Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania » Michezo na Burudani http://www.thehabari.com Habari Tanzania | Online Newspaper Tue, 09 Feb 2016 23:33:33 +0000 en-US hourly 1 http://wordpress.org/?v=4.2.7 Hofu Yatanda Barcelona Baada ya Messi Kukutwa na Tatizo la Figo http://www.thehabari.com/hofu-yatanda-barcelona-baada-ya-messi-kukutwa-na-tatizo-la-figo/ http://www.thehabari.com/hofu-yatanda-barcelona-baada-ya-messi-kukutwa-na-tatizo-la-figo/#comments Tue, 09 Feb 2016 13:09:34 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67135 Mshambuliaji wa kilabu ya Barcelona Lionel Messi alikosa mazoezi siku ya jana ...

The post Hofu Yatanda Barcelona Baada ya Messi Kukutwa na Tatizo la Figo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
messi

Mshambuliaji wa kilabu ya Barcelona Lionel Messi alikosa mazoezi siku ya jana Jumatatu ili kupimwa figo yake.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikosa kucheza mechi ya nusu fainali ya kilabu bingwa duniani baada ya kupatikana na tatizo la figo,baada ya kuwa na maumivu ya tumbo yanayosababishwa na mawe ndani ya figo.

Hatahivyo alifanikiwa kushiriki katika fainali ya michuano hiyo siku tatu baadaye na ameichezea timu yake katika mechi zake zote za ligi.

Taarifa ya kilabu ya Barcelona imesema kuwa Messi mwenye umri wa miaka 28 atarudi katika hali yake ya kawaida siku ya jumatano.

”Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi atafanyiwa vipimo kadhaa Jumatatu na Jumanne ili kubaini hali ya tatizo hilo la figo alilopata mwezi Disemba”,ilisema.

Messi amefunga mabao 12 katika mechi 17 za ligi ya La Liga msimu huu na kuisaidia Barcelona kupanda pointi tatu juu ya jedwali la ligi hiyo.

Alicheza dakika 90 siku ya jumapili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya kilabu iliopo chini ya jedwali ya Levante.

Siku ya Jumatano ,Barcelona itaitembelea Valencia katika awamu ya pili ya nusu fainali ya Kombe la Copa del Rey ambapo wanaongoza kwa jumla ya mabao 7-0.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Hofu Yatanda Barcelona Baada ya Messi Kukutwa na Tatizo la Figo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/hofu-yatanda-barcelona-baada-ya-messi-kukutwa-na-tatizo-la-figo/feed/ 0
Zouma Hataonekana Dimbani tena Hadi Msimu Ujao http://www.thehabari.com/zouma-hataonekana-dimbani-tena-hadi-msimu-ujao/ http://www.thehabari.com/zouma-hataonekana-dimbani-tena-hadi-msimu-ujao/#comments Tue, 09 Feb 2016 13:03:19 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67131 Beki wa klabu ya Chelsea Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa ...

The post Zouma Hataonekana Dimbani tena Hadi Msimu Ujao appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
zouma

Beki wa klabu ya Chelsea Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia goti kwenye mchezo dhidi ya Manchester United.

Zouma, atafanyiwa upasuaji kwenye kwenye goti lake ambalo aliumia Jumapili uwanjani Stamford Bridge baada ya kutua vibaya aliporuka kupiga mpira kwa kichwa.

Uchunguzi umethibitisha kwamba aliumia vibaya na hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kutibu tatizo hilo.

Kawaida, Mchezaji akipata majeruhi ya aina hii, basi huwa nje ya uwanja si chini ya Miezi hivyo mchezaji huyu atakosa michezo yote ya msimu uliobaki.

Zouma, ambaye amekuwa kama pacha wa John Terry uwanjani, ameichezea Chelsea mechi 32 msimu huu. Ameshaichezea Ufaransa mechi 2 za Kimataifa.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Zouma Hataonekana Dimbani tena Hadi Msimu Ujao appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/zouma-hataonekana-dimbani-tena-hadi-msimu-ujao/feed/ 0
Kamusoko Ampiku Tambwe, Baada ya Kutangazwa Kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi http://www.thehabari.com/kamusoko-ampiku-tambwe-baada-ya-kutangazwa-kuwa-mchezaji-bora-wa-mwezi/ http://www.thehabari.com/kamusoko-ampiku-tambwe-baada-ya-kutangazwa-kuwa-mchezaji-bora-wa-mwezi/#comments Tue, 09 Feb 2016 12:54:24 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67127 Mchezaji Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom ...

The post Kamusoko Ampiku Tambwe, Baada ya Kutangazwa Kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Kamusoko

Mchezaji Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Disemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga (Amissi Tambwe).

Kamusoko ameisaidia timu yake ya Yanga katika michezo iliyochezwa mwezi Disemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi wa Disemba.

Kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Kamusoko Ampiku Tambwe, Baada ya Kutangazwa Kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/kamusoko-ampiku-tambwe-baada-ya-kutangazwa-kuwa-mchezaji-bora-wa-mwezi/feed/ 0
Yanga Kutimuka Kesho Kwenda Kuivaa Cercle De Joachim http://www.thehabari.com/yanga-kutimuka-kesho-kwenda-kuivaa-cercle-de-joachim/ http://www.thehabari.com/yanga-kutimuka-kesho-kwenda-kuivaa-cercle-de-joachim/#comments Tue, 09 Feb 2016 12:45:51 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67124 Kikosi cha Yanga SC kitaanza safari ya kuelekea Mauritius kesho (Jumatano) alfajiri ...

The post Yanga Kutimuka Kesho Kwenda Kuivaa Cercle De Joachim appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Jerry Muro-Afisa habari klabu ya Yanga

Jerry Muro-Afisa habari klabu ya Yanga


Kikosi cha Yanga SC kitaanza safari ya kuelekea Mauritius kesho (Jumatano) alfajiri kwenda kukipiga mchezo wa awali wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Cercle De Joachim ya nchini humo.

Yanga itaondoka Dar kuelekea Mauritius ikiwa na kikosi cha wachezaji 21, viongozi wa 7 wa benchi la ufundi pamoja na mkuu wa msafara Ayoub Nyenzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Wachezaji ambao hawato safari na timu ni Geofrey Mwashiuya, Benedict Tinoco ambao wanashughulikia passport ao za kusafiria pamoja na Matteo Anthony ambaye hayuko vizuri kiafya.

Mchezo wa Yanga dhidi ya Cercle De Joachim umepangwa kuchezwa siku ya Jumamosi February 13 saa 9:30 alasiri kwa saa za Mauritius na utasimamiwa na waamuzi kutoka Madagascar wakati match commissioner anatoka Msumbiji.

Kwa mujibu wa afisa habari wa Yanga Jerry Muro, mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Yanga hakita rejea moja kwa moja nchini bali kitaendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuhezwa February 20 mwaka huu.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Yanga Kutimuka Kesho Kwenda Kuivaa Cercle De Joachim appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/yanga-kutimuka-kesho-kwenda-kuivaa-cercle-de-joachim/feed/ 0
DR Congo Wapokelewa Zaidi ya Mfalme, Baada ya Kutwaa Ndoo http://www.thehabari.com/dr-congo-wapokelewa-zaidi-ya-mfalme-baada-ya-kutwaa-ndoo/ http://www.thehabari.com/dr-congo-wapokelewa-zaidi-ya-mfalme-baada-ya-kutwaa-ndoo/#comments Mon, 08 Feb 2016 19:13:36 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67109 Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamelakiwa ...

The post DR Congo Wapokelewa Zaidi ya Mfalme, Baada ya Kutwaa Ndoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
1

Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamelakiwa kwa shangwe na nderemo katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa.

Hii ni baada yao kutwaa ubingwa wa Afrika katika michuano ya wachezaji wanaochezaji ligi za nyumbani (CHAN).

2

Raia wa nchi hiyo walijitokeza katika barabara za miji kuwakaribisha wachezaji hao.

3

Michuano ya mwaka huu iliandaliwa nchini Rwanda.
4

DR Congo walitwaa ubingwa kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali.

Taifa hilo ndilo la pekee kutwaa ubingwa wa CHAN mara mbili.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post DR Congo Wapokelewa Zaidi ya Mfalme, Baada ya Kutwaa Ndoo appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/dr-congo-wapokelewa-zaidi-ya-mfalme-baada-ya-kutwaa-ndoo/feed/ 0
StarTimes Wachezesha Droo ya Kwanza Kumtafuta Mshindi http://www.thehabari.com/startimes-wachezesha-droo-ya-kwanza-kumtafuta-mshindi/ http://www.thehabari.com/startimes-wachezesha-droo-ya-kwanza-kumtafuta-mshindi/#comments Sun, 07 Feb 2016 20:50:54 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67054  Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ...

The post StarTimes Wachezesha Droo ya Kwanza Kumtafuta Mshindi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia). 

Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).

 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo, akichezesha droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia) akiandika namba ya mshindi wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo.
 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo akizungumza na mshindi kwa njia ya simu aliyepatikana wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 
Na Dotto Mwaibale
 
MKUU wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa cha mkoani Iringa ambacho ni chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadeta Killian (50) amefanikiwa kuibuka mteja wa kwanza mwenye bahati kwa kujinyakulia tiketi ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga kutoka kwa kampuni ya StarTimes katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza kwa njia ya simu Profesa Killian baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi amesema kuwa anayo furaha isiyoelezeka kupata taarifa hiyo ya ushindi ambao hakufikiria kama kuna ofa hiyo nzuri kwa wateja.
 
“Ninajisikia furaha kwa kutangazwa kuwa mshindi kwani sikutarajia kama wateja wa StarTimes tunaweza kupewa kubwa kiasi hiki ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ‘Live’. Naweza kusema mwaka umeanza vizuri kwa kuonyesha dalili ya neema kama hii, ni fursa kubwa kwangu mimi kama mteja kwani kuna maelefu ya wateja ambao wangependa kupata fursa hii.  Nawashukuru kwa hili kwani wameliendesha zoezi bila ya upendeleo na sisi wateja wao tunafurahi na kuwapongeza sana na tutandelea kuwaunga mkono.” Alieleza Profesa Killian
 
Mshindi huyo wa kwanza wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’ alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Super ambacho ni shilingi 36,000/- katika dishi. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi 5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.
 
“Ningependa kutoa wito kwa wateja wenzangu waendelee kujiunga kwani bado nafasi zimebaki kushindaniwa na zote zipo kwa ajili yao, hivyo wasilaze damu. Ninaahidi kuitumia fursa hii ipasavyo kwa kuenda kutazama wenzetu wa ulaya wanafanya nini kwa upande wa soka kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukitazama kupitia kwenye luninga, pongezi tena kwa StarTimes kwa kuifanya ligi ya Bundesliga ionekane kupitia ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuipa ligi hiyo umaarufu nchini kwani sasa kwa kiasi kikubwa michezo yote inaonekana ‘Live’ na kufuatiliwa na watu wengi.” alihitimisha Mkuu huyo wa Chuo cha Ualimu Mkwawa
 
Naye kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa, “Hii si mara ya kwanza sisi kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa kuwazawadia wateja wetu ni zawadi mbalimbali, hivyo basi huu ni muendelezo tu wa ofa nyingi zinazoendelea kumiminwa kwa wateja wetu waaminifu. Safari hii wateja wetu tumeamua kuwazawadia safari itakayolipiwa gharama zote na kampuni kwenda Ujerumani kutazama ligi ya Bundesliga ambayo kwa Afrika ndio kampuni pekee yenye hakimiliki ya kuionyesha ‘Live’.”
 
“Makubaliano baina ya wamiliki wa ligi hiyo ya Ujerumani na kampuni ya StarTimes yaliingiwa kwa dhumuni kubwa la kuifanya ligi hiyo maarufu barani Afrika kama ligi zingine. Na ni kwa kupitia StarTimes pekee hilo linaweza kufanikiwa kutokana na wingi wa wateja wetu, ubora wa huduma na gharama nafuu ambazo mwananchi yoyote wa kipato cha chini anaweza kuzimudu,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo basi nampongeza mshindi wa leo na nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga nasi au walipie vifurushi vyao ili waingie kwenye droo ya bahati nasibu na kujishindia safari hii kubwa kwenda Ulaya kutazama mechi moja kwa moja pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni.”
 
Akielezea machache kutokana na ushuhuda wake baada ya kupata fursa ya kutembelea ofisi za Bundesliga na kushuhudia mechi kadhaa nchini Ujerumani, Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda, ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli za michezo, amesema kuwa, “Bahati ya kupata safari ya kwenda Ujerumani ni fursa kubwa sana kwa wateja na ningependa waitumie vema. Kuna mengi tu ya kujifunza licha ya kufurahia safari hiyo. Wenzetu wamepiga hatua kubwa na tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao, hivyo nawasihi waitumie vemam ili waje kutuhadithia na sie huku.”
Zoezi zima la uchezeshwaji wa droo ya bahati nasibu ya kumpata mshindi ilichezeshwa kwa uwazi na haki mbele ya waandishi wa habari ikishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post StarTimes Wachezesha Droo ya Kwanza Kumtafuta Mshindi appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/startimes-wachezesha-droo-ya-kwanza-kumtafuta-mshindi/feed/ 0
DR Congo Watwaa Ubingwa wa CHAN 2016 Nchini Rwanda http://www.thehabari.com/dr-congo-watwaa-ubingwa-wa-chan-2016-nchini-rwanda/ http://www.thehabari.com/dr-congo-watwaa-ubingwa-wa-chan-2016-nchini-rwanda/#comments Sun, 07 Feb 2016 20:11:00 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67050 JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndiyo mabingwa wa Michuano ya Ubingwa ...

The post DR Congo Watwaa Ubingwa wa CHAN 2016 Nchini Rwanda appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
CHAN

JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndiyo mabingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.

Hiyo inafuatia kuifunga Mali mabao 3-0 katika fainali ya michuano ya mwaka huu Uwanja wa Amahoro, Kigali, nchini Rwanda.

Elia Meschack alifunga dakika ya 28 na 62 kabla ya Jonathan Bolingi kufunga la tatu dakika ya 73 kuifanya DRC itwae taji la pili katika fainali za nne tangu kuanzishwa kwa CHAN.

Ikumbukwe DRC ndiyo mabingwa wa fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

DRC wamerudia mafanikio ya mwaka 2009 walipotwaa ubingwa wa fainali za kwanza za CHAN nchini Ivory Coast

chan

Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Ivory Coast iliifunga mabao 2-1 Guinea na kunyakua Medali ya Shaba.

Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na Mohamed Youla aliyejifunga dakika ya 33 na Gbagnon Anice Badie dakika ya 35, wakati la Guinea lilifungwa na Aboubacar Leo Camara dakika ya 86.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post DR Congo Watwaa Ubingwa wa CHAN 2016 Nchini Rwanda appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/dr-congo-watwaa-ubingwa-wa-chan-2016-nchini-rwanda/feed/ 0
Chelsea Yaponea Chupuchupu Kuchezea Kichapo Darajani http://www.thehabari.com/chelsea-yaponea-chupuchupu-kuchezea-kichap-darajani/ http://www.thehabari.com/chelsea-yaponea-chupuchupu-kuchezea-kichap-darajani/#comments Sun, 07 Feb 2016 19:56:53 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67040 Timu ya Chelsea imenusurika kuchezea kichapo wakiwa nyumbani katika uwanja wa Stanford ...

The post Chelsea Yaponea Chupuchupu Kuchezea Kichapo Darajani appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
1

Timu ya Chelsea imenusurika kuchezea kichapo wakiwa nyumbani katika uwanja wa Stanford Bridge baada ya kulazimisha dare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester United walitangulia kupata bao kupitia kwa Jesse Lingard dakika ya 61kisha Costa akainusulu Chelsea dakika za nyongeza

3
2

4

5

6

7

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Chelsea Yaponea Chupuchupu Kuchezea Kichapo Darajani appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/chelsea-yaponea-chupuchupu-kuchezea-kichap-darajani/feed/ 0
Wenger: Nikiwafikilia Leicester City Kichwa Kinauma http://www.thehabari.com/wenger-nikiwafikilia-leicester-city-kichwa-kinauma/ http://www.thehabari.com/wenger-nikiwafikilia-leicester-city-kichwa-kinauma/#comments Sun, 07 Feb 2016 19:30:28 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67027 Mara baada ya ushindi leo wa mabao 2-0 dhidi ya Bournemouthkocha wa ...

The post Wenger: Nikiwafikilia Leicester City Kichwa Kinauma appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
wenger

Mara baada ya ushindi leo wa mabao 2-0 dhidi ya Bournemouthkocha wa Arsenal Asene Wenger Amedai sasa akili yote ipo katika mchezo wao dhidi ya vinara wa ligi hiyo Leicester City mchezo utakaopigwa Wiki ijayo, Magoli ya Arsenal yalifungwa na Mesut Ozilpamoja na Alex Oxlade-Chamberlain.

1

3

4

30F7E3C500000578-0-image-a-38_1454853598864

asee2

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Wenger: Nikiwafikilia Leicester City Kichwa Kinauma appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/wenger-nikiwafikilia-leicester-city-kichwa-kinauma/feed/ 0
Ndani ya Dimba la Kambarage Simba Yaikarisha Kagera Sugar http://www.thehabari.com/ndani-ya-dimba-la-kambarage-simba-yaikarisha-kalisha-kagera-sugar/ http://www.thehabari.com/ndani-ya-dimba-la-kambarage-simba-yaikarisha-kalisha-kagera-sugar/#comments Sun, 07 Feb 2016 18:54:56 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67023 SIMBA imezoa pointi tatu za ugenini baada ya kuifunga Kagera Sugar bao ...

The post Ndani ya Dimba la Kambarage Simba Yaikarisha Kagera Sugar appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
simb

SIMBA imezoa pointi tatu za ugenini baada ya kuifunga Kagera Sugar bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mkoni Shinyanga.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 42 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara huku Yanga wakifikisha pointi 43 na kubaki kileleni.

Bao la Simba lilifungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 44 akipokea krosi ya Hamis Kiiza ambaye baadaye kocha wa Simba Jackson Mayanja aliamua kumtoa baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi nafasi yake ilichukuliwa na Brian Majwega.

Simba ilifika mara nyingi langoni mwa wapinzani wao lakini kukosa umakini kuliwakosesha mabao mengi huku Mayanja akiwatoa pia Hija Ugando na Mwinyi Kazimoto nafasi zao zilichukuliwa na Danny Lyanga na Emery Nimubona.

Kocha wa Kagera Sugar, Adolf Rishard naye alifanya mabadiliko ambapo aliwatoa Martin Lupart, Mbaraka Yusuph na George Kavila aliyeumia nafasi zao zilichukuliwa na Babu Ally, Idd Kurachi na Ramadhan Kiparamoto.

Simba ilipata penalti dakika ya 83 baada ya Ajibu kuangushwa eneo la hatari ambapo Ajibu alilazimika kupiga penalti hiyo lakini kipa wa Kagera Sugar, Andrew Ntala alipangua.

Mwamuzi wa mchezo huo, Mathew Akrama kutoka Mwanza alitoa kadi nyekundu dakika ya 90 kwa mchezaji wa Kagera Sugar, Jumanne Daudi kwa kile kilichoelezwa ni kumjibu vibaya mwamuzi huyo.

Kadi nyingine za njano zilikwenda kwa Job Ibrahim baada ya kumchezea rafu Mwinyi Kazimoto pamoja na Abdi Banda naye alipewa kadi hiyo.

Simba wataendelea kuwepo mkoani Shinyanga wakisubiri mechi yao dhidi ya Stand United itakayochezwa Jumamosi ya wiki ijayo kabla hawajarudi Dar es Salaam kucheza na Yanga.

Matokeo ya mechi zingine:

JKT Ruvu 0-4 Yanga
Azam 1-0 Mwadui
Mbeya City 0-0 Prisons
Ndanda 1-1 Mtibwa
Majimaji 1-0 Mgambo
Toto Africans 2-1 Coastal

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Ndani ya Dimba la Kambarage Simba Yaikarisha Kagera Sugar appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/ndani-ya-dimba-la-kambarage-simba-yaikarisha-kalisha-kagera-sugar/feed/ 0
Yanga Yainyeshea JKT Ruvu Mvua ya Mabao Uwanja wa Taifa http://www.thehabari.com/yanga-yainyeshea-jkt-ruvu-mvua-ya-mabao-uwanja-wa-taifa/ http://www.thehabari.com/yanga-yainyeshea-jkt-ruvu-mvua-ya-mabao-uwanja-wa-taifa/#comments Sun, 07 Feb 2016 18:34:47 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67017 Na shaffihdauda.com JKT Ruvu imekubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa Yanga ...

The post Yanga Yainyeshea JKT Ruvu Mvua ya Mabao Uwanja wa Taifa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
yang1

Na shaffihdauda.com
JKT Ruvu imekubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa Yanga na kuirejesha timu hiyo kwenye reli baada ya kuwa na wiki ya tabu kufuatia kupoteza mechi yake ya kwanza kwenye msimu huu kwa goli 1-0 dhidi ya Coastal Union kabla ya kubanwa na kulazimishwa sare ya kufungana bao 2-2 na Tanzania Prisons mkoani Mbeya.

yang2

Simon Msuva amefunga magoli mawili kwenye mchezo huku Issoufou Boubacar akifunga goli lake la kwanza kwenye ligi tangu ajiunge na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili mwezi January na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma aweka goli moja kambani kukamilisha ushindi wa bao nne.

yang3

JKT Ruvu wameonekana kucheza vizuri kwenye mchezo wa leo lakini walizidiwa mbinu za kimchezo na Yanga ambao walikuwa wanatumia sana wachezaji wao wa pembeni (Msuva na Kaseke) katika mashambulizi yao mengi.

yang5

Ushindi huo unaipa Yanga faida ya kuendelea kubakia kileleni mwa ligi wakiwa wamefikisha jumla ya pointi 43 baada ya kucheza michezo 18 wakifuatiwa na Simba ambao wanapointi 42 wakati nafasi ya tatu ikiwa mikononi mwa Azam yenye pointi 42 sawa na Simba lakini inafaida ya michezo miwili mkononi kutokana na kwenda Zambia kucheza mechi za kirafiki.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Yanga Yainyeshea JKT Ruvu Mvua ya Mabao Uwanja wa Taifa appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/yanga-yainyeshea-jkt-ruvu-mvua-ya-mabao-uwanja-wa-taifa/feed/ 0
Samatta Aanza Kwa Kishindo, Timu yake Yashinda 1 – 0 http://www.thehabari.com/samatta-aanza-kwa-kishindo-timu-yake-yashinda-1-0/ http://www.thehabari.com/samatta-aanza-kwa-kishindo-timu-yake-yashinda-1-0/#comments Sun, 07 Feb 2016 11:09:33 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67012 Na, Shaffihdauda.com Baada ya nyota wa Tanzania Mbwana Samatta kufanikiwa kukipiga kwa ...

The post Samatta Aanza Kwa Kishindo, Timu yake Yashinda 1 – 0 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Samatta-Genk

Na, Shaffihdauda.com
Baada ya nyota wa Tanzania Mbwana Samatta kufanikiwa kukipiga kwa mara ya kwanza kwenye klabu yake ya KCR Genk, mkali huyo ameandika ujumbe kwenye account yake ya instagram kuwashukuru wale wote wanaom-support na kumtakia mema.

Samatta ameandika ujumbe unaosomeka kama ifuatavyo: “Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru watanzania pamoja na mashabiki wangu wote wa @krc_genk_ kwa maombi na support yenu, Leo nimefanikiwa kucheza mchezo wa kwanza rasmi nikiwa na klabu yangu mpya @krc_genk_na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0”.

Kwenye mchezo huo ambao Genk ilikuwa ugenini ikicheza dhidi ya Muscron, Popa aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikos Kareli na kumaliza dakika zote zilizo salia.

Mtanzania Mbwana Samatta ameishaanza kuichezea KRC Genk ya Ubelgiji baada ya jana kuingia katika mechi ya ligi na kucheza kwa dakika 17 wakati timu hiyo ilipoivaa Mouscron na kushinda kwa bao 1-0.

saaa

Akiwa Ubelgiji, mara nyingi atakuwa akitumia usafiri wa kijamii, yaani treni. Lakini kwa shughuli za timu, Samatta atakuwa akitumia basi la wachezaji.

samata

Samatta anaonyesha ni mtu wa malengo kweli baada ya kuacha magari yake zaidi ya matatu, na kwenda kuanza kutafuta maisha upya Genk.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe, ameamua kuachana na kila kitu ukiwemo umaarufu wake mkubwa nchini DR Congo na kwenda kuanza upya nchini Ubelgiji kwa kuwa anataka kutimiza ndoto yake.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Samatta Aanza Kwa Kishindo, Timu yake Yashinda 1 – 0 appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/samatta-aanza-kwa-kishindo-timu-yake-yashinda-1-0/feed/ 0
Mwanamuziki Maurice White Afariki Dunia Akiwa na Miaka Sabini na Nne http://www.thehabari.com/mwanamuziki-maurice-white-afariki-dunia-akiwa-na-miaka-sabini-na-nne/ http://www.thehabari.com/mwanamuziki-maurice-white-afariki-dunia-akiwa-na-miaka-sabini-na-nne/#comments Sun, 07 Feb 2016 10:48:01 +0000 http://www.thehabari.com/?p=67008 Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa Soul Maurice White, aliyeanzisha kundi ...

The post Mwanamuziki Maurice White Afariki Dunia Akiwa na Miaka Sabini na Nne appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
Maurice

Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa Soul Maurice White, aliyeanzisha kundi maarufu la wanamuziki la Earth, Wind and Fire miaka ya sitini amefariki dunia.

Alijulikana kwa vibao kama vile September, Boogie Wonderland, Shining Star na After the Love has Gone.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 74 akiwa usingizini Los Angeles, kakake Verdine White amesema. Kundi hilo lilimshirikisha kakake na pia mwanamuziki Philip Bailey.

Wanamuziki hao kwa pamoja walichomoa vibao vilivyovuma sana miaka ya sabini. Kwa jumla, waliuza zaidi ya albamu milioni 90 kote duniani na kushinda tuzo sita za Grammy.

Maurice White, aliyejulikana sana kama Reese, alijiondoa Earth Wind And Fire mwaka 1995.

whit

Alifichua hadharani kwamba alikuwa akiugua ugonjwa wa kutetemeka (Parkinson) miaka mitano baadaye wakati bendi hiyo ilipokuwa ikiingizwa rasmi kwenye Rock and Roll Hall of Fame.

White pia alifanya kazi kama produsa, akifanya kazi na wanamuziki wengine maarufu kama vile Barbra Streisand, Cher na Neil Diamond.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

The post Mwanamuziki Maurice White Afariki Dunia Akiwa na Miaka Sabini na Nne appeared first on Habari | Michezo | Mahusiano | Blog Tanzania.

]]>
http://www.thehabari.com/mwanamuziki-maurice-white-afariki-dunia-akiwa-na-miaka-sabini-na-nne/feed/ 0