Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania » Burudani http://www.thehabari.com Habari Tanzania | Online Newspaper Fri, 29 Apr 2016 10:06:04 +0000 en-US hourly 1 http://wordpress.org/?v=4.2.7 Nguli wa Muziki Papa Wemba Afariki Dunia http://www.thehabari.com/nguli-wa-muziki-papa-wemba-afariki-dunia/ http://www.thehabari.com/nguli-wa-muziki-papa-wemba-afariki-dunia/#comments Sun, 24 Apr 2016 17:46:18 +0000 http://www.thehabari.com/?p=70950 Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ...

The post Nguli wa Muziki Papa Wemba Afariki Dunia appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
wemba

Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba amefariki dunia
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.

Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu – Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,
Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.

Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa
akitumbuiza jukwaani Abidjan.

Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.

Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele, Mama,Proclamation”Chouchouna” (Papa Wemba), “Eluzam” na ” Mbeya Mbeya” (Evoloko Lay Lay), “BP ya Munu” (Efonge Gina), “Mwana Wabi” , “Mizou” (Bimi Ombale) , “Zania” (Mavuela Somo.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Nguli wa Muziki Papa Wemba Afariki Dunia appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/nguli-wa-muziki-papa-wemba-afariki-dunia/feed/ 0
Mwanamuziki Prince Afariki Dunia Akiwa na Miaka 57 http://www.thehabari.com/mwanamuziki-prince-afariki-dunia-akiwa-na-miaka-57/ http://www.thehabari.com/mwanamuziki-prince-afariki-dunia-akiwa-na-miaka-57/#comments Fri, 22 Apr 2016 04:59:57 +0000 http://www.thehabari.com/?p=70867 Mwanamuziki kutoka Marekani maarufu kwa muziki wa chapa Funk, Prince ameaga dunia. ...

The post Mwanamuziki Prince Afariki Dunia Akiwa na Miaka 57 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
160421173755_prince_2002_640x360_getty_nocredit

Mwanamuziki kutoka Marekani maarufu kwa muziki wa chapa Funk, Prince ameaga dunia. Mwanamuziki huyo raia wa Marekani alipatikana ameaga dunia katika makazi yake ya huko Minneapolis. Alikuwa na umri wa miaka 57.
Prince alitawala chati za muziki kote duniani katika miaka ya 70 na themanini kwa vibao vyake maarufu kama vile ‘I Wanna Be Your Lover’ na ‘Little Red Corvette’.

Anasifika kwa ubunifu wake wa kutajika na kwa midundo iliyowaongoa wapenzi wa muziki kote duniani .Prince alibuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock na , funk na psychedelia”.

Muziki wake ulikuwa maarufu kiasi ya kwanza aliwahi kuuza takriban albamu milioni 100. Kipawa chake kilimwezesha kutunga kusanifu kutayarisha na pia kuimba nyimbo zake mwenyewe.

Vile vile aliwatungia nyimbo waimbaji wengi tu kote duniani.Yamkini msanii huyo nguli alikuwa anaugua kwa kipindi kirefu na hata alilazimika kukatiza Shoo zake kutokana na kudhohofika kwa afya yake.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mwanamuziki Prince Afariki Dunia Akiwa na Miaka 57 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mwanamuziki-prince-afariki-dunia-akiwa-na-miaka-57/feed/ 0
Filamu Kuuzwa Mwaka 2023 Matangazo Yaanza Mwaka Huu http://www.thehabari.com/filamu-kuuzwa-mwaka-2023-matangazo-yaanza-mwaka-huu/ http://www.thehabari.com/filamu-kuuzwa-mwaka-2023-matangazo-yaanza-mwaka-huu/#comments Sat, 16 Apr 2016 19:38:59 +0000 http://www.thehabari.com/?p=70686 Watengenezaji wa filamu ya Avatar franchise wamesema kutatolewa filamu zaidi katika mwendelezo ...

The post Filamu Kuuzwa Mwaka 2023 Matangazo Yaanza Mwaka Huu appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
filama

Watengenezaji wa filamu ya Avatar franchise wamesema kutatolewa filamu zaidi katika mwendelezo huo wa filamu, filamu ijayo ikitarajiwa kutolewa 2018.

Muongozaji wa filamu hizo James Cameron ametangaza kwamba filamu hizo zitaendelezwa hadi makala ya tano itakayotolewa 2023.

Alikuwa tayari amethibitisha kwamba filamu tatu zaidi zingetolewa lakini amefichua kwamba kuna mambo mengi sana ya kuelezwa kwenye hadithi hiyo na makala zijazo tatu hazitoshi.

Kote duniani, Avatar inasalia kuwa filamu iliyofanikiwa zaidi katika historia.Filamu hiyo imezoa $2.7bn tangu kutolewa wake 2009. Filamu ijayo ya Avatar itatoka 2018, na hizo nyingine 2020, 2022 na 2023.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Filamu Kuuzwa Mwaka 2023 Matangazo Yaanza Mwaka Huu appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/filamu-kuuzwa-mwaka-2023-matangazo-yaanza-mwaka-huu/feed/ 0
Tanzia Yatanda Tasnia ya Muziki, Ndanda Kosovo Afariki Dunia http://www.thehabari.com/70431/ http://www.thehabari.com/70431/#comments Sat, 09 Apr 2016 17:05:45 +0000 http://www.thehabari.com/?p=70431 Mwananamuziki maarufu wa dansi nchini, Ndanda Kosovo amefariki dunia usiku wa kuamkia ...

The post Tanzia Yatanda Tasnia ya Muziki, Ndanda Kosovo Afariki Dunia appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
ndnda

Mwananamuziki maarufu wa dansi nchini, Ndanda Kosovo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Taarifa zinazotufikia, zinaeleza Ndanda amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo.

Tumeelezwa mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Ndanda aliyekuwa maarufu kama “Kichaa” au Mjelajela” alitamba akiwa na bendi ya FM hasa baada ya wanamuziki wake kuswekwa lupango kutokana na kukosa kibao cha kuishi nchini.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Tanzia Yatanda Tasnia ya Muziki, Ndanda Kosovo Afariki Dunia appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/70431/feed/ 0
Manamuziki Afariki Akiwa Jukwaani Akipiga Shoo http://www.thehabari.com/manamuziki-afariki-akiwa-jukwaani-akipiga-shoo/ http://www.thehabari.com/manamuziki-afariki-akiwa-jukwaani-akipiga-shoo/#comments Fri, 08 Apr 2016 05:40:24 +0000 http://www.thehabari.com/?p=70371 Huzuni na mshangao umeghubika Indonesia baada ya muimbaji maarufu Irma Bule, aliyekuwa ...

The post Manamuziki Afariki Akiwa Jukwaani Akipiga Shoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
images

Huzuni na mshangao umeghubika Indonesia baada ya muimbaji maarufu Irma Bule, aliyekuwa akiwatumbuiza mashabiki wake kuanguka na kufariki dunia jukwaani

Yamkini bi Bule aliumwa na nyoka yapata dakika 45 zilizotangulia katika ”shoo yake” iliyokuwa magharibi mwa Java Indonesia.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muimbaji huyo nyota alimkanyaga kimakosa nyoka huyo ambaye alikuwa sehemu ya ”shoo” yake na kwa bahati mbaya nyoka huyo akamuuma kwenye paja.

Japo nyoka huyo alikuwa ameng’olewa chonge zake , kwa njia moja au nyingine aliweza kum’gata na kuingiza sumu ndani ya damu yake.

Duru zinasema kuwa alipewa dawa ya kutuliza makali ya sumu lakini akakataa akidhania kuwa nyoka yule hakumdhuru.

Aliendelea na onyesho hilo akiwatumbuiza mashabiki wake hadi pale alipoanza kutapika jukwani ndipo washirika wake wakang’amua hali haikuwa nzuri.

Mara akaanza kutetemeka na kuzirai.Walipomkimbiza hospitalini daktari aliwaambia kuwa alikuwa ameshakata roho yake.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Manamuziki Afariki Akiwa Jukwaani Akipiga Shoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/manamuziki-afariki-akiwa-jukwaani-akipiga-shoo/feed/ 0
Timu ya NMB Yamkabidhi Kikombe cha Ushindi Mkurugenzi Mtendaji http://www.thehabari.com/timu-ya-nmb-yamkabidhi-kikombe-cha-ushindi-mkurugenzi-mtendaji/ http://www.thehabari.com/timu-ya-nmb-yamkabidhi-kikombe-cha-ushindi-mkurugenzi-mtendaji/#comments Mon, 04 Apr 2016 18:46:59 +0000 http://www.thehabari.com/?p=70210 NAHODHA wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard ...

The post Timu ya NMB Yamkabidhi Kikombe cha Ushindi Mkurugenzi Mtendaji appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker moja ya vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki 'Brazuka Kibenki' iliyomalizika hivi karibuni. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker moja ya vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki ‘Brazuka Kibenki’ iliyomalizika hivi karibuni. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker moja ya vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki 'Brazuka Kibenki' iliyomalizika hivi karibuni. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker moja ya vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki ‘Brazuka Kibenki’ iliyomalizika hivi karibuni. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam.

Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker kabla ya kumkabidhi vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki 'Brazuka Kibenki' iliyomalizika hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa Timu ya NMB, Bi. Josephine Kulwa pamoja na mchezaji wa NMB aliyechaguliwa kuunda kikosi cha timu ya mabenki (katikati).

Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (kushoto) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker kabla ya kumkabidhi vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki ‘Brazuka Kibenki’ iliyomalizika hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa Timu ya NMB, Bi. Josephine Kulwa pamoja na mchezaji wa NMB aliyechaguliwa kuunda kikosi cha timu ya mabenki (katikati).

Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (wa kwanza kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa tatu kulia) moja ya vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki 'Brazuka Kibenki' iliyomalizika hivi karibuni. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam. Wengine ni viongozi waandamizi wa NMB pamoja na maofisa wa benki hiyo wakishuhudia.

Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba (wa kwanza kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa tatu kulia) moja ya vikombe walivyo twaa katika Mashindano ya Ligi ya Mabenki ‘Brazuka Kibenki’ iliyomalizika hivi karibuni. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam. Wengine ni viongozi waandamizi wa NMB pamoja na maofisa wa benki hiyo wakishuhudia.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker akifurahiya moya ya vikombe alivyokabidhiwa na Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba. Wengine ni viongozi waandamizi wa NMB pamoja na maofisa wa benki hiyo wakishuhudia.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker akifurahiya moya ya vikombe alivyokabidhiwa na Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba. Wengine ni viongozi waandamizi wa NMB pamoja na maofisa wa benki hiyo wakishuhudia.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker akipiga picha ya pamoja na walioshiriki hafla ya makabidhiano ya vikombe hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker akipiga picha ya pamoja na walioshiriki hafla ya makabidhiano ya vikombe hivyo.

NAHODHA wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Benki ya NMB, Richard Mwalwiba amekabidhi rasmi vikombe vya ushindi wa Mashindano ya Ligi ya Mabenki ‘Brazuka Kibenki’ kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker ikiwa ni pamoja na kutoa shukrani kwa uongozi wa benki hiyo kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa timu yake.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, ambapo uongozi wa timu ya mpira wa miguu ya NMB ilipofanya mazungumzo na uongozi wa Benki ya NMB kuelezea mafanikio na changamoto za mashindao hayo. Timu ya NMB ilifanikiwa kutwaa vikombe viwili katika ligi ya ‘Brazuka Kibenki’ iliyoshirikisha mabenki mbalimbali nchini Tanzania. NMB ilifanikiwa kutwaa kombe la ushindi wa tatu wa mashindano hayo pamoja na Kikombe cha Timu Bora iliyojipanga vizuri katika ushiriki wa mashindano hayo.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe hivyo, Nahodha Mwalwiba alisema timu yake ilifanikiwa kupata ushindi baada ya kujiandaa vizuri kimashindano ikiwa ni pamoja na nidhamu kwa wachezaji na kuzingatia mazoezi na maelekezo ya Kocha wa timu, Mohamed Hussein (Machinga) ambaye ni nyota wa zamani wa mpira wa miguu nchini.

Alisema kikosi chake mbali na kufanikiwa vikombe hivyo pamoja na medali za shaba pia kilifanikiwa kutoa Mchezaji Bora wa Mashindano na mfungaji bora, Ahmed Nasoro pamoja na kutoa wachezaji bora watatu walioenda kuunda kikosi kimoja cha timu ya mabenki. Alishauri mashindano yajayo timu za mabenki kuzingatia kanuni za mashindano na kuacha kuchezesha wachezaji ambao hawana sifa ili ligi kuleta msisimuko zaidi.

Kwa upande wake Meneja wa Timu ya NMB, Bi. Josephine Kulwa alisema ili kujiweka vizuri katika mashindano yajayo tayari wachezaji wote wa NMB wameanza mazoezi ya aina mbalimbali chini ya wakufunzi wa mazoezi. “…Sisi tupo fiti muda wote kimichezo, tunavyozungumza hivi sasa tayari wachezaji wanafanya mazoezi yote kujiweka vizuri zaidi,” alisema Bi. Kulwa.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Timu ya NMB Yamkabidhi Kikombe cha Ushindi Mkurugenzi Mtendaji appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/timu-ya-nmb-yamkabidhi-kikombe-cha-ushindi-mkurugenzi-mtendaji/feed/ 0
Jokate na Mo Dewji Kujenga Uwanja Sekondari ya Jangwani http://www.thehabari.com/jokate-na-mo-dewji-kujenga-uwanja-sekondari-ya-jangwani/ http://www.thehabari.com/jokate-na-mo-dewji-kujenga-uwanja-sekondari-ya-jangwani/#comments Sat, 02 Apr 2016 06:08:04 +0000 http://www.thehabari.com/?p=70108 WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa ...

The post Jokate na Mo Dewji Kujenga Uwanja Sekondari ya Jangwani appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Jokate Mwegelo (kulia) akibadilishana mawazo na fundi anayejenga uwanja wa michezo Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani Dar es Salaam.

Jokate Mwegelo (kulia) akibadilishana mawazo na fundi anayejenga uwanja wa michezo Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani Dar es Salaam.

Ujenzi wa uwanja huo ukiendelea.

Ujenzi wa uwanja huo ukiendelea.

Uwanja ulivyo kabla ya ujenzi

Uwanja ulivyo kabla ya ujenzi

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa kupata uwanja wa michezo ambao unajegwa kwa ushirikiano wa Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Taasisi ya Mo Dewji.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mwanadada Jokate amesema ujenzi wa kiwanja hicho cha michezo ni sehemu ya mipango aliyokuwa nayo baada ya kuanzisha mwaka jana bonanza la Kidoti ambalo lilikuwa na malengo ya kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri kimasomo na kushiriki katika michezo ili kukuza vipaji vyao.

Jokate alisema ameamua kuanza na shule ya Jangwani kwa kutambua kuwa shule hiyo ina hosteli za wanafunzi walemavu na wamekuwa wakipata shida kupata viwanja vya michezo hivyo kupitia kiwanja hicho wataweza kushiriki michezo kwa urahisi zaidi.

“Pale Shule ya Jangwani kuna wanafunzi walio na ulemavu na kama unavyojua mlemavu anatakiwa kufanya mazoezi ili kuweka afya yake vizuri na kama wakitaka kushiriki michezo hadi waende Gymkhana lakini tunawajengea uwanja wa Basketball na Netball,” amesema Jokate wakati akifanya mahojiano na Mo Blog.

Ameongeza kuwa ili kufanikisha ujenzi huo alizungumza na Mohammed Dewji ambaye alikubali kutoa Milioni 10 kupitia Taasisi yake ya Mo Dewji na hivyo kuanza kufanyika kwa ujenzi huo ambao utawawezesha wanafunzi wa Jangwani kushiriki michezo tofauti na hapo awali.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa viwanja vya michezo utakuwa endelevu katika shule za serikali ambazo bado hazijawa na viwanja na baada ya kukamilika kwa ujenzi katika shule ya Jangwani amepanga kufanya ujenzi wa viwanja vya michezo katika Shule ya Sekondari Kinyerezi na Shule ya Sekondari Maposeni iliyopo wilayani Peramiho, Ruvuma.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Jokate na Mo Dewji Kujenga Uwanja Sekondari ya Jangwani appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/jokate-na-mo-dewji-kujenga-uwanja-sekondari-ya-jangwani/feed/ 0
Amitabh Bachchan Azoa Tuzo ya Mwigizaji Bora http://www.thehabari.com/amitabh-bachchan-azoa-tuzo-ya-mwigizaji-bora/ http://www.thehabari.com/amitabh-bachchan-azoa-tuzo-ya-mwigizaji-bora/#comments Wed, 30 Mar 2016 06:04:36 +0000 http://www.thehabari.com/?p=69967 Nyota wa filamu za Bollywood Amitabh Bachchan na Kangana Ranaut wameshinda mataji ...

The post Amitabh Bachchan Azoa Tuzo ya Mwigizaji Bora appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
big-b-amitabh-bachchan

Nyota wa filamu za Bollywood Amitabh Bachchan na Kangana Ranaut wameshinda mataji makuu katika tuzo za kitaifa za filamu nchini India.

Bachchan alishinda tuzo ya muigizaji bora kwa jukumu lake katika Piku huku Ranaut akiwa muigizaji bora upande wa wanawake kwa filamu ya Tanu Weds Manu Returns.

Tuzo ya filamu bora lilichukuliwa na Bahubali huku Sanjay Leela Bhansali akijishindia mwelekezaji bora wa filamu ya Bajirao Mastani.

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na serikali ya India.Hiyo ni tuzo ya nne ya Bachchan.Alijishindia tuzo ya muigizaji bora mwaka 1990,2005 na 2009.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Amitabh Bachchan Azoa Tuzo ya Mwigizaji Bora appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/amitabh-bachchan-azoa-tuzo-ya-mwigizaji-bora/feed/ 0
Huyu Dogo Anatisha Video Zake Zatazamwa Mara Bilioni 10 http://www.thehabari.com/huyu-dogo-anatisha-video-zake-zatazamwa-mara-bilioni-10/ http://www.thehabari.com/huyu-dogo-anatisha-video-zake-zatazamwa-mara-bilioni-10/#comments Sun, 27 Mar 2016 12:24:21 +0000 http://www.thehabari.com/?p=69875 Mwanamuziki Justin Bieber amevunja rekodi ya Vevo kwa video yake kutazamwa mara ...

The post Huyu Dogo Anatisha Video Zake Zatazamwa Mara Bilioni 10 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
justinbieber1

Mwanamuziki Justin Bieber amevunja rekodi ya Vevo kwa video yake kutazamwa mara bilioni 10.
Msanii huyo wa Canada ambaye alitoa kibao kipya Purpose in Novemba alipata idadi hiyo katika kipindi cha miaka sita na miezi mitatu au siku 2,316.

Kutazamwa kwa video zake mara bilioni 4 kulifanyika baada ya Septemba mwaka jana na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa katika kilele cha chati ya muziki katika Vevo kwa wiki 19 mfululizo.

Justin Bieber,Katy Perry na Taylor Swift ni wasanii pekee wenye video mbili tofauti zilizotazamwa zaidi ya mara bilioni moja kila moja.

Lakini video yake ya What Do You Mean?Itafikisha kutazamwa mara bilioni moja katika kipindi cha wiki chache zijazo,na kumfanya kuwa msanii wa kwanza kuwa na video tatu zilizotazamwa mara bilioni moja.

Mnamo mwezi Januari ,David Bowie alivunja rekodi ya Vevo kwa siku moja.
Video zake ziliangaliwa mara milioni 51 baada ya kutangazwa kwamba amefariki akiwa na umri wa miak 69.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Huyu Dogo Anatisha Video Zake Zatazamwa Mara Bilioni 10 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/huyu-dogo-anatisha-video-zake-zatazamwa-mara-bilioni-10/feed/ 0
Mwanamuzi wa Nyimbo za Injili Malawi Afariki Dunia http://www.thehabari.com/mwanamuzi-wa-nyimbo-za-injili-malawi-afariki-dunia/ http://www.thehabari.com/mwanamuzi-wa-nyimbo-za-injili-malawi-afariki-dunia/#comments Fri, 18 Mar 2016 06:44:18 +0000 http://www.thehabari.com/?p=69470 Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za Injili nchini Malawi Grace Chinga amefariki. Rafiki ...

The post Mwanamuzi wa Nyimbo za Injili Malawi Afariki Dunia appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
AA

Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za Injili nchini Malawi Grace Chinga amefariki.

Rafiki wa karibu wa familia yake, Pasta Chris Suya, amenukuliwa na gazeti la gazeti la Nyasa Times la Malawi akisema mwanamuziki huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kulalamikia maumivu makali ya kichwa.

“Tulipokea simu kwamba alikuwa anatatizwa na maumivu ya kichwa na tukakimbia kwake nyumbani. Tulimpeleka hospitali ya Queens Elizabeth ambapo, alifariki.”

Kwa mujibu wa ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook, mwanamuziki huyo alikuwa akijiandaa kuchomoa albamu mpya.

Raia wa Malawi wamekuwa wakituma salamu za rambirambi kwenye mitandao ya kijamii kumuomboleza.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mwanamuzi wa Nyimbo za Injili Malawi Afariki Dunia appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mwanamuzi-wa-nyimbo-za-injili-malawi-afariki-dunia/feed/ 0
Brazil Wapuuza Uvumi wa Maandamano Michuano ya Olimpiki http://www.thehabari.com/brazil-wapuuza-uvumi-wa-maandamano-michuano-ya-olimpiki/ http://www.thehabari.com/brazil-wapuuza-uvumi-wa-maandamano-michuano-ya-olimpiki/#comments Sat, 12 Mar 2016 19:45:46 +0000 http://www.thehabari.com/?p=69128 Maafisa nchini Brazil wamepuuza vitisho vya kuzuka maandamano makubwa wakati wa michezo ...

The post Brazil Wapuuza Uvumi wa Maandamano Michuano ya Olimpiki appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
olimp

Maafisa nchini Brazil wamepuuza vitisho vya kuzuka maandamano makubwa wakati wa michezo ya Olimpiki, licha ya mgogoro wa uchmi na kisiasa na sakata linalochipuka la ufisadi katika kampuni ya serikali ya mafuta, Petrobas

Waziri wa UIinzi wa Brazil Aldo Rebelo anasema anatarajia kuwa maafisa wa usalama 85,000, wakiwemo wanajeshi 38,000 watatosha kuhakikisha usalama wakati wa mashindano hayo ya Rio de Janeiro kuanzia Agosti tano hadi 21.

Baadhi ya makundi ya wakaazi wa Rio de Janeiro wameahidi kuandamana tena wakati wa michezo hiyo, hasa yale yanayowawakilisha watu walioachwa bila makaazi kutokana na miradi ya ujenzi kwa ajili ya Olimpiki.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Brazil Wapuuza Uvumi wa Maandamano Michuano ya Olimpiki appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/brazil-wapuuza-uvumi-wa-maandamano-michuano-ya-olimpiki/feed/ 0
Proin Promotions Ltd Yajivunia Washindi Wawili Tunzo za Africa Magic 2016 http://www.thehabari.com/proin-promotions-ltd-yajivunia-washindi-wawili-tunzo-za-africa-magic-2016/ http://www.thehabari.com/proin-promotions-ltd-yajivunia-washindi-wawili-tunzo-za-africa-magic-2016/#comments Tue, 08 Mar 2016 09:02:59 +0000 http://www.thehabari.com/?p=68808 Single Mtambalike akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika uwanja ...

The post Proin Promotions Ltd Yajivunia Washindi Wawili Tunzo za Africa Magic 2016 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Single Mtambalike akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika uwanja wa Mwl Nyerere
 Baadhi ya wadau na wapenzi wa filamu wakiwa uwanja wa ndege wakimsubiri kumpokea Mshindi wa Tunzo ya Filamu bora ya Kiswahili Single Mtambalike katika shindano la Africa Magic lililofanyika nchini Nigeria Mwishoni mwa wiki
wapenzi wakisubiri mshindi
 Wapenzi wa filamu wakimsubiri Single kwa hamu

Familia ya Single Mtambalike
akipokelewa na familia
Mwakilishi wa Proin Promotions.Josephat Lukaza akiongea na wanahabari kuhusiana na filamu za Proin kunyakua tunzo hizo katika Kinyangiro cha AMVCA2016.Picha Zote na Josephat Lukaza
Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Proin Promotions Ltd Yajivunia Washindi Wawili Tunzo za Africa Magic 2016 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/proin-promotions-ltd-yajivunia-washindi-wawili-tunzo-za-africa-magic-2016/feed/ 0
Pacquiao Apata Pingamizi la Kisiasa Juu ya Pambano lake Kurushwa Kwenye Runinga http://www.thehabari.com/pacquiao-apata-pingamizi-la-kisiasa-juu-ya-pambano-lake-kurushwa-kwenye-runinga/ http://www.thehabari.com/pacquiao-apata-pingamizi-la-kisiasa-juu-ya-pambano-lake-kurushwa-kwenye-runinga/#comments Tue, 08 Mar 2016 07:32:56 +0000 http://www.thehabari.com/?p=68784 Mkali na Bingwa wa ndondi Mfilipino ambaye ni mwanasiasa Manny Pacquiao amelitetea ...

The post Pacquiao Apata Pingamizi la Kisiasa Juu ya Pambano lake Kurushwa Kwenye Runinga appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Manny Pacquiao v Timothy Bradley

Mkali na Bingwa wa ndondi Mfilipino ambaye ni mwanasiasa Manny Pacquiao amelitetea pigano lake lijalo na mwanamasumbwi Mmarekani Timothy Bradley dhidi ya madai kuwa litakiuka sheria za kampeni kabla ya uchaguzi unaokuja wa Mei

USP BOXING: TIMOTHY BRADLEY JR. VS MANNY PACQUIAO S BOX USA NV

Tume ya Uchaguzi Ufilipino imepokea malalamishi kuwa pigano la Pacquiao mnamo Aprili 9, litakalorushwa nchini Ufilipino na kote ulimwenguni, litampa faida isiyo ya haki ya kupata umaarufu kupitia vyombo vya habari.

Walalamishi wanahoji kuwa pigano hilo linapaswa kuahirishwa hadi baada ya uchaguzi wa Mei 9. Hata hivyo mawakili wa Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 wamejibu kuwa pigano hilo siyo “shughuli ya kisiasa inayoegemea upande wowote”

2

Wanasema nia yake ya kushiriki pigano hilo, ambalo huenda ikawa mara ya mwisho kwake kupanda ulingoni, hailengi kumpa faida yoyote isiyo ya haki. Badala yake ni kitu cha kuipa nchi na watu wake fahari na sifa wanayostahili, kabla ya bondia huyo kuumaliza ujana wake.

Pacquiao anakabiliwa na kibarua kikali cha kushinda kiti katika baraza la Seneti baada ya uchunguzi wa maoni kuonyesha kuwa alipoteza uungwaji mkono kufuatia matamshi yake ya kupinga ushoga aliyotoa kwenye televisheni moja nchini humo katikati ya mwezi uliopita.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Pacquiao Apata Pingamizi la Kisiasa Juu ya Pambano lake Kurushwa Kwenye Runinga appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/pacquiao-apata-pingamizi-la-kisiasa-juu-ya-pambano-lake-kurushwa-kwenye-runinga/feed/ 0