Blogs Tanzania | News | Michuzi ya Habari leo » Habari za Kimataifa

Obama Kuzuru Afrika, Mashambulio Iraq 95 Wauwawa
Rais wa Marekani, Barack Obama

RAIS wa Marekani anatarajiwa kuzuru Bara la Afrika mwezi ujao ambako atazuru mataifa ya Senegal, Afrika kusini na Tanzania. Katika taarifa msemaji wa Ikulu ya Rais Jay Carney amesema Obama anapangiwa kufanya ziara hiyo kati ya tarehe 28 mwezi ujao hadi tarehe 3 mwezi Julai ambako atakutana na viongozi wa serikali, biashara na wa mashirika ya kijamii kwa lengo la kuhimiza amani na ustawi wa bara Afrika.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Rais huyo wa Marekani atasisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na nchi za Afrika ikiwemo kupanua ukuaji wa kiuchumi, uwekezaji na biashara pamoja na kuboresha asasi za kidemokrasia. Mara ya mwisho kwa Obama kuzuru nchi ya bara Afrika ni mwaka 2009 alipozuru Ghana. Rais Obama hatarajiwi kuzuru Kenya.

Mashambulio Iraq 95 Wauwawa

Kiasi ya watu 95 wameuawa nchini Iraq hapo jana katika wimbi la mashambulio yanayowalenga waislamu wa kishia. Mashambulio kumi ya mabomu yaliripotiwa katika mji mkuu Baghdad na mashambulio mengine mawili katika mji unaokaliwa na washia wa Basra ulioko kilomita 420 kusini mashariki mwa nchi hiyo. Zaidi ya watu 150 pia wamejeruhiwa katika mashambulio hayo ya hapo jana.

Zaidi ya watu 240 wameuawa nchini Iraq katika kipindi cha wiki moja iliyopita katika mashambulio kati ya washia wanaoingoza Iraq na waislamu wa kisunni walio wachache na kuzua hofu ya taifa hilo kutumbukia tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kama vilivyoshuhudiwa mwaka 2006. Mashambulio ya hapo jana pia yalilenga maeneo ya wasunni katika mji wa Samarra ulioko kaskazini mwa Baghdad na katika jimbo la Anbar. Marekani imelaani mashambulio hayo na kutoa wito wa kuwepo utulivu nchini humo.

-DW

Polisi Uganda Wavamia Ofisi za Vyombo vya Habari Kusaka Kielelezo
Rais wa Uganda, Gen. Yoweri Museveni

POLISI nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais. Taarifa zinasema vituo viwili vya Redio pia vilivamiwa limeandika Gazeti la Serikali la New Vision.

Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa zipo njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda. Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji ilitolewa na Mkuu fulani wa Jeshi la Uganda.

Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung’atuka uongozini mwaka 2016. Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini kushikilia uongozi wa Uganda. Hata hivyo Serikali ya Museveni imekanusha taarifa hizo na kudai ni za uzushi.

Mwanawe Museveni Brig. Kainerugaba. Wiki iliyopita magazeti ya The Daily Monitor na Red Pepper, yalichapisha barua ya siri ikidai ilikuwa imeandikwa na Jeneral David Sejusa, ikitaka uchunguzi ufanywe kuthibitisha madai kwamba kuna mipango ya kuwauwa wote watakao pinga mipango ya Rais Museveni kumpachika mwanawe uongozini.

Uvamizi uliofanywa kwa magazeti na vituo vya polisi umeidhinishwa na Mahakama ya Uganda huku ukielezwa unalengo la kutafuta barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na mkuu huyo wa Jeshi akifichua njama za mauaji. Vituo viwili vya Redio vinavyohusiana na Daily Monitor, Dembe FM na KFM, pia vilivamiwa na kuzimwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Daily Monitor Bwana Alex Assimwe aliiambia BBC kwamba chumba chao cha Habari kilivamiwa na polisi wapatao 50 waliojihami kwa silaha.

Lakini wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanadai kuwa ikiwa barua ya Jenerali Sejusa ni ya kweli basi ni dalili kuwa kuna hali mvutano ndani ya jeshi huku ikidhaniwa kuwa wanajeshi wakongwe huenda wanapoteza uwezo kwa wanajeshi chipukizi wanaoongozwa na mwanawe Museveni Brigadia Kainerugaba.

Jenerali Sejusa ni mwanajeshi mkongwe aliyekuwa katika vita vya ukombozi uliyomuweka Rais Museveni madarakani mwaka 1986. Kwa mujibu wa taarifa za AP kamanda mmoja wa jeshi Jenerali Aronda Nyakairima amenukiliwa akisema kuwa Jenerali Sejusa kwa wakati huu anachunguzwa kutokana na barua anayodaiwa kuiandika.

-BBC

Watu Wanne Wafa, 13 Wajeruhiwa Katika Msongamano Kanisani, Achebe Kuzikwa
Kanisa likiwa limefurika waumini

WATU wane wamekufa na 13 kujeruhiwa katika mkanyagano ndani ya Kanisa la Kievangelisti nchini Ghana. Taarifa zinazohusianaafrika magharibiAjali hiyo ilitokea pale waumini walipoania kufikia maji matakatifu katika tawi la kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) katika Mji Mkuu, Accra.

Ripoti zinasema maelfu ya watu walikuwa wamekwenda kanisani humo. Kanisa hilo liloanzishwa na kasisi wa Nigeria, TB Joshua, ambaye anasema yeye ni mtume. Piya amezusha utata kwa kudai kuwa anaweza kutibu magonjwa yasiyotibika kama HIV na UKIMWI.

Wakati huo huo; mazishi ya mwandishi maarufu wa riwaya wa Nigeria, Chinua Achebe, yameanza katika mji wa Ogidi, kusini-mashariki mwa nchi ambako ndiko alikotoka.

Taarifa zinasema shughuli za maziko zinaendelea kwa juma zima, kumkumbuka na kusherehekea maisha ya mmoja kati ya waandishi maarufu kabisa wa Afrika. Bwana Achebe alifariki mwezi March akiwa na umri wa miaka 82.

Kongamano la waandishi, mihadhara ya wasomi na kanivali ni baadhi ya matukio katika mazishi ya wiki moja ya mwandishi Chinua Achebe. Shughuli zitakuwa nyingi katika mji wa Ogidi alikozaliwa kusini-mashariki mwa Nigeria.

Wageni kutoka pembe zote za dunia wanatarajiwa kutoa heshima zao za mwisho kwa yule waliyemwita baba wa fasihi ya kisasa ya Afrika. Bwana Achebe aliwakosoa viongozi wa Nigeria, hata hivo wanasiasa wengi maarufu wanatarajiwa kuhudhuria matanga yake.

Maziko yatafuata taratibu za Kikristo na utamaduni wa kabila lake la Igbo. Chinua Achebe alikuwa maarufu kwa mtindo wake wa uandishi ambao umefuata mila ya kutoa hadithi ya kabila lake la Igbo. Kitabu cha Chinua Achebe Things Fall Apart kimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 50.

-BBC

Wapiganaji 30 wa Boko Haram Wauwawa Nigeria
Baadhi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram

TAKRIBAN wapiganaji 30, wa waasi nchini Nigeria, wameuawa kwenye mashambulio ya anga yaliyofanywa na jeshi la serikali, Kaskazini Mashariki mwa nchini hiyo. Msemaji wa jeshi la Nigeria, amesema, ndege za kivita na helicopta zilitumika kushambulia kambi kadhaa wa waasi hao.

Aidha ameiambia BBC kuwa ndege moja ilishambuliwa kwa kombora na waasi hao lakini ilifanikiwa kurejea salama hadi kambi yao. Serikali ya Nigeria ilitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya Kaskazini Mashariki, yanayoshuhudia mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram.

Kwa sasa jeshi la Nigeria, linajaribu kutwaa uthibiti wa majimbo ya Adamawa, Yobe na Borno kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram. Wakati huo huo, milipuko na milio ya risasi imesikika usiku kucka katika jimbo la Katsina.

Raia wameiambia BBC kuwa mabenki, vituo vya polisi na magerza yaliharibiwa kufuatia mapigano makali mjini Daura karibu na mpaka wa nchi hiyo na Niger. Wanasema wameona miili ya wanajeshi watano na mitatu ya wapiganaji wa waasi lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa.

Mawasiliano ya simu ya mkononi yamekatizwa katika maeneo mengi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Lakini afisa mmoja wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa mitandao ya simu ilifungwa wakati wa operesheni hiyo ya kijeshi.

-BBC

Mapambano Dhidi ya Boko Haram Mipakani Nchini Nigeria
Baadhi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram

SERIKALI ya Nigeria imetuma kikosi kikubwa cha wanajeshi pamoja na silaha kukabiliana na wapiganaji wa kikundi cha Boko Haram katika majimbo matatu ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa kutoka kwa serikali ilisema kuwa nia ya kutumwa kwa wanajeshi hao ni kuweza kudhibiti wa sehemu ambazo inaaminika ziko chini ya udhibiti wa wapiganaji hao, pamoja na kuimarisha usalama

Jumanne Rais Goodluck Jonathan, alitangaza hali ya hatari, katika majimbo matatu ya Yobe, Borno na Adamawa baada ya majimbo hayo kushuhudia mashambulizi mabaya sana. Wapiganaji kutoka kundi la Boko Haram, wanalaumiwa kwa kufanya mashambulizi hayo. Kundi hilo ambalo lina mizizi yake Kaskazini mwa Nigeria,limehusishwa na mauaji ya watu 2,000 tangu mwaka 2010.

Boko Haram, limedhibiti baadhi ya sehemu za kaskazini mwa nchi, kwa miaka mitatu iliyopita na nyingi ya ghasia wanazofanya zimekuwa sana sana katika eneo hilo. Hakuna shaka kuwa hali Kaskazini mwa Nigeria inaendelea kuzorota na sasa rais Goodluck Jonathan amekiri hilo. Hakuna yeyote serikali angeweza kulitamka hilo.

Ukubwa wa mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram, umelazimisha rais Jonathan kuchukua hatua na hata kuwanyamazisha baadhi ya wakosoaji wake wanaosema kuwa amejikokota kuchukua hatua.

Baadhi ya wadadisi wamependekeza kuwa ikiwa hali itaandelea kuzorota hivyo, itakuwa vigumu kukabiliana na kundi la Boko Haram na litaweza hata kuunda taasisi zake. Je, wanajeshi zaidi wataweza kukabiliana na hali? kikubwa ni ambavyo wanajeshi hao wataendesha harakati zao.

Wadadisi wanasema kuwa , jeshi lina kibarua kigumu kwani kuna dalili tayari limeshindwa katika vita hivi, na raia wanahisi kuwa katikati ya mtego Nigeria

-BBC

Hali ya Hatari Yatangazwa Nchini Nigeria
Rais wa Nigeria, Good Luck Johnthan

MSEMAJI wa Rais wa Nigeria, Davip Okupi amesema rais Good Luck Johnthan ametangaza hali ya hatari katika majimbo matatu kaskazini mwa nchi. Akifafanua zaidi ameongeza kuwa hatua ya Rais Johnthan kufanya uamuzi wa kutangaza hali ya hatari ni kuzuia taifa hilo kutumbukia kwenye vita.

Msemaji huyo Davip Okupi ameambia BBC kwamba magavana wa majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa wameunga mkono mipango ya sasa, ili kukabiliana na mashambulio yanayotekelezwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.

Akilihutubia taifa kupitia Runinga, Rais Good Luck Jonathan alisema serikali itatumia kila mbinu kumaliza kundi hilo. Aliongeza kuwa wanamgambo walio na agenda ya kufanya mauaji ya halaiki, wametangaza vita nchini Nigeria. Rais kwa mara ya kwanza amekubali kuwa sehemu kadfhaa za nchi haziko chini ya udhibiti wa serikali.

-BBC

Wagonjwa wa Akili Watoroka Hospitalini Kenya, Boko Haram wamewateka Watoto
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

POLISI wanawatafuta wagonjwa karibia arobaini waliotoroka kutoka hospitali ya watu wenye matatizo ya kiakili, mjini Nairobi ya Mathare. Wagonjwa hao wanasemekana waliwashinda nguvu walinzi wao na kutoroka.

Zogo hilo lilizuka katika hospitali ya Mathare baada ya kutokea hali ya sintofahamu iliyowahusisha wafungwa arobaini wanaume. Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa wagonjwa hao walikuwa wanateta kuhusu hali mbaya na kibinadamu katika hospitali hiyo.

Wakati huo huo, wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake na watoto katika kujibu hatua ya jeshi kuwakamata wake za wanachama wa kundi hilo pamoja na watoto wao. Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alitoa kanda ya video inayoonyesha wanawake na watoto waliowakamata.

Habari zinazohusianaMakao ya polisi yashambuliwa NigeriaKiongozi wa Boko Haram akombolewaTaarifa zinazohusianaSiasaIkiwa hili litathibitishwa, watakuwa mateka wa kwanza raia wa Nigeria kutekwa nyara na kundi la Boko Haram. Shekau pia alisema kuwa kundi hilo ndilo lilifanya mashambulizi mawili ya hivi karibuni Kaskazini Mashariki mwa nchi ambayo yaliwaacha takriban watu 240 wakiwa wameuawa.

Kundi hilo limekataa msamaha uliotolewa kwao na serikali ili waweze kuacha vurugu zao ambazo zimesababisha vifo vya watu 2000 katika miaka mitatu iliyopita. Kundi la Boko Haram, limekuwa likituhumu vikosi vya usalama kwa kuwazuia kinyume na sheria jamaa za wapiganaji wa Boko Haram likisema kuwa kuachiliwa kwao itakuwa kikwazo cha kuwa na mwafaka wowote.

Kwenye kanda hiyo, Shekau hakusemna chochote kuhusu idadi ya wanawake na watoto waliokamatwa.

“tuliwakamata wanawake na watoto kadhaa pamoja na vijana barobaro,” alisema bwana Shekau.

-BBC

Ulinzi Wahimarishwa Uchaguzi Nchini Pakistan
Ulinzi ukiwa umeimarishwa nchini Pakistan

MAMILIONI ya raia wa Pakistan wanashiriki katika uchaguzi wa kihistoria utakaoonesha demokrasia katika kipindi cha mpito kwenye nchi inayomiliki silaha za nyuklia na nchi iliotawaliwa kijeshi kwa nusu ya historia yake.

Kundi la waasi la Taliban limeitaja demokrasia kuwa jambo ambalo haliendani na uislamu na wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara kwa vyama visivyoegemea misingi ya kidini na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200 katika mashambulizi yaliotajwa kuwa mabaya zaidi kwa wakati wa uchaguzi.

Hii imeongeza wasiwasi kwamba huenda kukafanyika mashambulizi katika vituo vya kupigia kura. Vituo hivyo vilivyofunguliwa saa mbili kamili asubuhi vinatarajiwa kufungwa saa kumi na moja jioni kutoa nafasi kwa takriban wapiga kura milioni 86 wanaowachaguwa wabunge 342 katika bunge la Pakistan.

Huku hayo yakiarifiwa usalama umeimarishwa nchini humo, zaidi ya maafisa wa polisi 600,000 wamesambazwa kote katika vituo 70,000 vya kupigia kura Pakistan. Uchaguzi huu unatoa nafasi ya kwanza kabisa kwa utawala uliochaguliwa na raia kumaliza muda wake na kutoa nafasi kwa utawala mwengine kuingia madarakani kupitia uchaguzi. Pakistan imekumbwa na visa vitatu vya mapinduzi na kutawaliwa kijeshi mara nne.

Kibarua kigumu kiko kati ya Nawaz Sharif na Imran Khan. Kinyan’ganyiro kikali kiko kati ya waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif ambaye pia ni kiongozi wa chama cha mrengo wa kati kulia wa (PML-N) na mchezaji bingwa wa mchezo wa Kriketi Imran Khan aliyeahidi mabadiliko nchini humo na kukomesha ufisadi iwapo atachaguliwa.

Mgombea mwingine ni Tehreek-e-Insaf wa chama cha (PTI) aliye na umri wa miaka 60 aliyeanguka siku ya Jumanne wakati alipokuwa katika harakati ya kampeni zake.

Hata hivyo kwa sasa Tehreek-e-Insaf yuko hospitalini na anakopokea matibabu baada ya kupata jeraha la uti wa mgongo na inasemekana kwamba hatoweza kupiga kura yake hii leo.

Wakati huo huo Chama tawala kinachoondoka cha mrengo wa kati kushoto PPP kimekuwa na kampeni ambazo hazikuonekana kufua dafu sana kwa kuwa mwenyekiti wake Bilawal Bhutto Zardari, anaonekana kuwa mdogo sana katika kugombea na pia amekuwa akifichwa kufuatia vitisho vya waasi wa Taliban dhidi yake.

Chama hicho cha PPP kiliwapoteza viongozi wake wakuu muanzilishi wa chama hicho Zulfikar Ali Bhutto aliyenyongwa chini ya utawala wa kijeshi mwaka wa 1979 na mtoto wake Benazir Bhutto aliyeuwawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi la kujitoa mhanga mwaka wa 2007.

Maswala muhimu ambayo utawala mpya unapaswa kuyashughulikia ni kuinua uchumi wa nchi hiyo, kutatua maswala ya kawi hali inayosababisha kukatika kwa umeme kwa zaidi ya saa 20, Juhudi inayoongozwa na Marekani ya kupambana na waasi wa itikadi kali za kiislamu, ufisadi na maendeleo ya Pakistan.

Hata hivyo wanaharakati wengi ndani na nje ya Pakistan wanajiuliza iwapo wapiga kura watajitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo kutokana na vitisho vya waasi wa Taliban kushambulia vituo vya kupiga kura. Awali msemaji wa kundi hilo Ehsanullah Ehsan aliwataka raia kususia uchaguzi wa leo ili kulinda maisha yao nchini Pakistan.

-DW

Rais wa Ujerumani Aanza Ziara Amerika Kusini
RAIS wa Ujerumani Joachim Gauck Mai 9, 2013 anaanza ziara ya siku tisa katika Bara la Amerika Kusini, ambayo itampeleka kwanza Colombia na baadae Brazil, mshirika muhimu zaidi wa Ujerumani Amerika ya Kusini.

Akiwa nchini Brazil, ambayo ndiyo taifa la sita kwa uchumi mkubwa duniani, Gauck anatarajiwa kujikita katika masuala ya kiuchumi, na nchini Colombia atazungumzia haja ya maridhiano ya kitaifa.

Serikali ya Colombia kwa sasa inashiriki mazungumzo na kundi la waasi wa “Revolutionery Armed Forces of Colombia” FARC, mchakato ambao kwa mara ya kwanza umeonyesha matumaini ya kufanikiwa. Mgororo wa nchi hiyo uliodumu kwa nusu karne sasa, umegharimu maisha ya watu karibu laki mbili, na kusababisha wengine milioni 4 kuyakimbia makaazi yao.

Gauck ambae ni mchungaji wa zamani wa kilutheri na mwanaharakati wa kupinga ukomunisti kutoka Ujerumani ya Mashariki, ana uzoefu mkubwa katika mchakato wa ushirikishwaji na anatarajiwa kuzungumzia suala hilo mara nyingi wakati wa ziara yake. Ujerumani inajiona kama mshirika katika mdahalo wa Colombia, na imekuwa ikielekeza msaada wake kwa uendelezaji wa mchakato wa amani. Ingawa hali ya haki za binaadamu nchini humo haiwezi kuchukuliwa kama isiyo na matatizo, serikali ya rais wa Colombia Juan Manuel Santos inachukuliwa kuwa katika njia sahihi kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Ujerumani.

Maridhiano miongoni mwa jamii ya Wacolombia ni sharti la kupatikana kwa mafanikio ya kiuchumi. Serikali ya Ujerumani imeikubali Colombia kuwa miongoni mwa shabaha zake za masoko, na nchi hiyo ndiyo mshirika mkuu wa Kibishara wa Colombia katika bara la Ulaya, na kimataifa, ujerumani ni nchi ya nne nyuma ya Marekani, China na Mexico.

Rais Gauck ataizuru Brazil siku ya Jumapili, ambapo masuala ya kiuchumi ndiyo yatakuwa kwenye ajenda yake. Ziara yake mjini Sao Paulo itaashiria kuanza kwa mwaka wa Ujerumani katika taifa hilo la Amerika Kusini, ambao mtangulizi wa Gauck Chritian Wulff alikubaliana na Rais wa Brazil Dilma Rousseff kuuanzisha mei 2011.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameizuru Brazil mara moja tu katika uongozi wake, mwaka 2008. Mwaka uliyopita, alifuta ushiriki wake katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu, maarufu kama Rio+20, jambo lililowasikitisha Wabrazil. Jumuiya ya wafanyabiashra wa Ujerumani nchini Brazil wangependa kumuona Merkel tena, kwa sababu nchi hiyo ndiyo mshirika imara zaidi wa kiuchumi wa Ujerumani katika Amerika ya Kusini, na Gauck anatizamiwa kusafisha njia kwa ajili ya ziara hiyo.

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff.

Gauck anaongoza ujumbe mkubwa wa kiuchumi, unaojumlisha wataalamu wa mazingira na teknolojia ya dawa, uhandisi, usafiri wa anga na usafirishaji, pamoja na wawakilishi wa sekta ya ujenzi na usanifu majengo. Wafanyabiashara wa Ujerumani wanatumaini kushiriki katika miradi ya ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014, na michezo ya olimpiki mwaka 2016 na pia katika upanuzi wa bandari za nchi hiyo.

Kuna karibu makampuni 800 ya Ujerumani yanayoendesha shughuli zake katika mji wa Sao Paulo peke yake. Mji huo unaoshikilia uchumi wa Brazil ndiyo unaochukuliwa kuwa na shughuli nyingi za viwanda vya Kijerumani nje ya Ujerumani. Lakini uchumi wa nchi hiyo ulipungua kasi na kufikia kiwango cha ukuaji cha asilimia 0.9 tu mwaka uliyopita, huku mfumuko wa bei ukiwa asilimia 5.8, na unatarajiwa kuendelea kuwa katika kiwango hicho mwaka huu.

-DW

President of the African Development Bank, on the Somalia Conference Held in London
LEADERS from more than 50 states and international organizations have gathered in London, UK to attend the Somalia Conference today on Tuesday (May 7th, 2013) with the co-chairing of Somalia President Hassan Sheikh Mohamud and UK Premier David Cameron. In light of this event, please find below an Op-Ed signed by the African Development Bank President, Donald Kaberuka (http://www.afdb.org).

It has been two decades of mayhem, chaos and bloodletting in Somalia.  A child born at the onset of the Somali crisis is now twenty one.  Somalia has still a long way to go: the Al Shabaab are defeated, but they are not yet fully eliminated, and they still have the capacity to kill and to maim.

The risks of reversal – and of humanitarian crisis – are always there, and we are not yet done with the effects of disaster.  News agency reports last week remind us of the delicate humanitarian and fragile political situation.

But while Somalia has a long way to go, it is clear that it has also come a long way. The country now – with its new Government, Parliament, President, Prime Minister and 6-point reconstruction plan – is getting to its feet.  This week’s Lancaster House Conference, convened by the UK and the Somali Government, marked a significant step on a long journey.

This is the first time in a long time that there has been such optimism, even if it is tempered by the unfinished business on the security and humanitarian front.

Pirate attacks off the coast of Somalia have fallen by three-quarters in a year.

Somali armed forces – with the help of the AU and the UN’s newly extended AMISOM mission – have reclaimed territory from the insurgents of al-Shabaab, retaking their last urban stronghold of Kismayo in October. What was the world’s largest settlement of internally displaced people at Afgoye, outside Mogadishu, has seen its numbers drop by two-thirds in a year.  Canvas is replaced by brick, and fear is replaced by hope as business picks up, from construction in Mogadishu, to mobile telephony and property.

Somalis are returning: over 60,000 came back last year alone. We estimate that two billion dollars are sent back each year. The Somali shilling has appreciated; commercial airlines are doing well; and there are nine mobile phone networks across the country.  Cargo ship arrivals in Mogadishu, seeking to regain its reputation as the white pearl of the Indian Ocean, have risen dramatically in a year.  UNICEF reports that children are going back to school in large numbers.  Somalis are not just talking with their neighbours; they are talking amongst themselves. Their commitment to dialogue with all the regions of Somalia is testimony to the potential of a collective national will.

The country of one language, one history, and one religion has more to unite it than divide it: Somalia can build itself anew. In this, the international community which turned out in force to join the Somalis at Lancaster House has a critical role to play. If it is to play an active role in Somalia, however, there are certain preconditions.

First, we must apply the lessons we have learned in post-conflict state-building in Africa and elsewhere.  The meeting on Tuesday was a good beginning.  The Somali Authorities reported on their own progress on their own plans, especially in the security sector, the judiciary, the rule of law, and the management of public finances.  These are indeed the start-points.  The Somalis must be in the driver’s seat, and be seen by all – above all their own people – to be so.

Our task is to support them as they build their own capacity, plan, and execute.  At no time should the international community want to supplant what the Somalis themselves are planning and doing.  It may be well intended, but it will not work.

Second, we need to manage the complex relationship between humanitarian agencies providing short-term emergency help, and those addressing longer-term issues of development, ‘resilience’ and reconstruction. Time has taught us that the two phases can blend and reinforce each other.

The famine and drought of 2011-12 claimed over a quarter of a million Somali lives, reminding us of the close links between security, humanitarian support and long-term resilience-building.

Thirdly, we must remember the regional context.  The Greater Horn is not only a collateral victim of the Somali crisis; it is also the bedrock of the security solution. If today we see light at the end of the tunnel, it is thanks to Kenyans, Ugandans and Burundians who have been ready to lay down their lives.  There is no solution for Somalia which does not involve the people and the countries of East Africa and the Greater Horn.

Rebuilding the Somali state will challenge us all.  There is no manual, no toolkit.  We will be learning as we go, drawing on the lessons of the past.

In London, the Somalis reported on their progress in putting in place a transparent Public Finance Management system, with a strong fiduciary framework.  It is a very good place to begin.  It is this kind of detail – and commitment – that will assure Somalis and their partners that the scarce resources available for the rebuilding Somalia will be well used.

The African Development Bank, with a uniquely African character, is already on the ground, helping to strengthen the foundations in Somalia, and to apply the lessons learned in other fragile states.

In the history of Somalia, especially the 1970s and 1980s, the outside world did not always help, and at times it actually contributed to some of the causes of the Somali crisis of the last twenty years. That is why it is essential that it supports Somalia now – and that it does so with humility.  Let us empower Somalis to take charge; let us minimize the burdens and demands on the new young State.

An immediate priority is regularizing Somalia’s relationship with the International Financial Institutions.  Let us begin by ensuring that a quick external debt arrears clearance scheme is put in place. It took three frustrating years in Liberia to clear the bilateral, multilateral and London Club debt, but Somalia’s modest debt should enable the process to go faster.

Somalia’s journey of reconstruction has begun.  It could be the most complex African journey in fifty years, but it can prove to be the most rewarding if we get it right.