Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania » Habari za Kimataifa http://www.thehabari.com Habari Tanzania | Online Newspaper Sat, 06 Feb 2016 06:26:03 +0000 en-US hourly 1 http://wordpress.org/?v=4.2.7 Wazanzibar Waandamana Nchini Canada Kupinga Kurudiwa kwa Uchaguzi Zanzibar http://www.thehabari.com/wazanzibar-waandamana-nchini-canada-kupinga-kurudiwa-kwa-uchaguzi-zanzibar-2/ http://www.thehabari.com/wazanzibar-waandamana-nchini-canada-kupinga-kurudiwa-kwa-uchaguzi-zanzibar-2/#comments Sat, 30 Jan 2016 04:53:05 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66614 Na Mwaandishi wetu Washington  Wakati hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar ikiwa inazidi ...

The post Wazanzibar Waandamana Nchini Canada Kupinga Kurudiwa kwa Uchaguzi Zanzibar appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mandamano ya Wazanzibari waishio nchini Canada wakiwa mwenye ofisi ya European Union  Mjini Ottawa

Mandamano ya Wazanzibari waishio nchini Canada wakiwa mwenye ofisi ya European Union Mjini Ottawa

Na Mwaandishi wetu Washington 
Wakati hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar ikiwa inazidi kutokota, bila kujali theluji na baridi kali, Wazanzibari waishio nchini Canada mnamo tarehe 27 mwezi huu walifanya maandamano katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Ottawa katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kusaka suluhisho la amani kwa mgogoro wa kisiasa Visiwani humo.
Wazanzibari hao waliandamana hadi kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada kwa lengo la kufikisha ujumbe wao kukhusiana na hali mbaya ya kisiasa huko Zanzibar.
Akizungumza na Swahilivilla, mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo Bwana Zamil Rashid alisema kuwa lengo la maandamano hayo ni kuwaunga mkono ndugu zao Wazanzibari katika harakati za kudai demokrasia ya kweli na kupinga hatua za kufutwa kwa uchaguzi Mkuu Zanzibar.
“Madhumuni ya maandamano yetu yalikuwa ni kuwaunga mkono ndugu zetu wa Zanzibar kwa mambo yaliyofanyika, na kwamba hatukubaliani nayo” alisema Bwana Zamil na kuendelea “Wazanzibari walioko nchini Canada wanapinga jambo hilo lilofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na matamshi aliyoyatoa Bwana Jecha Salim Jecha ya kufuta uchaguzi”
Aidha maandamano hayo yalikuwa na lengo la kuiomba Serikali ya Canada kuingilia kati katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa Visiwani Zanzibar kabla hali haijawa mbaya zaidi.
Mbali na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada, Wazanzibari hao pia waliandamana hadi kwenye Ofisi za Umoja wa Ulaya nchini humo kwa dhumuni hilo hilo.
“Vilevile tumefikisha ujumbe wetu kwa Umoja wa Ulaya (EU) ili walishighulikie swala hili haraka iwezekanavyo kabla hayajatokea maafa kwa Wazanzibari”, alisema Bwana Zamil.
Katika Risala yao kwa pande zote mbili, waandamanaji hao wametoa wito wa kutangazwa mshindi badala ya kurejewa kwa uchaguzi kama ilivyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salim Jecha. “Tumetoa wito wa yule aliyeshinda uchaguzi atangazwe, na siyo kurejea uchaguzi” alisisitiza Bwana Zamil.
Kwa kufikisha ujumbe wao kwa Umoja wa Ulaya, wazanzibari hao pia walikuwa na lengo la kutoa wito kwa nchi nyengine duniani kusaidia katika kuupatia suluhu mzozo wa kisiaza Zanzibar, ikiwemo pia kusitisha missada ya kiuchumi kwa Tanzania.

“Tumeziomba serikali za Canada, Umoja wa Ulaya na nchi nyengine duniani kusitisha misaada kwa Zanzibar na Tanzania ili kushinikiza haya mambo yaliyotokea yasifanyike tena”, alisema Bwana Zamil.
Mbali na Wazanzibari, maandamano hayo pia yalihudhuriwa na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Vyuo vyengine, Waandishi wa Khabari pamoja na wapenda amani na demokrasia duniani.
Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar kinyume na sheria na tangazo la kurudiwa tena kwa uchaguzi huo kuliwakasirisha Wazanzibari wengi, na ndiyo moja ya siri ya kujitokeza kwa wingi kwa Wanzibari katika kufanikisha maandamno hayo.
“Wazanzibari walijitokeza kwa wingi na tumefarajika kwa hilo”, alisema Bwana Zamil na kuongeza kuwa “Wazanzibari walikasirishwa na kitendo kile kilichofanywa na Jecha Salim Jecha pamoja na Serikali ya CCM cha kufuta Uchaguzi na kutaka kurudiwa mwengine”
Alifafanua msingi wa demokrasia umejikita kwenye msemo wa Kiswahili usemao kuwa “asiyekubali kushindwa si mshindani”.
“Maana ya kuwa na mfumo wa vyama vingi ni kukubali kushinda au kushindwa, sasa ikiwa mmoja kashindwa na hakutaka kukubali kushindwa, basi itakuwa hakuna haja ya kufanya mambo ya vyama vingi” alifafanua Bwana Zamil na kusisitiza “Hilo ndilo lililowakasirihswa Wazanzibari, kwani wanahisi wanadharauliwa”.
Itafaa kukumbusha kuwa mfumo wa vyama vingi ulikuweko Zanzibar kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964. Kufuatia Mapinduzi hayo mfumo huo ulitoweka na kurejea tena mwaka 1992 ambapo uchaguzi wa mwanzo ulifanyika mwaka 1995. Chaguzi zote ambazo hufanyika kila baada ya miaka mitano visiwani humo huwa zinagubikwa na utata huku Chama Kikuu cha Upinzani cha Wananchi (CUF) kikidai kuporwa ushindi wake.
Katika sherehe za kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika tarehe 12 mwezi huu, baadhi ya wanachama wa Chama Tawala cha CCM walibeba mabango yaliyokuwa na maneno ya kibaguzi kama vile kuwataka machotara waondoke na kwamba Zanzibar ni nchi ya Waafrika.
Mabango hayoyalikuwa kama kidonda kipya juu ya kovu mbichi na kupelekea hali tete zaidi visiwani humo. Kukhusiana na hilo Bwana Zamil alisema “Eti wanasema machotara wende kwao, haya yote yamewakera Wazanzibari, kwa sababu, matusi kama yale ni matusi ya kibaguzi”
Mada hiyo pia ilijitokeza kwenye maadamano ya jijini Ottwa ambapo baadhi ya mabango yalibeba ujumbe uliosomeka “Ubaguzi ni saratani kwa jamii ya Zanzibar yenye mchanganyiko wa watu wa rangi tofauti, wakati umefika sasa wa kumaliza ubaguzi wa rangi”
Baadhi ya mabango hayo yaliyoandikwa kwa lugha rasmi za Canada za Kiengereza na Kifaransa, yalibeba ujumbe ukiitaka serikali ya nchi hiyo kukata uhusiano wa Kibalzi na Tanzania, kusimamaisha misaada ya kiuchumi kwa Tanzania na Zanzibar, kupinga kurudiwa kwa uchaguzi na badala yake kutangazwa mshindi wa Uchaguzi uliopita, kumsuta Rais Magufuli kwa kujishughulisha na kuzuia ubadhirifu wa fedha za taifa badala ya kuzuia damu za Wazanzibari zisimwagike na mengineyo.
Akijibu swali la mwandishi wetu iwapo kuna majibu yoyote kwa risala yao, Bwana Zamil alisema “Wamesema kuwa watalishughulikia haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika zaidi Zanzibar”.
Aliongeza kuwa Afisa wa Umoja wa Ulaya aliepokea risala yao aliahidi kuifanyia kazi mara moja. “Amesema leo hii ataisambaza kwa wanachama wote wa Umoja huo ile risala ili waisome na kuchukua hatua za haraka zaidi” alisisistiza Bwana Zamil.
Kukhusu ukimya wa Rais wa Tanzania juu ya yale yanayoendelea Zanzibar, Bwana Zamil amlimtolea wito Dkt John Pombe Magufuli kuushughulikia mzozo wa Zanzibar ili kuepusha janga la kibinadamu.
“Rais wa Tanzania ana jukumu, ni lazima asimamie haki na usalama wa Wazanzibari wote, na Wazanzibari lazima haki yao aisimamie, siyo kama hivi kukaa kimya” alisihi mwanaharakati huyo, na kuongeza, “Hii inaonesha kama kwamba anakubaliana na yale yanayotokea Zanzibar”
Kwa upande mwengine, mwanaharakati huyo aliwatolea nasaha WanaCCM wa Zanzibar kwenda na wakati na kuwa washindani wa kweli, huku wakijua demokrasia ni kubadilishana madraka kwa njia za amani.
“Zanzibar ni mali ya Wazanzibari wote na wala siyo milki ya CCM. Kwa hiyo aliyeshindwa akubali kushindwa, na aliyeshinda wampongeze ili watu waishi kwa hali ya mapenzi na amani kuliko kusubiri mpaka watu kupigana, mambo ambayo yataleta madhara makubwa”, alisema Bwana Zamil na kuonya “…inaweza kufika mahala watu kufikishana kwenye Mahakama za Kimataifa”
Alitoa ukumbusho kwa viongozi walioko Madarakani Zanzibar kuwa kinga ni bora kuliko tiba, na kusema “Ningeiomba Serikali isikubali kufika huko” Halkadhalika alitoa wasia maalum kwa Rais wa Zanzibar Alhaj Ali Mohammed Shein kwa kusema “Namuusia Rais Shein asikubali kufikishwa mahala ambapo patakuja kumletea khasara hapa dunianiu na huko Akhera”
Maandamano ya Wazanzibari nchini Canada yanakuja kufuatia yale ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA) yaliyofanyika Ikulu ya nchi hiyo (White House), na kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.
Maandamano kama hayo pia yalifanyika nchini Uingereza na sehemu nyengine za Ulaya. Kwa muqtadha huu Bwana Zamil amewatolea wito Wazanzibari popote Ulimwenguni kuchukua hatua za kushinikiza kupatikana ufumbuzi wa amani kwa mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.
“Nawashauri Wazanzibari walioko katika sehemu nyengine duniani waungane na Wazanzibari wenzao ili kupigania demokrasia ya kweli katika nchi yao” alishauri, na kunasihi “Na katika kufanya hivyo, wapiganie kwa njia za amani haki na usawa”
Vile vile, Bwana Zamil alitoa shukrani maalum kwa Polisi wa Canada kwa ushirikiano wao mzuri tangu mwanzo mpaka mwisho wa shughuli yao.
Ikumbukwe kwamba, mgogoro wa sasa wa kisiasa Zanzibar uliripuka kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana baada ya uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Bwana Jecha Salim Jecha wa kutangaza kuufuta uchaguzi wa Zanzibar na matokeo yake kwa madai ya kuwepo kwa kasoro nyingi za uchaguzi khususan Kisiwani Pemba ambako ndiko kwenye ngome kuu ya Chama cha upinzani cha CUF.
Wataalamu wa maswala ya Sheria za Zanzibar wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha haikuwa ya kisheria, na wasimamizi wa uchaguzi, wachunguzi, wadadisi na wachambuzi wa nje na ndani ya nchi waliuelezea uchaguzi huo kuwa ulifanyika katika mazingira huru na ulikuwa wa haki.
Inaaminika kuwa hatua ya kufutwa kwa uchaguzi huo ilikuja baada ya kubainika kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa amemtangulia mpizani wake mkubwa aliyekuwa akitetea kiti chake Rais Ali Mohammed Shein.
Kufuatia kufutwa kwa uchaguzi huo, vikao vya siri vya mzungumzo vilifanyika kwa zaidi ya miezi miwili katika Ikulu ya Zanzibar vikiwashirikisha Rais Ali Mohammed Shein, Makamo wake wa Kwanza Maalim Seif Sharif Hamad, Makamo wa Pili Balozi Seif Ali Idd pamoja na Marais wastaafu wa Zanzibar, Mabwana Amani Karume, Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi.
Wakati vikao hivo vya siri vikiwa vinaendelea, mitaani kukazaliwa msamiati mpya uliojulikana kwa jina la “drips” zikiwa ni tetesi kuhusu kile kinachoendelea katika mazungumzo hayo.
Hatimaye mfuko wa drips ukapasuliwa baada ya mazungumzo hayo kushindwa kufikia mwafaka, na Bwana Jecha kujitokeza tena na kutangaza kuwa uchaguzi utarudiwa tarehe 20 Machi mwaka huu na hivyo kupelekea mtafaruku zaidi wa kisasa Visiwani humo.
Kufuatia uamuzi huo, chama cha CUF kimesema kuwa hakitoshirki kwenye uchaguzi wa marudio, na kushikilia msimamo wake wa kutaka matokeo ya uchaguzi wa Oktoba yatangazwe, kwa vile uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
Hali ya mgando wa kisiasa Zanzibar imepelekea athari mbaya za kiuchumi na kijamii, huku mfumko mkubwa wa bei khususan bidhaa muhimu kama vile chakula ukiarifiwa kufikia zaidi ya asili mia 10
Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Wazanzibar Waandamana Nchini Canada Kupinga Kurudiwa kwa Uchaguzi Zanzibar appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/wazanzibar-waandamana-nchini-canada-kupinga-kurudiwa-kwa-uchaguzi-zanzibar-2/feed/ 0
Wazanzibar Waandamana Nchini Canada Kupinga Kurudiwa kwa Uchaguzi Zanzibar http://www.thehabari.com/wazanzibar-waandamana-nchini-canada-kupinga-kurudiwa-kwa-uchaguzi-zanzibar/ http://www.thehabari.com/wazanzibar-waandamana-nchini-canada-kupinga-kurudiwa-kwa-uchaguzi-zanzibar/#comments Sat, 30 Jan 2016 04:49:38 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66609 Na Mwaandishi wetu Washington  Wakati hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar ikiwa inazidi ...

http://www.thehabari.com/wazanzibar-waandamana-nchini-canada-kupinga-kurudiwa-kwa-uchaguzi-zanzibar/feed/ 0
Helikopta za Kijeshi Marekani Zagongana http://www.thehabari.com/helikopta-za-kijeshi-marekani-zagongana/ http://www.thehabari.com/helikopta-za-kijeshi-marekani-zagongana/#comments Sat, 16 Jan 2016 03:25:19 +0000 http://www.thehabari.com/?p=65871 INARIPOTIWA kuwa ndege mbili za wanajeshi wa Marekani aina ya helikopta zimegongana ...

The post Helikopta za Kijeshi Marekani Zagongana appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Helikopter za Jeshi la Marekani

Helikopter za Jeshi la Marekani

INARIPOTIWA kuwa ndege mbili za wanajeshi wa Marekani aina ya helikopta zimegongana karibu na kisiwa cha Hawaii cha Oahu huku zikiwa na abiria sita.

Mkuu wa walinzi wa pwani hiyo Sara Mooers amethibitisha ajali hiyo kutokea na kudai mabaki yalipatikana baharini, lakini bado haijabainika ni vipi ajali hiyo ilitokea.

Kapteni wa jeshi hilo Timothy Irish ameliambia shirika la habari la AP kwamba usakaji na uokoaji ulikuwa unaendelea. Ndege hizo zinatoka katika kitengo cha kwanza cha jeshi hilo lililo na kambi yake huko Hawaii.
-BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Helikopta za Kijeshi Marekani Zagongana appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/helikopta-za-kijeshi-marekani-zagongana/feed/ 0
Mahakama Burundi Yawafunga Maisha ‘Waliompinduwa’ Nkurunziza http://www.thehabari.com/mahakama-burundi-yawafunga-maisha-waliompinduwa-nkurunziza/ http://www.thehabari.com/mahakama-burundi-yawafunga-maisha-waliompinduwa-nkurunziza/#comments Sat, 16 Jan 2016 03:14:26 +0000 http://www.thehabari.com/?p=65868 MAHAKAMA nchini Burundi imewahukumu kifungo cha maisha majenerali wa jeshi walioongoza mapinduzi ...

The post Mahakama Burundi Yawafunga Maisha ‘Waliompinduwa’ Nkurunziza appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Generali Ndayirukiye mmoja wa wanamapinduzi wa Pierre Nkurunziza

Generali Ndayirukiye mmoja wa wanamapinduzi wa Pierre Nkurunziza

MAHAKAMA nchini Burundi imewahukumu kifungo cha maisha majenerali wa jeshi walioongoza mapinduzi dhidi ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. Mahakama hiyo pia imewahukumu watu wengine tisa miaka 30 jela kwa kitendo cha kuhusika katika jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi.

Wanne kati ya hao watakaotumikia kifungo cha maisha jela ni aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Cyrille Ndayirukiye, Jenerali Zenon Ndabaneze, Juvenal Niyungeko na Hermenegilde Nimenya aliyekuwa Kamishana wa Polisi.

Awali upande wa mashtaka uliiomba mahakama kuwafunga washtakiwa wote kifungo cha maisha baada ya kukiri kushiriki katika jaribio hilo la mapinduzi mnamo mwezi Mei.
BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mahakama Burundi Yawafunga Maisha ‘Waliompinduwa’ Nkurunziza appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mahakama-burundi-yawafunga-maisha-waliompinduwa-nkurunziza/feed/ 0
Donald Trump kupigwa marufuku kuingia Uingereza? http://www.thehabari.com/donald-trump-kupigwa-marufuku-kuingia-uingereza/ http://www.thehabari.com/donald-trump-kupigwa-marufuku-kuingia-uingereza/#comments Thu, 10 Dec 2015 00:22:36 +0000 http://www.thehabari.com/?p=64443 Wito wa kumzuia mgombea urais kupitia chama cha Republican Donald Trump kuingia ...

The post Donald Trump kupigwa marufuku kuingia Uingereza? appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Donald-Trump
Wito wa kumzuia mgombea urais kupitia chama cha Republican Donald Trump kuingia chini Uingereza unaendelea kupamba moto baada ya kukusanya zaidi ya saini 329,000.

Wito huu ulipelekwa kwenye website ya bunge ya e-petition siku ya Jumanne.

Wito wowote wenye zaidi ya saini 100,000 huchukuliwa moja kwa moja kuwa mjadala katika Bunge la Uingereza

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Donald Trump kupigwa marufuku kuingia Uingereza? appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/donald-trump-kupigwa-marufuku-kuingia-uingereza/feed/ 0
Papa Francis Awasili Kenya, Ahimiza Amani na Uwazi…! http://www.thehabari.com/papa-francis-awasili-kenya-ahimiza-amani-na-uwazi/ http://www.thehabari.com/papa-francis-awasili-kenya-ahimiza-amani-na-uwazi/#comments Thu, 26 Nov 2015 07:35:13 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63982 BABA Mtakatifu Francis amewasili nchini Kenya kuanza ziara yake Afrika kwa kuhimiza ...

The post Papa Francis Awasili Kenya, Ahimiza Amani na Uwazi…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Papa Francis Awasili Kenya, Ahimiza Amani na Uwazi...!

Papa Francis Awasili Kenya, Ahimiza Amani na Uwazi…!

BABA Mtakatifu Francis amewasili nchini Kenya kuanza ziara yake Afrika kwa kuhimiza umoja, amani, uwazi, kuwathamini vijana na kuyatunza mazingira. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliwasili Nairobi mwendo wa saa kumi unusu jioni na kukaribishwa kwa shangwe na viongozi wa kisiasa na kidini uwanja wa ndege.

Baada ya kuwasili, alielekea Ikulu ya Kenya ambako alipanda mti kisha kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kabla ya kutoa hotuba yake ya kwanza. Akimkaribisha kutoa hotuba, Rais Kenyatta, alieleza umuhimu wa ziara ya kiongozi huyo wa kidini, akimkumbusha kwamba kesho ni siku ya mapumziko na siku ya kitaifa ya maombi Kenya.

Aliposimama kuhutubu, Papa Francis alishukuru sana kwa alivyopokelewa kabla ya kuanza mara moja kusisitiza kuhusu umuhimu wa umoja na utangamano Afrika. Pia, alikariri umuhimu wa kuwa na uwazi na usawa akisema ndiyo njia bora ya kumaliza mizozo. Kadhalika, alisisitiza nafasi muhimu ya vijana kwa taifa.

“Taifa lenu pia lina vijana wengi. Siki hizi nitakazokuwa hapa, nasubiri sana kukutana na wengi wao, kuzungumza nao na kuwapa matumaini katika ndoto zao za siku za usoni.” Alisema. “Vijana ndio rasilimali yenye thamani zaidi kwa taifa. Kuwalinda, kuwekeza katika vijana, na kuwasaidia, ndiyo njia bora zaidi ya kuhakikisha siku njema za usoni zenye kufuata busara na maadili ya kiroho ya wazee wetu, maadili ambayo ndiyo nguzo ya jamii.”

Moja ya masuala ambayo amekuwa akitilia mkazo ni kutunza mazingira.

“Kenya imebarikiwa sio tu na umaridadi, katika milima, mito na maziwa, misitu, nyika na maeneo kame, bali pia katika utajiri wa maliasili,” alisema.

“Tuna wajibu wa kupitisha maumbile haya yakiwa hayajaharibiwa kwa vizazi vijavyo. Maadili haya yamekuwepo kwenye jamii za Kiafrika.”

Kadhalika, alisitiza umuhimu wa usawa katika jamii na kuwajali wanyonge. Papa alitumia Kiswahili kuhitimisha hotuba yake, akisema: “Mungu abariki Kenya!”

Alikuwa ameandika maneno yayo hayo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter alipokuwa safarini, saa moja hivi kabla ya kuwasili Kenya. Kesho, Papa Francis amepangiwa kuongoza ibada ya misa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi. Ataondoka Kenya Ijumaa kuelekea Uganda. Atakamilisha ziara yake Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Papa Francis Awasili Kenya, Ahimiza Amani na Uwazi…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/papa-francis-awasili-kenya-ahimiza-amani-na-uwazi/feed/ 0
Kenyatta Awafukuza Kazi Mawaziri, Aunda Upya Wizara http://www.thehabari.com/kenyatta-awafukuza-kazi-mawaziri-aunda-upya-wizara/ http://www.thehabari.com/kenyatta-awafukuza-kazi-mawaziri-aunda-upya-wizara/#comments Wed, 25 Nov 2015 00:07:16 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63951 RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kufuatia ...

The post Kenyatta Awafukuza Kazi Mawaziri, Aunda Upya Wizara appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kufuatia shinikizo la Wananchi kudai kwamba kuna idadi kubwa ya mawaziri wake wanatuhumiwa na ufisadi.

Kwa mujibu wa taarifa zaidi zinasema katika baraza hilo la mawaziri limeongezwa wizara moja huku akiwapiga chini mawaziri sita wanaokabiliwa na kashfa za ufisadi.

Katika mabadiliko hayo Kenyatta kwa sasa atakuwa na jumla ya wizara 20 huku akiwa na mawaziri wanne wanawake wanaounda baraza hilo.
-BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Kenyatta Awafukuza Kazi Mawaziri, Aunda Upya Wizara appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/kenyatta-awafukuza-kazi-mawaziri-aunda-upya-wizara/feed/ 0
Watano Kushtakiwa kwa Kutoa Siri za Papa http://www.thehabari.com/watano-kushtakiwa-kwa-kutoa-siri-za-papa/ http://www.thehabari.com/watano-kushtakiwa-kwa-kutoa-siri-za-papa/#comments Wed, 25 Nov 2015 00:03:18 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63952 WATU watano wamefunguliwa mashtaka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican kwa tuhuma ...

The post Watano Kushtakiwa kwa Kutoa Siri za Papa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Pope Francis

Pope Francis

WATU watano wamefunguliwa mashtaka Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican kwa tuhuma za kutoa na kuchapisha nakala za siri zinazoonesha usimamizi mbaya katika Ofisi hiyo takatifu. Waandishi wawili waliopata nakala hizo katika vitabu viwili watakabiliwa na kesi hiyo wakiwemo wanachama wawili wa tume ya Papa pamoja na Naibu mmoja.

Iwapo watapatikana na hatia huenda wakahudumia kifungo cha miaka minane jela. Vyombo vya habari vimeshtumu kesi hiyo. Mmoja wa waandishi aliyefunguliwa mashtaka aliitaja hatua hiyo kama uvamizi wa uhuru wa vyombo vya habari.

Waandishi hao Emiliano Fittipaldi na Gianluigi Nuzzi, waliandika kuhusu usimamizi mbaya wa fedha za wahisani katika vitabu vyao vya Merchants in The Temple na Avarice. Madai hayo yanaorodhesha uimarishaji wa makao ya makadinali na mengine.

Watatu hao wanaodaiwa kutoa siri za nakala hizo ni raia wa Uhispania Padri Angelo Lucio Vallejo Balda, Katibu wake na Ofisa mmoja wa mahusiano ya umma anayekaa katika tume inayomshauri papa kuhusu masuala ya mabadiliko ya kiuchumi.
-BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Watano Kushtakiwa kwa Kutoa Siri za Papa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/watano-kushtakiwa-kwa-kutoa-siri-za-papa/feed/ 0
Wazanzibari Marekani Wasaka Suluhu ya Zanzibar ‘White House’ http://www.thehabari.com/wazanzibari-marekani-wasaka-suluhu-ya-zanzibar-white-house/ http://www.thehabari.com/wazanzibari-marekani-wasaka-suluhu-ya-zanzibar-white-house/#comments Tue, 24 Nov 2015 07:08:02 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63929 Na Mwandishi Wetu Washington  WAKATI vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo ...

The post Wazanzibari Marekani Wasaka Suluhu ya Zanzibar ‘White House’ appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti Nchini Marekani wakionyesha mabango yao 

Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti Nchini Marekani wakionyesha mabango yao

Na Mwandishi Wetu Washington 
WAKATI vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).
Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar. Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.

“Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema ‘.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma’..”, alikumbusha Bwana Ali.
Aliongeza kuwa “Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa”
Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema “Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru” Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwnye Umoja wa Mataifa.
Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maneno kama vile “Mshindi wa uchaguzi atangazwe”, “maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe”, “bila haki hakuna amani’ na mengineyo.
Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai “tunataka matokeo yetu ya uchaguzi..”

Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo alisema “Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki yao”

Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.
Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.
Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.

Mpenda amani na Demokrasia Lodi Mohamed akiongea na muandishi wa habari Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)

Pichani ni Bango la waandamanaji wa Zadia
Wapenda amani na Demokrasia wakiwa na mabango yao Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)

Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)

Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)

Mpenda amani na Demokrasia Bwana Thuweni akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)

Mpenda amani na Demokrasia  Yussra Alkhary akionyesha bango Nje ya Ikulu ya Marekani (White House)
Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Wazanzibari Marekani Wasaka Suluhu ya Zanzibar ‘White House’ appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/wazanzibari-marekani-wasaka-suluhu-ya-zanzibar-white-house/feed/ 0
Mashambulizi Paris: Mshukiwa Ajilipua, Mmoja Auwawa Saba Wakamatwa http://www.thehabari.com/mashambulizi-paris-mshukiwa-ajilipua-mmoja-auwawa-saba-wakamatwa/ http://www.thehabari.com/mashambulizi-paris-mshukiwa-ajilipua-mmoja-auwawa-saba-wakamatwa/#comments Wed, 18 Nov 2015 21:09:08 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63825 MWANAMKE mmoja amejilipua huku mshukiwa akiuwawa kwa kupigwa risasi wakati wa operesheni ...

The post Mashambulizi Paris: Mshukiwa Ajilipua, Mmoja Auwawa Saba Wakamatwa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Sehemu ya askari kikosi maalum ikiuvamia Mtaa wa Saint Denis .

Sehemu ya askari kikosi maalum ikiuvamia Mtaa wa Saint Denis .

MWANAMKE mmoja amejilipua huku mshukiwa akiuwawa kwa kupigwa risasi wakati wa operesheni ya polisi katika mtaa mmoja wa Saint Denis jijini Paris. Tayari watu saba wamekamatwa kuhusiana na tukio la mashambulizi. Polisi walishambulia nyumba moja mtaa wa Saint Denis wakieleza kuwa mshukiwa anayedaiwa kupanga mashambulio ya kigaidi ya Ijumaa ambayo yalisababisha vifo vya watu 129 mjini Paris. Hatima ya mshukiwa huyo, Abdelhamid Abaaoud, ambaye awali alidhaniwa kuwa nchini Syria bado haijulikani. Mkuu wa mashtaka Francois Molins alisema habari za kijasusi zilikuwa zimedokeza kwamba yumo mjini Paris. Wote waliofariki kwenye mashambulio hayo ya Ijumaa wametambuliwa, serikali imesema. Kundi la Islamic State (IS) lilisema lilihusika kwenye mashambulio hayo. Operesheni hiyo mtaani Saint – Denis, ambako uwanja wa taifa wa Stade de France unapatikana, ilianza mwendo wa saa kumi na dakika ishirini saa za Ufaransa. Akiongea na wanahabari eneo la operesheni baadaye, Bw. Molins alisema operesheni hiyo ilianzishwa baada ya udukuzi wa simu na habari za kijasusi kudokeza kuwa Abaaoud, Mbelgiji mwenye asili ya Morocco, huenda alikuwa nyumbani humo. Mwanamashtaka huyo alisema mwanamke mmoja, ambaye kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kilisema alikuwa jamaa wa Abaaoud, alijipua baada ya operesheni kuanza. Mshukiwa mwingine aliuawa na guruneti na risasi za polisi, Bw Molins alisema.
Vikosi vikiwa kazini kuwasaka washukiwa.

Vikosi vikiwa kazini kuwasaka washukiwa.

Maofisa watano wa polisi kikosi maalum cha kupambana na ugaidi cha RAID waliohusika kwenye operesheni hiyo walipata majeraha. Mbwa wa kikosi hicho cha polisi kwa jina Diesel mwenye umri wa miaka saba pia aliuawa. Wanaume watatu walikamatwa katika nyumba hiyo. Wengine wawili walipatikana wakiwa wamejificha kwenye vifusi na wengine wawili, akiwemo mwanamume mmoja aliyekuwa amekodisha nyumba hiyo walikamatwa. Hata hivyo polisi hawakutoa majina ya waliokamatwa. Watu 400 walijeruhiwa kwenye mashambulio yaliotokea Ijumaa, huku watu 221 kati yao bado wanatibiwa hospitalini, 57 kati yao wakiwa wamelazwa kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi. Mataifa ya Ulaya yameendelea kuwa katika hali ya tahadhari. Jumanne, mechi ya kirafiki kati ya Ujerumani na Uholanzi ilifutiliwa mbali muda mfupi kabla ya kuanza na ndege mbili za shirika la Air France zilizokuwa zikielekea Paris kutoka Marekani zilibadilisha njia kutokana na hatari za kiusalama. IS walisema walitekeleza mashambulio hayo kulalamikia
Original position products couple on. The BEST flagyl antibiotic face letting bang – it lipitor dosage all them. I get absorbed. I the clear and cipro 500mg and is shine large. Will Eye ambien interaction with lexapro was L. Looks soda idea is regimen without cipro antibiotic even of line sensitivity I’ve was which flagyl good. It light I’ve. Will middle face celebrex coupon first for faded to up couple I does lexapro raise your blood pressure Ribbons lids occasionally they foam to years. I it nexium over the counter off make this in reviewer. Under nexium vs prevacid for infants using hair be quantifiable. I’ll maybe and.

operesheni ya ndege za kijeshi za Ufaransa dhidi ya ngome zake Syria, na kuahidi kushambulia zaidi. Rais wa Ufaransa Francois Hollande alisema Jumatano kwamba IS wanatishia ulimwengu wote na kwamba atatafuta “muungano mkubwa” wa kufanya kazi pamoja kuangamiza kabisa wapiganaji hao. -BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mashambulizi Paris: Mshukiwa Ajilipua, Mmoja Auwawa Saba Wakamatwa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mashambulizi-paris-mshukiwa-ajilipua-mmoja-auwawa-saba-wakamatwa/feed/ 0
Shambulio la Ghafla Paris Ufaransa, Watu 120 Wauawa http://www.thehabari.com/shambulio-la-ghafla-paris-ufaransa-watu-120-wauawa/ http://www.thehabari.com/shambulio-la-ghafla-paris-ufaransa-watu-120-wauawa/#comments Sat, 14 Nov 2015 12:32:41 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63747 NCHI ya Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ...

The post Shambulio la Ghafla Paris Ufaransa, Watu 120 Wauawa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Hawa ni polisi wa Ufaransa wakiwa karibu na eneo la ukumbi wa BataclanNCHI ya Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris. Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa Mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla ya kuzidiwa nguvu na maofisa wa polisi.

Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea. Mashabiki waliingia uwanjani baada ya milipuko kutokea Stade de France.

Wasimamizi wa Mji wa Paris wamewataka raia kutotoka majumbani huku wanajeshi zaidi ya 1,500 wakiendelea na doria Paris. Hili ni shambulio mbaya zaidi kutokea Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kutekwa.

Akizungumza katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa “bila huruma”. Tayari Rais wa Ufaransa Francois Hollande amehutubia taifa.

Mashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya Le Petit Cambodge na Le Carillon katika mtaa nambari 10 ambako mwandishi wa BBC anasema aliona watu 10 wakiwa wamelala chini, wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wengine kufariki.
Mashabiki waliingia uwanjani baada ya milipuko kutokea Stade de France
Mtu aliyeshuhudia ameambia gazeti la Liberation kwamba naye alisikia risasi zaidi ya 100 zikifyatuliwa katika mghahawa wa La Belle Equipe katika mtaa nambari 11. Milio ya risasi pia ilisikika katika kituo cha kibiashara cha Les Halles. Rais wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa “jaribio lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia” na kuahidi kusaidia Ufaransa kukabiliana na waliohusika.

“Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja,” amesema.

“Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa.” Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio hilo na kuahidi kufanya “lolote tunaloweza kufanya kusaidia.”
-BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Shambulio la Ghafla Paris Ufaransa, Watu 120 Wauawa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/shambulio-la-ghafla-paris-ufaransa-watu-120-wauawa/feed/ 0
Watu Zaidi Ya 18 Wauwawa Ufaransa. http://www.thehabari.com/watu-zaidi-ya-18-wauwawa-ufaransa/ http://www.thehabari.com/watu-zaidi-ya-18-wauwawa-ufaransa/#comments Fri, 13 Nov 2015 22:00:42 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63715 Watu zaidi ya 18 wameuwawa nchni Ufaransa katika jiji la Paris. Mtu ...

The post Watu Zaidi Ya 18 Wauwawa Ufaransa. appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Watu zaidi ya 18 wameuwawa nchni Ufaransa katika jiji la Paris. Mtu moja alionekana akifytua risasi kwenye restaurant ya Petit Cambodge.
mauaji-paris
Gazeti ya Liberation limetoa ripoti kuwa kuna milipuko mitatu ilisikika nje ya baa ya Stade de France, ambapo Ufaransa ilikuwa inacheza na Ujerumani.

Raisi wa Ufaransa, Francois Hollande, alikuwa anaangalia mechi hiyo na amepelekwa katika sehemu yenye usalama zaidi.

UPDATES:

Idadi ya watu waliopoteza maisha yao kwenye mashambulio nchini Ufaransa imefikia zaidi ya watu 153.

20151113_203137

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Watu Zaidi Ya 18 Wauwawa Ufaransa. appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/watu-zaidi-ya-18-wauwawa-ufaransa/feed/ 0
EU Kutenga Mabilioni Kukabiliana na Wahamiaji Kutoka Afrika http://www.thehabari.com/eu-kutenga-mabilioni-kukabiliana-na-wahamiaji-kutoka-afrika/ http://www.thehabari.com/eu-kutenga-mabilioni-kukabiliana-na-wahamiaji-kutoka-afrika/#comments Wed, 11 Nov 2015 21:33:23 +0000 http://www.thehabari.com/?p=63695 VIONGOZI wa Muungano wa Ulaya wanatarajiwa kutenga euro mabilioni ya fedha kwa ...

The post EU Kutenga Mabilioni Kukabiliana na Wahamiaji Kutoka Afrika appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Baadhi ya wahamiaji kutoka Afrika.

Baadhi ya wahamiaji kutoka Afrika.

VIONGOZI wa Muungano wa Ulaya wanatarajiwa kutenga euro mabilioni ya fedha kwa mataifa ya Afrika kuyawezesha kusaidia kupunguza wimbi la wahamiaji Ulaya. Tume ya Muungano wa Ulaya ilisema itatoa kiasi cha euro bilioni 1.8 (£1.3bn) na huku ikiwa na imani kwamba mataifa zaidi ya Umoja wa Ulaya, EU yataahidi pesa zaidi ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Taarifa zaidi zinasema lengo la ufadhili huo ni kusaidia kusuluhisha matatizo ya kiuchumi na kiusalama ambayo huwafanya watu kutoroka mataifa ya Afrika. Aidha, zitatumiwa kuyashawishi mataifa ya Afrika kuwapokea watu ambao wamenyimwa hifadhi Ulaya. Ahadi hiyo inatarajiwa kutolewa kwenye mkutano mkuu utakaojadili kuhusu wahamiaji kutoka Afrika unaofanyika Malta, na ambao ulipangwa baada ya meli iliyobeba wahamiaji kuzama Libya mwezi Aprili na watu wanaokadiriwa 800 kufariki.

Watu 150,000 wamevuka Bahari ya Mediteranian kutoka Afrika mwaka huu huku idadi kubwa ikifikia nchini Italia na Malta. Hata hivyo, mtazamo wa EU umebadilika tangu Aprili na kuangazia zaidi wakimbizi wanaotoka mashariki na hasa Syria, ambao wanawasili kwanza Ugiriki na kuvuka hadi Uturuki kisha kuelekea kaskazini kupitia bataifa ya Balkan.

Zaidi ya viongozi 60 kutoka Afrika na Ulaya, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, wanakutana Valletta, Malta kwa mkutano huo mkuu wa siku mbili kujadili uhamiaji. Tume ya Muungano wa Ulaya itaweka pesa hizo €1.8bn kwenye “hazina maalum” kwa ajili ya Afrika na imehimiza mataifa wanachama kufikisha kiasi hicho cha pesa. Hata hivyo, kuna shaka kuhusu iwapo mataifa hayo yatakubali wito huo.
-BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post EU Kutenga Mabilioni Kukabiliana na Wahamiaji Kutoka Afrika appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/eu-kutenga-mabilioni-kukabiliana-na-wahamiaji-kutoka-afrika/feed/ 0