Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania » Habari za Nyumbani http://www.thehabari.com Habari Tanzania | Online Newspaper Thu, 04 Feb 2016 19:16:23 +0000 en-US hourly 1 http://wordpress.org/?v=4.2.7 Waajiriwa Waomba Serikali Kudhibiti Rushwa Maofisini http://www.thehabari.com/waajiriwa-waomba-serikali-kudhibiti-rushwa-maofisini/ http://www.thehabari.com/waajiriwa-waomba-serikali-kudhibiti-rushwa-maofisini/#comments Thu, 04 Feb 2016 07:59:10 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66894 Na Woinde Shizza,Arusha Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa ...

The post Waajiriwa Waomba Serikali Kudhibiti Rushwa Maofisini appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Mkurugenzi wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Agrey Mlimka  akiwa anafafanua jambo katika mkutano wa siku moja wa kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili waajiri mkutano uliowashirikisha  waajiri kutoka katika sekta mbalimbali uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo palace jijini Arusha leo

Mkurugenzi wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Agrey Mlimka akiwa anafafanua jambo katika mkutano wa siku moja wa kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili waajiri mkutano uliowashirikisha waajiri kutoka katika sekta mbalimbali uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo palace jijini Arusha leo

Na Woinde Shizza,Arusha

Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na kimataifa.

2

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri (ATE), Aggrey Mlimuka akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi za ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi

3

Mkurugenzi huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.

4

Kwa upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje.

Baadhi ya Wanachama wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wakiwa wanajadili  kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na jinsi ya kuzitatua.

Baadhi ya Wanachama wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wakiwa wanajadili kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na jinsi ya kuzitatua.

5

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Waajiriwa Waomba Serikali Kudhibiti Rushwa Maofisini appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/waajiriwa-waomba-serikali-kudhibiti-rushwa-maofisini/feed/ 0
Madiwani Halmashauri ya Arusha DC Wilaya ya Arumeru Wapitisha Taarifa Halmashauri Hiyo http://www.thehabari.com/madiwani-halmashauri-ya-arusha-dc-wilaya-ya-arumeru-wapitisha-taarifa-halmashauri-hiyo/ http://www.thehabari.com/madiwani-halmashauri-ya-arusha-dc-wilaya-ya-arumeru-wapitisha-taarifa-halmashauri-hiyo/#comments Wed, 03 Feb 2016 19:53:32 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66871 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha DC wilaya ya Arumeru mkoa wa ...

The post Madiwani Halmashauri ya Arusha DC Wilaya ya Arumeru Wapitisha Taarifa Halmashauri Hiyo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
1

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha DC wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha,Fidelis Lumato akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani,kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri,Noah Sapuk

2

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC,Noah Sapuk akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani

3

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Arusha DC wakifatilia mijadala kwenye kikao hicho

4

Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa madiwan

5

Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa madiwani

6

Diwani wa Viti Maalumu katika halmashauri ya Arusha DC,Nuru Ndossy akichangia hoja

7

Diwani wa Kata ya Mateves ,Julius Mollel akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

9

8

Picha na rweyemamuinfo.blogspot.com

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Madiwani Halmashauri ya Arusha DC Wilaya ya Arumeru Wapitisha Taarifa Halmashauri Hiyo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/madiwani-halmashauri-ya-arusha-dc-wilaya-ya-arumeru-wapitisha-taarifa-halmashauri-hiyo/feed/ 0
Rais Magufuli Aanzisha Mkoa Mpya wa Songwe…! http://www.thehabari.com/rais-magufuli-aanzisha-mkoa-mpya-wa-songwe/ http://www.thehabari.com/rais-magufuli-aanzisha-mkoa-mpya-wa-songwe/#comments Wed, 03 Feb 2016 18:23:42 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66859 Na Raymond Mushumbusi-Maelezo RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe ...

The post Rais Magufuli Aanzisha Mkoa Mpya wa Songwe…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu kuanzishwa kwa Mkoa mpya wa Songwe na Wilaya sita mpya. Picha na Raymond Mushumbusi-maelezo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu kuanzishwa kwa Mkoa mpya wa Songwe na Wilaya sita mpya. Picha na Raymond Mushumbusi-maelezo.


Na Raymond Mushumbusi-Maelezo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa Mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.

Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.

George Simbachawene alisema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.

Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.

“Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Rais Magufuli Aanzisha Mkoa Mpya wa Songwe…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/rais-magufuli-aanzisha-mkoa-mpya-wa-songwe/feed/ 0
Serikali Yasema Kila Mtanzania Atapata Bima ya Afya http://www.thehabari.com/serikali-yasema-kila-mtanzania-atapata-bima-ya-afya/ http://www.thehabari.com/serikali-yasema-kila-mtanzania-atapata-bima-ya-afya/#comments Mon, 01 Feb 2016 22:28:03 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66778 Na Raymond Mushumbusi MAELEZO SERIKALI imejipanga kutoa huduma bora za afya kwa ...

The post Serikali Yasema Kila Mtanzania Atapata Bima ya Afya appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Hamis Adrea Kigwangalla

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Hamis Adrea Kigwangalla

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

SERIKALI imejipanga kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kuwawezesha kila mwananchi kupata Bima ya Afya itakayosaidia kupata huduma bora za afya katika zahanati na hospitali mbalimbali.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Faida Mohammed Bakar (CCM) lililouliza kuwa bado kuna ukiukwaji wa huduma za afya, haki za afya na haki za uzazi katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa maswali na majibu, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kuhakikisha kuwa haki hizi zinapatikana, Serikali kwa kupitia mifumo yake, ikiwa ni pamoja na mabaraza ya weledi, kurugenzi ya uhakiki na ubora wa huduma za afya na idara mbalimbali zilizo chini ya Waziri zinatoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusiana na haki za wateja.

Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kutekeleza hili vituo vyote vya kutolea huduma za afya vina masanduku ya maoni na ofisi za malalamiko ambazo ni sehemu muhimu ambapo wateja wanaweza kupeleka malalamiko yao ili hatua zaidi zichukuliwe kukomesha na kutokomeza ukiukwaji wowote wa haki za wateja.

“ Tutawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukiuka haki za wateja kwa kupitia baraza la wauguzi na wakunga ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazostahili ili kuokoa maisha ya wananchi hasa maisha ya mama na mtoto,” Alisema Kigwangalla.

Aidha Hamis Adrea Kigwangalla amesema Wizara yake imeandaa rasimu ya Sheria ya Bima ya Afya ambayo itamuwezesha kila mwananchi kupata bima ya afya itakayomsaidia kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.

Serikali kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee inatoa mafunzo kwa Wakunga wa Jadi ambao wamekuwa wakitumika sana sehemu ambazo huduma za afya zipo mbali ili kuwezesha wananchi hao kupata huduma bora za afya kutoka kwa wakunga hao hasa katika afya ya mama na mtoto.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Serikali Yasema Kila Mtanzania Atapata Bima ya Afya appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/serikali-yasema-kila-mtanzania-atapata-bima-ya-afya/feed/ 0
Dk Kikwete Akutana na Dk Nkosazana Zuma…! http://www.thehabari.com/dk-kikwete-akutana-na-dk-nkosazana-zuma/ http://www.thehabari.com/dk-kikwete-akutana-na-dk-nkosazana-zuma/#comments Mon, 01 Feb 2016 22:22:31 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66777 RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa  Dk. Nkosazana Dlamini Zuma, ...

The post Dk Kikwete Akutana na Dk Nkosazana Zuma…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dk. Nkosazana Dlamini Zuma mara tu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dk. Nkosazana Dlamini Zuma mara tu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.

RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa  Dk. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika  katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Kufuatia uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dk. Zuma makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.
Mheshimiwa Dk. Kikwete amemshukuru Dk. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.  Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
Naye Dk. Zuma amemshukuru Dk. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na  kuwa tayari kubeba jukumu hilo. Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake. Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha katika kutekeleza majukumu yake.
Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Dk Kikwete Akutana na Dk Nkosazana Zuma…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/dk-kikwete-akutana-na-dk-nkosazana-zuma/feed/ 0
Wakimbizi 126,000 wa Burundi Wakimbilia Tanzania, UN Yasaidia…! http://www.thehabari.com/wakimbizi-126000-wa-burundi-wakimbilia-tanzania/ http://www.thehabari.com/wakimbizi-126000-wa-burundi-wakimbilia-tanzania/#comments Mon, 01 Feb 2016 22:13:38 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66774 KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa dola za Marekani ...

The post Wakimbizi 126,000 wa Burundi Wakimbilia Tanzania, UN Yasaidia…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Baadhi ya wakimbizi waliopo katika kambi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma

Baadhi ya wakimbizi waliopo katika kambi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa dola za Marekani milioni 100 (US$ 100m, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220) kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha. Tanzania—ambayo kihistoria imepokea mamilioni ya wakimbizi kutoka nchi jirani kwa miaka mingi—imetengewa dola za Marekani milioni 11 (Sawa na shilingi za Tanzania bilioni 24) kutoka katika kiasi hicho kwa lengo la kushughulikia mahitaji ya wakimbizi kutoka Burundi.

liu

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa msaada katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara mkoani humo

Zaidi ya raia 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini. Tanzania hivi sasa ina zaidi ya wakimbizi 193,000. Kutokana na ukweli kwamba takribani wakimbizi 1,500 wanawasili nchini kila wiki, inabashiriwa kwamba huenda idadi jumla ya wakimbizi ikafikia 230,000 hadi mwisho wa mwaka 2016. Hali hii inasababisha changamoto nyingi hasa katika kutoa msaada na kinga ya kutosha kwa wakimbizi.

Mchango huu mkubwa kutoka CERF utakuwa muhimu sana katika kutoa misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli katika mkoa wa Kigoma, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, na vilevile kwa jamii za wenyeji ambazo zinahitaji kwa haraka huduma bora za maji safi, usafi wa kutosha, matunzo ya afya, chakula na makazi. Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kushughulikia mlipuko uliopo wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeathiri mikoa 19 nchini. Fedha za CERF kwa hiyo zitasaidia kuhakikisha kwamba maeneo muhimu zaidi katika dharura yanafanyiwa kazi na kwamba wakimbizi wanapewa kinga na huduma za msingi.

“Shirika la Kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) linakaribisha mchango huu wenye ukarimu mkubwa kutoka CERF ambao unakuja katika kipindi mwafaka kabisa. Utoaji msaada kwa wakimbizi ulikuwa ukikabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha katika mwaka 2015, hali iliyoathiri sana uwezo wetu wa juhudi za pamoja katika mwaka 2015. Tuna imani kwamba hii ni ishara ya kwanza kwa upatikanaji wa fedha nyingi zaidi kwa utoaji msaada katika mwaka 2016. Kwa hakika, mchango huu utasaidia kuziba upungufu mkubwa uliojitokeza katika wito wetu wa sasa na hivyo kushughulikia mahitaji makubwa zaidi ya wakimbizi na jamii za wenyeji,” alisema Mwakilishi wa UNHCR nchini Tanzania, Bi. Joyce Mends-Cole.

Kadiri mahitaji ya kiutu yanavyoongezeka, mchango kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) umetoa matumaini ya kuendelea kushughulikia dharura ya wakimbizi kutoka Burundi. Tangu mwaka 2006, Nchi 125 Wanachama wa Umoja wa Mataifa na waangalizi, wahisani kutoka sekta binafsi na serikali katika kanda zinazohusika wameendelea kuusaidia Mfuko huo hadi sasa. CERF hadi sasa imetoa jumla ya dola za Marekani bilioni 4.2 (US$ 4.2bn, sawa na shilingi za Tanzania trilioni 9) kwa miradi ya kiutu katika nchi 94. CERF hupokea michango ya hiyari katika mzunguko wa mwaka ili kutoa msaada wa kifedha kwa hatua za kiutu za kuokoa uhai. CERF inapata fedha zake kutoka kwa washirika wengi huku michango mingi zaidi ikitoka: Uingereza, Swideni, Norwei, Uholanzi na Kanada.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Wakimbizi 126,000 wa Burundi Wakimbilia Tanzania, UN Yasaidia…! appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/wakimbizi-126000-wa-burundi-wakimbilia-tanzania/feed/ 0
Naibu Waziri Atoa Kauli Kali Juu ya Utatuaji wa Matatizo Mpaka wa Holili http://www.thehabari.com/naibu-waziri-atoa-kauli-kali-juu-ya-utatuaji-wa-matatizo-mpaka-wa-holili/ http://www.thehabari.com/naibu-waziri-atoa-kauli-kali-juu-ya-utatuaji-wa-matatizo-mpaka-wa-holili/#comments Mon, 01 Feb 2016 12:23:28 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66760 Na; Ferdinand Shayo, Arusha. Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano ...

The post Naibu Waziri Atoa Kauli Kali Juu ya Utatuaji wa Matatizo Mpaka wa Holili appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki Susan Kolimba akiteta jambo na Meneja wa  Mamlaka ya Kukusanya kodi nchini Kenya (KRA) Dan Nyambaka katika ziara yake aliyoifanya mpaka wa Holili kati ya Kenya na Tanzania mwishoni mwa wiki.

Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Susan Kolimba akiteta jambo na Meneja wa
Mamlaka ya Kukusanya kodi nchini Kenya (KRA) Dan Nyambaka katika ziara yake aliyoifanya mpaka wa Holili kati ya Kenya na Tanzania mwishoni mwa wiki.

Na; Ferdinand Shayo, Arusha.
Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Susan Kolimba amezitaka mamlaka zinazofanya kazi katika mpaka kati ya Kenya na Tanzania wa Holili kuhakikisha kuwa wanatatua matatizo ya uchache wa wafanyakazi, uhaba wa vitendea kazi ili kuhakikisha kuwa wanatatua kero za wananchi wanaofanya biashara na shughuli za kijamii katika ukanda wa Afrika mashariki.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara yake mwishoni mwa wiki katika mpaka wa Holili ambapo alizungumza na wafanyakazi wa vitengo mbali mbali vya serikali ikiwemo TBS,TFDA,Uhamiaji,Polisi pamoja na idara nyingine ambazo ziliwasilisha changamoto zao mbele ya waziri huyo ambaye aliahidi kuzifikisha kwa mamlaka husika ili ziweze kutatuliwa.

“Tunahitaji kuboresha huduma katika mipaka ili biashara zienfdelee na kukuza mahusiano mazuri katika jumuiya ya Afrika mashariki “ Alisema Kolimba

Mkaguzi wa TFDA ,Edward Mwamilawa amesema kuwa licha ya unyeti wa mpaka huo bado ofisi yake inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kitaalamu vya kupima ubora wa vyakula na vipodozi jambo ambalo linazorotesha utendaji hivyo ameiomba serikali isaidie kitengo hicho ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Mkuu wa kituo cha TRA mpaka wa Holili Mwaikalobo Aden na Afisa wa Mamlaka ya Kukusanya kodi nchini Kenya (KRA) Dan Nyambaka wamesema kuwa ukusanyaji wa mapato katika mpaka huo umekua ukiongezeka kutokana na biashara inayofanyika kati ya Tanzania na Kenya .

Kuanzishwa kwa kituo kimoja Mpakani (One Stop Border Post) kimerahisisha upatikanaji wa huduma za kiutawala na kurahisisha biashara kati ya nchi Mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Naibu Waziri Atoa Kauli Kali Juu ya Utatuaji wa Matatizo Mpaka wa Holili appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/naibu-waziri-atoa-kauli-kali-juu-ya-utatuaji-wa-matatizo-mpaka-wa-holili/feed/ 0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ashiriki Ibada ya Kumuingiza Madarakani Askofu Shoo http://www.thehabari.com/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-ashiriki-ibada-ya-kumuingiza-madarakani-askofu-shoo/ http://www.thehabari.com/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-ashiriki-ibada-ya-kumuingiza-madarakani-askofu-shoo/#comments Mon, 01 Feb 2016 08:23:19 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66752 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili ...

The post Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ashiriki Ibada ya Kumuingiza Madarakani Askofu Shoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
5

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

2

Baadhi ya waalikwa walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

3

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

4

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ashiriki Ibada ya Kumuingiza Madarakani Askofu Shoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-ashiriki-ibada-ya-kumuingiza-madarakani-askofu-shoo/feed/ 0
Wanafunzi Wa Sekondari Arusha Wapewa Elimu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa http://www.thehabari.com/wanafunzi-wa-sekondari-arusha-wapewa-elimu-ya-mabadiliko-ya-hali-ya-hewa/ http://www.thehabari.com/wanafunzi-wa-sekondari-arusha-wapewa-elimu-ya-mabadiliko-ya-hali-ya-hewa/#comments Mon, 01 Feb 2016 07:21:26 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66748 Mkurugenzi wa Utafiti Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dr.Ladislaus Chang`a ...

The post Wanafunzi Wa Sekondari Arusha Wapewa Elimu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
IMG_7535

Mkurugenzi wa Utafiti Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dr.Ladislaus Chang`a akizungumza na mamia ya wanafunzi wa shule ya sekondari Arusha juu ya jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

IMG_7538

Mkurugenzi wa Utafiti Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dr.Ladislaus Chang`a akizungumza na mamia ya wanafunzi wa shule ya sekondari Arusha juu ya jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Picha na Ferdinand Shayo

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Wanafunzi Wa Sekondari Arusha Wapewa Elimu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/wanafunzi-wa-sekondari-arusha-wapewa-elimu-ya-mabadiliko-ya-hali-ya-hewa/feed/ 0
Rais Magufulia Alaani Mauaji ya Rubani wa Helkopta Simiyu http://www.thehabari.com/rais-magufulia-alaani-mauaji-ya-rubani-wa-helkopta-simiyu/ http://www.thehabari.com/rais-magufulia-alaani-mauaji-ya-rubani-wa-helkopta-simiyu/#comments Sun, 31 Jan 2016 19:38:42 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66714 Jiunge nasi kwenye social media Facebook Instagram Youtube Twitter

The post Rais Magufulia Alaani Mauaji ya Rubani wa Helkopta Simiyu appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Rais Magufulia Alaani Mauaji ya Rubani wa Helkopta Simiyu

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Rais Magufulia Alaani Mauaji ya Rubani wa Helkopta Simiyu appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/rais-magufulia-alaani-mauaji-ya-rubani-wa-helkopta-simiyu/feed/ 0
Waziri Makamba Atoa Mabati 300 kwa Waliokumbwa na Mafuriko http://www.thehabari.com/waziri-makamba-atoa-mabati-300-kwa-waliokumbwa-na-mafuriko/ http://www.thehabari.com/waziri-makamba-atoa-mabati-300-kwa-waliokumbwa-na-mafuriko/#comments Sun, 31 Jan 2016 19:24:36 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66713 Na Raisa Said, Bumbuli WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ...

The post Waziri Makamba Atoa Mabati 300 kwa Waliokumbwa na Mafuriko appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
January Makamba

January Makamba

Na Raisa Said, Bumbuli

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na Mazingira,January Makamba ametoa msaada wa mabati 300 kwa wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.

Nyumba hizo zilikuwa 40 ikiwemo Kanisa na Msikiti zimeezuliwa mapaa katika kijiji cha Msamaka kilichopo wilayani Bumbuli kufuatia Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha.

Mvua hiyo imesabisha kaya hizo kukosa mahali pa kuishi, huku wengi wa waathirika wakipewa hifadhi kwenye nyumba za majirani
zao. Akizungumza na waandishi wa habari hapo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Msamaka Mbazi Shemhando alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo January 27 mwaka huku saa kumi jioni.

Alitaja sehemu zilizo athirika zaidi kuwa ni Vitongoji vya Kwemchaa, Nazareti, CCM, Kwakorosi pamoja na kitongoji cha Kwamingojo ndio
vimeweza kuathirika na maafa hayo.

Hata hivyo aliongeza kuwa waathirika watukio hilo Kwa sasa wamehifadhiwa kwenye nyumba za Jirani wakati utaratibu mwingine wa
kuwasaidia ukiendelea kuwekwa. Akikabidhi msaada huo Makamba alisema kuwa kutokana na tukio hilo anatanguliza msaada huo kwanza wakati akiendelea kutafuta msaada
zaidi.

“Nimejikusanya Kwa hiki kidogo ili kiweze kusaidia pale penye uhitaji Kwa haraka wakati tukiendelea na utaratibu mwingine” alisema Makamba. Makamba aliwataka wananchi wote kupanda miti ili kuepuka upepo mkali unaosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Waziri Makamba Atoa Mabati 300 kwa Waliokumbwa na Mafuriko appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/waziri-makamba-atoa-mabati-300-kwa-waliokumbwa-na-mafuriko/feed/ 0
Ada Elekezi Shule Binafsi Yaendelea Kufanyiwa Kazi http://www.thehabari.com/ada-elekezi-shule-binafsi-yaendelea-kufanyiwa-kazi/ http://www.thehabari.com/ada-elekezi-shule-binafsi-yaendelea-kufanyiwa-kazi/#comments Sun, 31 Jan 2016 18:47:09 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66700 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema suala la ada elekezi linaendelea kufanyiwa kazi ...

The post Ada Elekezi Shule Binafsi Yaendelea Kufanyiwa Kazi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema suala la ada elekezi linaendelea kufanyiwa kazi na Serikali na likifika hatua nzuri litahusisha wadau wote ili kupata maoni yao. Ametoa ahadi hiyo Januari 31, 2016 wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumuingiza kazini Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Onaeli Shoo iliyofanyika kwenye usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Dk. Shoo ambaye alisema kama Serikali inataka kuondoa ada elekezi haina budi kuziimarisha shule zake ili ziwe kama zilivyokuwa zamani.

Akijibu hoja kuhusu miundombinu ya reli, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua miundombinu hiyo na kwamba hivi sasa inafanya mapitio ili kujua gharama halisi kwa maeneo husika. Alisema Serikali imepanga kuanza na maeneo manne ambapo la kwanza alilitaja kuwa ni reli ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza – Tabora – Kaliua – Mpanda hadi Karema.

“Eneo la pili ni reli ya ukanda wa Kaskazini ambayo itatoka Dar es Salaam – Tanga – Arusha hadi Musoma. Ya tatu ni ya kutoka Tabora – Kahama – Kigali (Rwanda) na kuishia nchini Burundi ambayo tunataka isaidie kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam. Reli ya nne ni ile ya kutoka Mtwara kupitia Tunduru kwenda Songea hadi Mbamba Bay,” alisema.

Kuhusu ulinzi wa demokrasia ndani ya Bunge, Waziri Mkuu alisema anakubaliana na Askofu Dk. Shoo juu ya mihimili yote mitatu kuheshimiana na kwamba ameshukuru kwamba ameonya juu ya lugha zinazotumika ndani ya Bunge.

“Bunge ni eneo linaloweza kujenga jamii mpya kwa sababu Bunge ni kioo na jamii ya Watanzania inatuangalia sisi tuliomo mle. Ni vema tuwe na lugha nzuri, tabia njema na hata jinsi tunavyovaa ili wanaotuona wapate hamu ya kuiga,” alisema.

Kuhusu ombi la kuibuliwa upya mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alisema suala hilo amelichukua na anaenda kulifanyia kazi. “Nakuhakikishia Baba Askofu ushauri ulioutoa kwa Serikali tumeupokea,” alisisitiza.

Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Shoo alisema Bunge ni nyumba ya demokrasia kwa hiyo jamii inatarajia kuona hoja zikijadiliwa kwa haki na amani badala kutumia ubabe na mabavu au nguvu ya dola.

“Nimewaona baadhi ya wabunge mko hapa… hili ninalolisema ni lenu na linawahusu ninyi na spika wenu. Wabunge tunzeni heshima yenu na Mungu awasaidie kulitimiza hilo. Wewe Waziri Mkuu ni Msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni kwa hiyo una kazi ya kusimamia. Kila mhimili unapaswa utunze heshima yake…,” alisisitiza.

Kuhusu Katiba mpya, Askofu Dk. Shoo alisema Watanzania wengi wana kiu ya kuona mchakato huo ukiibuliwa upya na kukamilishwa ili nchi ipate Katiba mpya yenye kukidhi kiu ya watu wake na inayoheshimu matakwa ya wengi.

“Mchakato huo ukianza utumike kuganga majeraha yote yaliyopita. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali ya Awamu ya Tano kuipelekea nchi yetu kule ambako imedhamiria. Yote yanawezekana tukitaka na tukipenda,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Askofu ambaye amemaliza muda wake wa kuliongoza kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa alisema anamshukuru Mungu kwa kupata kibali cha kushuhudia Mkuu mpya wa kanisa hilo akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwake.

“Si kwa akili na uwezo wangu bali ni kwa uweza wa Mungu kwamba nimeweza kuishuhudia siku ya leo. Ninamuomba Mungu akusaidie kuongoza kanisa hili, akusaidie kukemea na kuonya kwa upole. Najua Mungu atakupunguzia hata marafiki kwa sababu ya matamshi utakayokuwa ukiyatoa, lakini si wewe bali ni uweza wa Bwana na roho mtakatifu anayekuongoza,” alisema.

Aliahidi kuendelea kuwaombea Rais Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa katika majukumu waliyonayo. “Msiogope kwa ajili ya majukumu mliyopewa, msihofu tunaendelea kuwaombea kwa sababu tuko pamoja na sisi ni sehemu ya utumishi wa Taifa,” alisema.

Waziri Mkuu anarejea Dodoma jioni hii kuendelea na vikao vya Bunge.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Ada Elekezi Shule Binafsi Yaendelea Kufanyiwa Kazi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/ada-elekezi-shule-binafsi-yaendelea-kufanyiwa-kazi/feed/ 0
Waziri Mkuu Majaliwa Akuta ‘Madudu’ Hospitali ya Mawenzi Moshi http://www.thehabari.com/waziri-mkuu-majaliwa-akuta-madudu-hospitali-ya-mawenzi-moshi/ http://www.thehabari.com/waziri-mkuu-majaliwa-akuta-madudu-hospitali-ya-mawenzi-moshi/#comments Sun, 31 Jan 2016 18:41:26 +0000 http://www.thehabari.com/?p=66697 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kilimanjaro na kufanya ziara kushtukiza kwenye ...

The post Waziri Mkuu Majaliwa Akuta ‘Madudu’ Hospitali ya Mawenzi Moshi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Hospitali ya Rufaa Mawenzi mjini Moshi, Kilimanjaro.

Hospitali ya Rufaa Mawenzi mjini Moshi, Kilimanjaro.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kilimanjaro na kufanya ziara kushtukiza kwenye hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali ya mkoa huo. Waziri Mkuu Majaliwa ambaye mara baada ya kuwasili Ikulu ndogo ya Moshi mjini Januari 30, 2016 alipangiwa kupokea taarifa ya mkoa huo, alimweleza Mkuu wa mkoa huo kwamba anataka kufanya ziara katika hospitali hiyo na kuwaomba radhi watendaji waliokuwa wanasubiri taarifa ya mkoa iwasilishwe.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu ameamua kufanya ziara katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali yetu ya mkoa na atakuja kupokea taarifa ya mkoa wetu tukishatoka huko,” alisema Mkuu wa mkoa huo, Bw. Amos Makalla.

Mara baada ya kuwasili hospitalini, Waziri Mkuu alielekeza apelekwe kwenye chumba cha upasuaji (theatre) huku akimuuliza maswali kadhaa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Bingileki Lwezaula. Katika chumba cha upasuaji ilibainika kuwa kuna vyumba vitatu vya kufanyia upasuaji lakini kinachotumika ni kimoja tu kwa sababu vingine havina dawa za kulaza wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji (anesthesia) licha ya kuwa jengo la upasuaji lina mwaka sasa tangu lilipozinduliwa Februari, 2015 na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Akiwa katika wodi ya utabibu ya wanawake, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya kukosekana kwa dawa hospitalini hapo. Afisa Muuguzi wa wodi hiyo, Bi. Anjela Mwakalile alisema wametuma maombi ya kupatiwa dawa kutoka MSD lakini bado hazijafika.

Hali hiyo ilijitokeza pia kwenye wodi ya watoto. Akizungumza na wazazi wa watoto aliowakuta wamelazwa, mama mmoja alimweleza Waziri Mkuu kwamba sera ya Taifa inasema watoto wachanga hadi walio na miaka mitano wanapaswa kupata matibabu bure, lakini wao hapo hospitalini wanalazimika kununua dawa. Waziri Mkuu alimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako kubadili haraka mfumo wa uagizaji wa dawa baada ya kupokea maelezo ya Dk. Lwezaula kwamba wametuma maombi MSD tangu miezi miwili iliyopita lakini hadi sasa hawajaletewa dawa walizoomba.

“RMO ni kwa nini hamuwezi kuagiza dawa nyingi (bulk) kwa magonjwa ambayo mnajua yanajirudia mara kwa mara ili wagonjwa weu wasipate usumbufu? Hii ni hospitali ya mkoa na mgao wa dawa unaopaswa kuja hapa ni wa level ya mkoa? Haiwezekani mnafanya hivyo ili wagonjwa wajinunulie dawa kutoka kwenye maduka yenu?,” alihoji Waziri Mkuu.

“Hii hospitali ni kubwa kuliko idadi ya wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa na hii ni kwa sababu wengi wao wanaishia kwenye hospitali za wilaya. Kwa hiyo mlipaswa kuwa na dawa za kutosha. Wodini nimekuta wagonjwa wachache katika wodi nilizopita, ina maana mna ahueni hapa… mnao madaktari wa kutosha, wataalamu 12, lakini ni kwa nini hakuna dawa za kutosha?” alihoji.

Wakati akitoka wodi ya watoto, kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Hussein ambaye anauguza mgonjwa wake hospitalini hapo alimweleza Waziri Mkuu kwamba dawa pekee wanayopatiwa kwenye hospitali hiyo ni paracetamol tu.

“Hapa dawa ya bure pekee unayopata ni paracetamol tu. Dawa nyingine zote unaandikiwa ukanunue maduka ya nje. Na ukizipata ni kati ya sh. 60,000/- hadi 70,000/- kwa mkupuo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Severine Kahitwa apeleke maombi ya kupatiwa mafundi wa mashine za xray haraka iwezekanavyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kukuta mashine kubwa kwenye chumba cha mionzi cha hospitali haifanyi kazi na inayofanya kazi ni ndogo haiwezi kufanya baadhi ya vipimo.

Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kitengo cha Radiolojia, Dk. Ephraim Minja alisema: “Tuliambiwa spare parts zimekwama bandarini, na vifaa hivyo vikipatikana vitaweza kutatua tatizo lililopo.”

Alipoulizwa na Waziri Mkuu kabla ya mashine ya kuharibika alikuwa akihudumia wagonjwa wangapi, Dk. Minja alisema kwa wastani alikuwa akihudumia wagonjwa 60 hadi 70. “RAS fuatilia mafundi kwa Katibu Wizara ya Afya. Hii ni hospitali kubwa tena ya Serikali kwa hiyo haiwezekani wagonjwa waje hapa na kuambiwa waende kupata vipimo mtaani,” alisema.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Waziri Mkuu Majaliwa Akuta ‘Madudu’ Hospitali ya Mawenzi Moshi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/waziri-mkuu-majaliwa-akuta-madudu-hospitali-ya-mawenzi-moshi/feed/ 0