuwa maeneo ya mijini yana maambukizi mengi zaidi ambapo kwa wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.8, Ripoti hiyo ilionyesha kuwa zaidi ya robo ya Watanzania walioko kwenye ndoa wana maambukizi ya Ukimwi.

CHANZO: http://www.mwananchi.co.tz

Kesi za Mimba kwa Wanafunzi Zapungua Handeni
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu akizungumza na mwandishi wa habari hizi (hayupo pichani)

Ofisa Elimu wa Wilaya ya  Handeni, Mgaza Muchiwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi

Na Joachim Mushi, Handeni

MATUKIO ya kesi za kuwatia mimba/kuwabaka wanafunzi yaliokuwa yameshamiri katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Handeni sasa yameanza kupungua tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 na Machi 2013 matukio ya mimba yanapungua.

Akizungumzia hali hiyo juzi Wilayani Handeni, Ofisa Elimu wa Wilaya, Mgaza Muchiwa alisema matukio ya mimba kwa wanafunzi yanapungua tofauti na miaka ya nyuma ambapo matukio ya utoro wa mimba kwa wanafunzi yalikuwa mengi.

“Picha ya mwaka jana niliiona na tulikuwa tukifuatilia kwa karibu matukio ya kesi za mimba kwa wanafunzi…huwezi kufananisha na ilivyo sasa kunamabadiliko kwani matukio haya yamepungua,” alisema Muchiwa akizungumza na mwandishi ofisini kwake Handeni juzi.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera alithibitisha pia kupungua kwa kesi za mimba zinazofikishwa katika vituo vya Polisi ukilinganisha na hapo nyuma. Akifafanua zaidi kupitia taarifa za Dawati la Jinsia na Watoto Kituo cha Handeni, alisema hadi Novemba 2012 walipokea kesi 66 za matukio hayo lakini tangu hapo hadi Machi mwaka huu kesi hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa.

Uchunguzi uliofanywa na www.thehabari hivi karibuni katika shule za sekondari Komnyang’anyo, Kileleni na Kivesa zote za wilayani Handeni umeonesha kupungua kwa matukio ya mimba kwa wanafunzi, huku walimu wakidai hali hiyo imechangiwa na kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya, Muhingo Rweyemamu.

“Kweli kampeni ya ‘Niache Nisome’ iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya mpya imesaidia sana maana watu wameanza kuogopa kuwarubuni wanafunzi…hata wazazi na wanafunzi nao wanaogopa kuhusishwa katika kesi hizo hii imesaidia kupunguza matukio ya mimba,” alisema Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Komnyang’anyo Nadhiru Kinyama.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Rweyemamu Agosti 2012 alianzisha kampeni ya kupambana na watu waliyokuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi kwa kuwatia mimba na kuwaozesha kwa kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii juu ya umuhimu wa elimu wilayani humo.

*IMEANDALIWA NA WWW.THEHABARI.COM KWA KUSHIRIKIANA NA TAMWA

Utafiti wa TAMWA Wamrudisha Mwanafunzi shuleni Handeni
Bibi wa mwanafunzi Mwenjuma Magalu, Amina Mohamed akizungumza na Mhariri wa mtandao wa Thehabari, Joachim Mushi (kulia) kijijini Msasa, wilayani Handeni juzi.

Mwenjuma Magalu (wa kwanza kulia mstari wa pili) ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo akiwa darasani na baadhi ya wanafunzi wenzake alipotembelewa na mwandishi wa habari hizi.

Na Thehabari.com, Handeni

UTAFITI wa kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 umefanikisha kumrudisha shuleni mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa ametelekezwa yeye pamoja na familia yao.

Mwenjuma Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Komnyang’anyo alitelekezwa na babayake yeye pamoja na mamayake mwaka jana, hivyo kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo licha ya kuchanguliwa kuendelea na masomo.

Hata hivyo baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya Handeni na taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na sekondari baada ya mamayake (kwa sasa marehemu) kukosa uwezo kuripotiwa, alijitokeza mfadhili wa kumsomesha ambaye anagharamia masomo yake hadi sasa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni Komnyang’anyo, mwanafunzi huyo aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa umma na kupatikana kwa mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya familia yao kutelekezwa.

“Binafsi nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi shuleni…hii kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa amekata tamaa kabisa kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua mitaani huku wenzake wakiendelea na shule,” alisema bibi wa mtoto huyo, Amina Mohamed akizungumza.

Bibi huyo akizungumzia maisha ya sasa ya familia hiyo alisema bado wanahitaji msaada wa huduma hasa baada ya mwanaye kufariki dunia mwaka jana na kumuachia watoto wake.

Aliongeza kwa sasa yeye ni mgonjwa wa TB anayetumia dawa hivyo kwa hali yake ameshauriwa kupumzika jambo ambalo limempa mzigo mkubwa kimajukumu mwanafunzi (Mwenjuma), kufanya kazi za nymbani kama kupika kulima na shughuli nyingine.

Hata hivyo mama wa mtoto huyo (Hadija Magalu) ambaye alitelekezwa na mzazi mwenzake alifariki dunia mwaka jana kwa tatizo la uzazi na kuiacha tena familia hiyo ya watoto watatu katika hali ngumu zaidi chini ya malezi ya bibi mzaa mama.

Watanzania Ujerumani Kusherekea Miaka 49 ya Muungano
Ukumbi wa Circus Fabric

UMOJA wa Watanzania nchini Ujerumani (U.T.U) Unapenda kuwajulisha kwamba Sherehe za miaka ya Muungano Wa Tanzania Bara na Visiwani zitafanyika mjini Koloni, ujerumani Jumamosi ya Aprili 27, 2013 kuanzia saa 8 za Mchana, katika Ukumbi wa Circus Fabric uliopo; Bergisch Gladbacher Strasse 1007a, 51069 Köln.

Vikundi mbalimbali vinatarajiwa kutumbuiza katika shughuli ya Ufunguzi kuanzia saa 8 mchana. Vikundi hivyo ni pamoja na Maigizo ya Watoto, Sarakasi Za Watoto na Wakubwa, Ngoma za kiasili kutoka Tanzania, Break Dance pamoja na Live Bands.

Pia kutakuwa na Maonesho ya mavazi ya kisili ya Kitanzania, pamoja na chakula (a.k.a mnuso)

Kila Mtanzania anaweza kushiriki kuuza bidhaa zake binafsi za sanaa kama Vinyago, picha, michoro, ususi NK. kuchukua nafasi katika ratiba ya maonyesho, wasanii wanaotaka kushiriki katika maonyesho wanatakiwa kujiandikisha moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa UTU kupitia barua pepei ifuatayo-:

Imetolewa na Kamati.utu@googlemail.com

Cell:   +491733 779720

Cell    +491734297997

Umoja ni Nguvu! Utengano ni Udhaifu!